Chimbuko na Upotofu wa kanisa la Waadventista Wasabato

Chimbuko na Upotofu wa kanisa la Waadventista Wasabato

Of course mkuu.

Ila unapaswa kufocus kukua kiroho sio kwa kutegemea nguvu zako kushinda dhambi. hapana. Hayo yote unapaswa kuyatenda sio ili upate kuokolewa(wokovu) au uende mbinguni bali unapaswa kuyafanya kwa kuwa wewe ni kiumbe kipya ndani ya kristo baada ya roho yako kuungana na Roho wa Mungu.

Ukimpokea Roho wa Mungu hautumii nguvu kubwa kushinda hayo (japo utaanza kwa ugumu kwa kuwa mwili ni dhaifu kwa mambo ya Kimungu/Kiroho).

Aliyeamini ameokolewa/ameokoka tayari. kinachofuata ni kutembea kwa kudhihirisha ule wokovu aliuopokea kwa Kufa na kufufuka kwa Yesu.
🤝
 
Kuhusu sabato pia tangu mwanzo ilikuwa moja ya vitu vilivyofanyika kama vivuli vya yale yatakayokuja baada ya Yesu kudhihirika katika mwili.

Yote kuhusu Chakula cha jangwani(Manna),Nyoka wa Shaba,Hema la kukutania na sherehe za vibanda,Sadaka ya kondoo ni ufananisho wa Kristo ambavyo vilikoma baada ya kitu halisi(Yesu Kristo) kuja.

Baada ya kitu halisi kuja haiwezekani ukabaki na kushikilia kivuli ambacho sio kitu halisi.

Yesu aliheshimu agano la kale lakini pia hakumaanisha yale yaliyokuwa kule ni ya kushikilia bado.mifano ipo mingi ila mmoja ni kuhusu mwanamke aliyezini.

Sheria ilisema alipaswa kuuwawa lakini Yesu hakumuachia watu wampige bali aliweka mazingira ya wao kujua kwamba wenyewe pia wana dhambi zao na hawawezi kujikomboa isipokuwa kupitia yeye kwa namna alivyokuja duniani kufa kwa ajili yetu ili tusamehewe dhambi zetu.

Yesu hakutaka kuonyesha kwamba walioshika agano la kale hawakuwa na akili..hapana bali anaonyesha kuwa agano jipya ni bora zaidi kwa kuwa lina tuhakikishia msamaha wa dhambi na wokovu kwa imani na nafasi yetu sio kujiokoa bali tumeshaokolewa(tukiamini) ila tunapaswa kutembea katika mwenendo wa Kiumbe mpya baada ya roho yetu kuungana na Roho wa Mungu.

Asili yeti inakuwa ina chembe ya Mungu ndani yetu ambaye kwa Roho wake tuna nguvu na mamlaka ya kutembea sawasawa na asili mpya tulioipokea katika Kristo.

UNAZIJUA AMLI ZA MUNGU??????????
 
Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.

Danieli 7:25

ANAYEZUNGUMZWA HAPA NI U PAPA.

haya mambo yalitabiliwa agano la kale.

Kuwa huyo KIONGOZI atabadiri Kila kitu.

Kunena kinyumena ALIYE juu MUNGU.
 
soma maandiko vizuri
Elimu niliyonayo katika Dini wewe nyumbu wa kisabato huwezi kuniambia nikosome maandiko
Nyie mmesomea kuikashifu catholic ndio mnachojua😂
 
Yesu mwenyewe aliitunza sabato

Agano jipya lina anzia wapi?
-Kama Yesu asingefufuka Ukristo wetu ungekuwa ni kazi bure.

-Baada ya Yesu kufufuka alikaa duniani siku 40 akiwatokea wanafunzi wake. Niambie wapi aliwatokea siku ya Sabato?

-Sabato ni kwa ajili ya Mwanadamu na wala si mwanadamu kwa ajili ya sabato.

-Siku ya kwanza ya juma ndiyo Bwana Yesu alifufuka kuashiria dhambi/ mauti imeshindwa. Kuna Ubayo wowote hiyo kuwa ndio ika beba yote ya sabato na kumbukumbu ya ukombozi.

