Chile: Mji mzima wateketea Kwa Moto, tusipuuze Manabii

Chile: Mji mzima wateketea Kwa Moto, tusipuuze Manabii

Salaam,Shalom,

Wiki mbili zimepita sasa, iliripotiwa mlipuko mkubwa wa moto Kutoka msituni uliosambaa na kutekeleza mji mzima. Watu wengi wamefariki, nyumba za mji huo kugeukia majibu kabisa,Chanzo Cha moto huo hakijafahamika Hadi sasa.

Jinsi mji huo ulivyoteketea, Si Rahisi kuamini moto Kutoka msitu wa asili ndio chanzo Cha kuteketea kwake.

Kumekuwa na ujumbe unaojirudia wa Manabii wa Mungu kuwaarifu wakazi wa Bandari salama kuhama mji huo, watu hawataki kusikia sauti ya manabii wa Mungu.

Utii ni Bora kuliko SADAKA.

Source: ALJAZEERA TV.
Kuna yule nabii wetu alituambia tulihame jiji kabla ya April na mali zote tuuze au kumpa yeye ili tubarikiwe
 
Kuna yule nabii wetu alituambia tulihame jiji kabla ya April na mali zote tuuze au kumpa yeye ili tubarikiwe
Alikwambia ana pesa za kununua Mali zote za mji mzima sio!!
 
Hata kuwaka moto mlima Kilimanjaro ungesema ni manabii..

Dini zilisha wafanya muwe wendawazimu.
 
Kumekuwa na ujumbe unaojirudia wa Manabii wa Mungu kuwaarifu wakazi wa Bandari salama kuhama mji huo, watu hawataki kusikia sauti ya manabii wa Mungu.
Naona unampigia debe jamaa.
Unafahamu Mungu anapotoa ujumbe wake kupitia nabii wake, hueleza chanzo cha tatizo, adhabu yake na suluhisho kama mkifanyia kazi chanzo cha tatizo.

Mfano Yona pale ninawi, aliwaambia wamemuasi Mungu (chanzo cha tatizo), kisha akamwambia mji mzima utateketezwa kwa moto (adhabu ) halafu akawaambia watubu kabla ya siku tatu ili kuepuka hiyo adhabu. (suluhisho)

Huyo nabii anawaambia watu wahame Dar, tena anasema wenye nyumba wauze (hao wanunuzi wao hawatakufa?). Mkuu unabii unaotoka kwa Mungu una vitu vitatu hapo juu.
 
America kusini kuna laana huko za kila aina uhuni kwa sana.
 
Naona unampigia debe jamaa.
Unafahamu Mungu anapotoa ujumbe wake kupitia nabii wake, hueleza chanzo cha tatizo, adhabu yake na suluhisho kama mkifanyia kazi chanzo cha tatizo.

Mfano Yona pale ninawi, aliwaambia wamemuasi Mungu (chanzo cha tatizo), kisha akamwambia mji mzima utateketezwa kwa moto (adhabu ) halafu akawaambia watubu kabla ya siku tatu ili kuepuka hiyo adhabu. (suluhisho)

Huyo nabii anawaambia watu wahame Dar, tena anasema wenye nyumba wauze (hao wanunuzi wao hawatakufa?). Mkuu unabii unaotoka kwa Mungu una vitu vitatu hapo juu.
Usifuate stori za wazushi,

Fuatilia vizuri hatua hizo zote zilitangazwa.
 
  • Thanks
Reactions: 511
Nabii anahusikaje hapo !! Moto una visababishi watakuja na report jinsi moto ulivyotokea ! Na kilichosababisha

Mnawapa kichwa sana hawa watu na story za unabii !! Hiyo alibahatisha tu mkeka umetiki anaenda kukamata watu akili hapo !!

Kama alitabiri kwamba moto utatokea kwanini asiombe akazuia ! au ndo mnataka kusema Mungu anashindana na watu anaojua kabisa anawazidi uwezo ! Anaona kabisa hivi ni viumbe dhaifu bado anavionesha mabavu kwa maumivu ! Anaumba watu halafu anawateketeza kwa moto for what ? Kwanini asiwaoneshe upendo wakazidi kumuamini sio kwa vitisho na adhabu ?
ISINGETOKEA UNGESEMA HAYUPO UMETOKEA UNASEMA HANA UPENDO.MUNGU ANA PRINCIPLE ZAKE LAZIMA UTEMBEE KTK KANUNI ZAKE.
 
Salaam,Shalom,

Wiki mbili zimepita sasa, iliripotiwa mlipuko mkubwa wa moto Kutoka msituni uliosambaa na kutekeleza mji mzima. Watu wengi wamefariki, nyumba za mji huo kugeuka majivu kabisa,Chanzo Cha moto huo hakijafahamika Hadi sasa.

Jinsi mji huo ulivyoteketea, Si Rahisi kuamini moto Kutoka msitu wa asili ndio chanzo Cha kuteketea kwake.

Kumekuwa na ujumbe unaojirudia wa Manabii wa Mungu kuwaarifu wakazi wa Bandari salama kuhama mji huo, watu hawataki kusikia sauti ya manabii wa Mungu.

Utii ni Bora kuliko SADAKA.

Source: ALJAZEERA TV.
Hivi lile swala la Dar Lilifikia wapi...
Ila ukiwa unaamini hivi vitu bhna
 
Yakitokea Mtasema Mungu hawapendi wakati amewatumia mjumbe kabisa kuwaasa.
Watu wa Dar tayari walishaambiwa na nabii wanaenda kuzama mwaka huu, mbona hawahami? Wewe mwenzetu unaishi wapi?
 
Back
Top Bottom