Cheo ni dhamana, IGP Mstaafu Mahitta ajitokeza kuaga mwili wa OCD wa Chanika

Cheo ni dhamana, IGP Mstaafu Mahitta ajitokeza kuaga mwili wa OCD wa Chanika

HIYO ndio inaitwa fainali uzeeni, watu wakiwa vijana na wakiwa na madaraka wanakuwa wanasahau kama kuna uzeek , kufa na hata kutoka madarakani, imagine mtu alikua ana nyumba kila mkoa ana mke kila mkoa na wilaya leo hii kwishnehi, tuishi tu kwa upendo amani na utulivu,kikubwa tusiwe na roho mbaya thats it. sasa hapo anapewa huduma zote na serikali je ingekua wenzangu na mimi kule mpimbwe ama namanyele siingekua tayari Innalilyhi.
 
Juzi Nilimuona pale Kunduchi aliyekuwa side kick wake akiitwa Mwansasu nae amechoka!
 
Uzuri wakati huwa hausubiri mtu, neng'eneka wee lakini wakati ukifika haina kungojana.

Leo Mahita mwili wote kwisha, hata kutembea mwenyewe hawezi.
Mtume Muhammad (SAW) pia alisema:
"Mwenyezi Mungu ameniamrisha kuwa mnyenyekevu ili mtu yeyote asimfanyie jeuri mwingine, wala yeyote asijivune mbele ya mwingine."
(Hadithi imepokelewa na Muslim)

Hii inatufundisha kuwa jeuri haifai, kwani kila mtu atapitia hatua tofauti za maisha, ikiwa ni pamoja na uzee, udhaifu, na utegemezi kwa wengine.
 
Mzee tulisoma na mwanae kwa sasa ni marehemu (alikua anapiga pombe kali) akaugua ini, halfu akili zilikua mbali sana form two alirudia kama mara 4 hivi , inaonekana Mahita alikua ana watoto kila kona ya nchi hii..Maana huyo mwanae alizikwa ujombani kwao huko kwa Wahangaza...Rest in Peace Abdul Mahita
 
Ule ubabe na kiburi Cha IGP Omarry Mahita , leo nimemuona kwenye msiba wa mtoto wa rafiki yake Chico, akitembelea magongo Kwa Uzee .

Asee cheo ni dhamana, na duniani tunapita, tuache kibri na tuishi na watu vizuri .

View attachment 3277205
Sioni hata cha kushangaza, kutembea na magongo haitokani na ubabe wake, but ni uzee, ingawa hakuacha alama nzuri
 
Wamemkagua Hana jambia kweli hapo.maaana huyo alikua ngunguri
 
Uwe mbabe usiwe mbabe wote tutazeeka panapo majaaliwa na kufariki. Ponda Raha kufa kwaja.
 
Ule ubabe na kiburi Cha IGP Omarry Mahita , leo nimemuona kwenye msiba wa mtoto wa rafiki yake Chico, akitembelea magongo Kwa Uzee .

Asee cheo ni dhamana, na duniani tunapita, tuache kibri na tuishi na watu vizuri .

View attachment 3277205
Lilikuwa jitu katili sana, lilikuwa kwenye mtandao wa kuiba magari kuyavusha Kenya, jitu ngunguri.
Kwa sasa ni kwishnei.
 
Back
Top Bottom