-Tumepewa funguo za ufalme wa Mbinguni tutakalolifungua duniani likiwa ni kwa mapenzi ya Mungu na mbinguni limefunguliwa.

-Kwa mmoja siku moja ni muhimu kwake na kwa mwengine siku zote saba.

-Pazia lilipopasuka siku ile Bwana Yesu aliposulubishwa na kufa ndio ulikuwa mwanzo kwa kila muamini kuwa na uwezo wa kuingia Patakatifu pa Patakatifu na tuna,Roho Mtakatifu maana Yesu alitupa hiyo ahadi na ikatimia siku ya Pentekosti. Kwa nini Yesu asubiri mpaka 31/10/1884 ndio angie Patakatifu pa Patakatifu?

-Huyu mama Ellen White na wenzake walitupu baada ya kusema uongo kuhusu hiyo tarehe ya mwisho wa dunia ambapo haikuwa hivyo. Hawakuona Maneno yaliyo sema hakuna ajuaye hiyo tarehe ila Baba/ Bwana Mungu wa Mbinguni??
 
Elimu niliyonayo katika Dini wewe nyumbu wa kisabato huwezi kuniambia nikosome maandiko
Nyie mmesomea kuikashifu catholic ndio mnachojua😂
Kusomea theology ..watu wengi wamesomea
Ninachosemea hapo ni usome maandiko vzuri kwa kuyaelewa

Another thing ..nani amesema wasabato wanawakashifu dhehebu fulani ?
 
Agano jipya lina anzia wapi?
-Kama Yesu asingefufuka Ukristo wetu ungekuwa ni kazi bure.

-Baada ya Yesu kufufuka alikaa duniani siku 40 akiwatokea wanafunzi wake. Niambie wapi aliwatokea siku ya Sabato?

-Sabato ni kwa ajili ya Mwanadamu na wala si mwanadamu kwa ajili ya sabato.

-Siku ya kwanza ya juma ndiyo Bwana Yesu alifufuka kuashiria dhambi/ mauti imeshindwa. Kuna Ubayo wowote hiyo kuwa ndio ika beba yote ya sabato na kumbukumbu ya ukombozi.

-Tumepewa funguo za ufalme wa Mbinguni tutakalolifungua duniani likiwa ni kwa mapenzi ya Mungu na mbinguni limefunguliwa.

-Kwa mmoja siku moja ni muhimu kwake na kwa mwengine siku zote saba.

-Pazia lilipopasuka siku ile Bwana Yesu aliposulubishwa na kufa ndio ulikuwa mwanzo kwa kila muamini kuwa na uwezo wa kuingia Patakatifu pa Patakatifu na tuna,Roho Mtakatifu maana Yesu alitupa hiyo ahadi na ikatimia siku ya Pentekosti. Kwa nini Yesu asubiri mpaka 31/10/1884 ndio angie Patakatifu pa Patakatifu?

-Huyu mama Ellen White na wenzake walitupu baada ya kusema uongo kuhusu hiyo tarehe ya mwisho wa dunia ambapo haikuwa hivyo. Hawakuona Maneno yaliyo sema hakuna ajuaye hiyo tarehe ila Baba/ Bwana Mungu wa Mbinguni??
Nionyeshe wapi Yesu hakutunza sabato??
Na ni wapi walisema baada ya agano jipya tuache kusali siku ya ibada siku ya Bwana ambayo ni sabato
 
Unabii alioandika Ellen White unatofautiana wapi na Amri za Mungu??

Walisema uongo wa hiyo tarehe ya mwisho wa Dunia/ kurudi kwa Bwana Yesu. Kwa maana hiyo alivunja ile amri "Usishuhudie Uongo." Na Biblia iko wazi kwamba nabii wa uongo utamjua akikutabiria na baadaye akikuambia fuata njia ya utabiri wake ambayo ni ya upotovu inayokutoa kwa Mungu. Kwa hiyo Wasabato wanafuata njia ya upotovu wa Ellen na wenzake, iliyosema siku ya mwisho wa dunia ni 31/10/1884 ambayo ilipita bila walichotabri kutimia.

Neno la Mungu linasema na liko wazi kuwa hatujui siku wala saa atakayorudi Bwana wa Majeshi. Sitaki kuamini Ellen na wenzslake walikuwa hawajui hili Neno, na rudia sitaki kuamini hivyo.
Sijui ni mangapi yamepotoshwa. Hilo moja ni dhahiri.
 
