China: Fursa za biashara, usafiri na masoko

mkuu hizi taarifa za silent ocean kutochukua loose cargo hazikuwa za kweli .nilifatilia na nimeweka mawasiliano yao hapa kwenye thread unaweza kuwasiliana nao moja kwa moja.
 
mkuu hizi taarifa za silent ocean kutochukua loose cargo hazikuwa za kweli .nilifatilia na nimeweka mawasiliano yao hapa kwenye thread unaweza kuwasiliana nao moja kwa moja.
Asante kiongozi wangu kwa taarifa! Wafanyabiashara wote wangekuwa na moyo mnyoofu wa kutoa msaada wa kimawazo kama wako, watu wangepiga hatua kimaendeleo! Kipilipili umekuwa wa msaada sana katika hii thread ya biashara za China, MUNGU akubariki!
 
Eti Kipilipili ni miezi ipi mizuri kwa kufanya safari za China? Yaani kuepuka baridi, mvua (hizi zinasababisha hadi land slide) n.k? Asante!
 
Wakuu wenye uelewa katika hili naomba msaada,

Ninahitaji kuwa na home industry, itayohusika na izaloshaji wa mvinyo.

mahitaji yangu ni vifaa vya kufungashia bidhaa(plastic) na kifaa cha kupimia alcohol.

Nahitaji kujua brand za mashine na bei zake
 
Eti Kipilipili ni miezi ipi mizuri kwa kufanya safari za China? Yaani kuepuka baridi, mvua (hizi zinasababisha hadi land slide) n.k? Asante!
mkuu inategemea unafanya biashara ya aina gani. kuna biashara ambazo ukija wakati wa summer masoko ni mengi na bidhaa ni nyingi mfano bidhaa kama nguo(tunazovaa nyumbani ambazo nyingi ni nyepesi na kwa huku huvaliwa wakati wa summer) ukija wakati wa winter miez ya november-march hutapata machaguo mengi kwa sababu maduka mengi yatakuwa yanauza nguo za winter. lakini pia kama wewe ni mfanyabiashara wa spare parts kuja kipindi cha baridi inaweza kukupunguzia gharama za nauli mana kipindi hiki mashirika ya ndege huwa na ofa nyingi na pia abiria wanaosafiri ni wachache kwa hiyo bei ya nauli iko chini...kwa hyo inategemea mkuu
 
mkuu tafadhali naomba unisaidie ni jins gan nitapata masoko china ili niweze kupeleka bidhaa kule I mean kamchakato kazma plz
 
uzi mzuri saana
je ile safari ya kwenda thailand imefikia wapi wakuu
 
Siko la asali sina details za soko lake hapa China.

Natoa wito kwa wengine wanaotaka ku export bidhaa zao nje ya nchi wanitumie majina ya vitu hivyo kisha nitavituma kwa wahusika
Mkuu nahitaji kufahamu juu ya kununua mtumba online kutoka china hapa namainisha belo za mtumba sijui hata pakuanzia lakini je mfano nikiwa na kianzio cha milioni tatu au nne naweza kuanzisha biashara yakuimport mzigo?
Msaada wako unahitajika kwangu hata pia mawazo
 
NIMEPATA RAFIKI/WORKMATE AMBAYE TUTAENDA NAYE NA KUNUNUA MZIGO PAMOJA NA KUJA KUUZA PAMOJA-TUTAFUNGUA DUKA K/KOO
 
#hii thread ni educative, ahsante Mkuu!!
 
Ninyi watu, Rais wenu si amekataza kusafiri? Ama?
 
Huu Uzi uko vizuri lakini kwa mtazamo inaonekana wengi tunatamani kwenda China kununua mzigo tatizo lipo kwenye mitaji.

Kwamba ni kiwango gani cha mtaji kitafaa kwenda nacho ili ukirudi uweze kumudu ushindani.

Nasikia wachina wanapunguza bei kulingana na ukubwa wa mzigo wako unaochukua,
Hivyo ni vizuri wenyewe uzoefu muwatahadharishe wanaotegemea kwenda na Pesa kidogo wakitegemea wakirudi waweze kushindana na makampuni yanayoagiza mizigo kama God one au Sunda.
Nadhani wataishia kulaumu na kupoteza mitaji yao kidogo.
 
Ni kweli mkuu suala la mtaji ni changamoto kwa wengi,japokuwa tusitishike na haya makampuni makubwa. Hata Roma haikujengwa siku moja kama watu wasemavyo.cha msingi ni kuanza na hicho hicho kidogo mtu alichonacho na akiwa ndani ya biashara tayari atagundua vingi ambavyo akiwa nje hawezi kugundua wala kuwa na tajiriba(experience) navyo.
Hawa wafanyabiashara wadogo nashauri wawe wana"segment" soko lao kwa kuangalia ni aina gani ya wateja watawahudumiwa .Hii itasaidia kupanua soko na kuwafikia wateja wa hadhi,kada na madaraja tofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…