China: Fursa za biashara, usafiri na masoko

China: Fursa za biashara, usafiri na masoko

Nafahamu, ila nimeshasogea sana namalizia miaka michache iliyobaki ndio nistaafu. Naskilizia hili zuio la kusafiri kwa watumishi kama ndio limetukumba wote na tunaosafiri kwa gharama zetu wenyewe wakati wa likizo zetu maana ndio huwa muda wangu wa kufuata mzigo.

Polenii aisee itabidi usubiri tu
 
Vipi kuhusu masoko ya Prastic recylce naona wachina wamejazana wananunua Machupa ya uhai na Prastic mbovu
 
Mimi ninampango wa kwenda China kununua Spares za piki piki na kuja kuuza jumla na reja reja dukani kwangu nani anauzoefu na biashara hii haswa anayeenda china
 
Mimi ninampango wa kwenda China kununua Spares za piki piki na kuja kuuza jumla na reja reja dukani kwangu nani anauzoefu na biashara hii haswa anayeenda china

Mkuu mimi siuzi,ila nipo china na huwa nawapeleka ndugu zangu wanafanya hyo biashara.kama una swali ambalo liko ndan ya uwezo wangu bila shaka nitakusaidia majibu
 
Nashukuru Mkuu; Kwanza uaminifu wa wauza hizo bidhaa upoje? wanaweza wakakupa bidhaa fake bila wewe kutaka?
Mfano nikija nanunua dukani moja kwa moha au naweka order kwanza?
Nikitaka order yangu ya ubora zaidi inawezekana na gharama inakua nafuu?
Suala la wizi au ujambazi utapeli huko likoje?
Unafahamu cbm moja ni bei gani?
Ni rahisi kumtumia mtu order akaitekeleza bila mimi kuja china?
 
1.suala la uaminifu mara nyingi huwa linakuwa ni la mtu binafsi.tatizo huwa lina anza mtu anataka bidhaa bora kwa bei ya chini mno,mara nyingi wachina huwa hawakatai hela so atakacho fanya ni kukupa bidhaa inayoendana na bei yako

2.itafatana na bidhaa unayotaka kama ipo stock au la.ukiweka order it means utawaachia maelezo wakikamilisha wapeleke cargo gan kwa ajil ya usafirishaj

3.order yako inawezekana pia.bei ni makubaliano na muuzaji.ukiona kakataa katakata kushuka bei ,usilazimishe sana coz kama sio mwaminifu atachukua hela yako na kukufanyia kaz chin ya kiwango

4.security iko vzuri sana.cameras ziko mitaan pia madukan zikinasa matukio muda wote

4.cbm ina fatana na kampuni ya usafirishaji unayo itumia.ila kuna kampuni kama
Silent ocean
GNM CARGO
ZAZEME CARGO.

Bei ni kati ya 300 -400/cbm

5.uwezekano upo na baadhi ya watu wanafanya hvo.
 
thanks kwa uzoefu wako kwa ndugu zako with 10m naweza kuanza hiyo business wth profit
 
Shukrani acha nifanye tafiti ya spares za kuchukua na return yake itakuaje
 
Back
Top Bottom