Nionyeshe wapi Yesu hakutunza sabato??
Na ni wapi walisema baada ya agano jipya tuache kusali siku ya ibada siku ya Bwana ambayo ni sabato

Yesu hakutunza Sabato kwani, aliponya siku ya Sabato na wanafunzi wake wakiwa naye wakachuma/vuna masuke siku ya sabato ili wale njaa ilpowakabili

Bwana Yesu alitoa ufafanuzi kwa nini alitenda alichotenda siku hiyo ya Sabato. Hii kwa mtazamo mwengine ni kuwa Sabato yaweza kuwa kama siku nyengine yeyote ili mradi dhamira yako ni njema na inatenda yaliyo mapenzi ya Mungu. Tena sehemu nyingine Neno la Mungu linasema Sabato ni kwa mwanadamu ie kwa faida ya mwanadamu na wala si sabato kwa ajili ya mwanadamu ie mwanadamu asiende mbali akaiabudu au kuinufaisha au kuitukuza sabato zaidi ya Mwenyezi Mungu maana itakuwa ni makosa/ kutenda dhambi.
Kwa sababu hiyo hiyo ndio kukawa na hili Neno la Mungu linalosema kwa mtu mmoja siku moja ni muhimu na kwa mwengine siku zote ni muhimu. Basi kama zote ni muhimu kwangu, mimi siku ya kwanza ya juma naipa umuhimuule wa Sabato na kuwa ndio itakuwa Sabato yangu,, nitafanya ibada kwa Mungu wangu siku hiyo na pia nitaitumia kama kumbukumbu ya ukombozi wangu, na kama haitoshi na mnyanganya umiliki wa siku hii shetani na wakala wake mungu jua. Hili la kuweka kuwa sasa aabudiwe Mungu wa Kweli wa Mbinguni badala ya huyu tambuzi mungu jua ndilo jambo limuuzi na kumuuma sana shetani na akanyanyua mawakala wake kuipinga jumapili ili watu wasimuabudu Kristo Bwana, maana amenyang'anywa kila kitu.
.
Nimesema hapa ninao Ufunguo wa Ufalme wa Mbinguni ambao nimepewa na Bwana Yesu. Ninaye Roho wa Kristo ndani yangu wa kuniongoza yaliyo Mapenzi ya Bwana Mungu wa Ibrahim, Isaka (si ishumaili huyu hakuwa wa mpango wa Mungu. Alikuwa wa mpango sarai, kijakazi wake na wakamshawishi Ibrahimu akatotoka nje ya mpango wa Mungu. Na ashukuriwe Mungu maana Neema yake ni Kuu na ya ajabu safari hii haikula kwa Ibrahim)na Yakobo. Nimetumia Ufunguo wa Ufalme wa Mbinguni na Roho wa Mungu aliye ndani yangu kuifanya Siku ya kwanza ya juma kwamba ndiyo Sabato yangu na pia kukumbuka Ukombozi wangu.

Neno la Mungu/ Bwana Yesu alituambia hivi kwa kutumia Jina la .Yesu "Lake" tutafanya kazi zile zote alizozifanya na kubwa zaidi ya hizo. Kazi moja ndio hiyo kuiitisha siku ya kwanza ya juma iwe ni Sabato ya Bwana hutaki unaacha uendelee kulishwa Matango pori ya kina ellen, kibwetere, na juzi kati hapo chakahola mackezie.
 
Kusomea theology ..watu wengi wamesomea
Ninachosemea hapo ni usome maandiko vzuri kwa kuyaelewa

Another thing ..nani amesema wasabato wanawakashifu dhehebu fulani ?
Wasabato mnasomea wapi hiyo theology 😂😂😂
 
Kusomea theology ..watu wengi wamesomea
Ninachosemea hapo ni usome maandiko vzuri kwa kuyaelewa

Another thing ..nani amesema wasabato wanawakashifu dhehebu fulani ?

Usipate shida mkuu.

Hapa hamnazo.

Ni Yale mapapai ya VATCAN.

JAMAA HANA KOFIA.
 
Back
Top Bottom