Naona hutaki kufata adabu za mjadala.
Naanzia hapa mwanzo ulikana juu ya uwepo wa uchawi. Unakubali hili au unakataa ? Naweia kiporo nukta hii.
Naanza upya kukuthibitisha ya kuwa uchawi upo,kisha nitakupa nafasi uthibitishe ya kuwa uchawi haupo. Nakuoa sharti moja kuu "Nikikuuliza swali langu lolote ujibu".
Uchawi ni nini ?
Uchawi ni kubadilisha jambo mbali na uhakika wake, nako ni kuwadhihirishia watu jambo lisilo la kweli wakaliona kuwa ni la kweli.
Pia,husemwa katika maana za Uchawi ni kila jambo lililo fichika sababu zake, linalo tokeza kwa sababu zisizo za kawaida na ndani yake mna hadaa (ghishi/uongo).
Kwanza soma kwa umakini maana hii ya Uchawi,kabla sijaendelea uliza swali ili tuweke kumbukumbu vizuri.