Nionyeshe wapi Yesu hakutunza sabato??
Na ni wapi walisema baada ya agano jipya tuache kusali siku ya ibada siku ya Bwana ambayo ni sabato
Yesu hakutunza Sabato kwani, aliponya siku ya Sabato na wanafunzi wake wakiwa naye wakachuma/vuna masuke siku ya sabato ili wale njaa ilpowakabili
Bwana Yesu alitoa ufafanuzi kwa nini alitenda alichotenda siku hiyo ya Sabato. Hii kwa mtazamo mwengine ni kuwa Sabato yaweza kuwa kama siku nyengine yeyote ili mradi dhamira yako ni njema na inatenda yaliyo mapenzi ya Mungu. Tena sehemu nyingine Neno la Mungu linasema Sabato ni kwa mwanadamu ie kwa faida ya mwanadamu na wala si sabato kwa ajili ya mwanadamu ie mwanadamu asiende mbali akaiabudu au kuinufaisha au kuitukuza sabato zaidi ya Mwenyezi Mungu maana itakuwa ni makosa/ kutenda dhambi.
Kwa sababu hiyo hiyo ndio kukawa na hili Neno la Mungu linalosema kwa mtu mmoja siku moja ni muhimu na kwa mwengine siku zote ni muhimu. Basi kama zote ni muhimu kwangu, mimi siku ya kwanza ya juma naipa umuhimuule wa Sabato na kuwa ndio itakuwa Sabato yangu,, nitafanya ibada kwa Mungu wangu siku hiyo na pia nitaitumia kama kumbukumbu ya ukombozi wangu, na kama haitoshi na mnyanganya umiliki wa siku hii shetani na wakala wake mungu jua. Hili la kuweka kuwa sasa aabudiwe Mungu wa Kweli wa Mbinguni badala ya huyu tambuzi mungu jua ndilo jambo limuuzi na kumuuma sana shetani na akanyanyua mawakala wake kuipinga jumapili ili watu wasimuabudu Kristo Bwana, maana amenyang'anywa kila kitu.
.
Nimesema hapa ninao Ufunguo wa Ufalme wa Mbinguni ambao nimepewa na Bwana Yesu. Ninaye Roho wa Kristo ndani yangu wa kuniongoza yaliyo Mapenzi ya Bwana Mungu wa Ibrahim, Isaka (si ishumaili huyu hakuwa wa mpango wa Mungu. Alikuwa wa mpango sarai, kijakazi wake na wakamshawishi Ibrahimu akatotoka nje ya mpango wa Mungu. Na ashukuriwe Mungu maana Neema yake ni Kuu na ya ajabu safari hii haikula kwa Ibrahim)na Yakobo. Nimetumia Ufunguo wa Ufalme wa Mbinguni na Roho wa Mungu aliye ndani yangu kuifanya Siku ya kwanza ya juma kwamba ndiyo Sabato yangu na pia kukumbuka Ukombozi wangu.
Neno la Mungu/ Bwana Yesu alituambia hivi kwa kutumia Jina la .Yesu "Lake" tutafanya kazi zile zote alizozifanya na kubwa zaidi ya hizo. Kazi moja ndio hiyo kuiitisha siku ya kwanza ya juma iwe ni Sabato ya Bwana hutaki unaacha uendelee kulishwa Matango pori ya kina ellen, kibwetere, na juzi kati hapo chakahola mackezie.