China: Fursa za biashara, usafiri na masoko

Mkuu hongera kwa kuwapa mwanga watanzania wenzako wenye nia ya kujikwamua kibiashara, na mie niombe kupewa muongozo nahitaji kufanya biashara ya nguo za jeans za kike na kiume toka china ni mji gani naweza kupata bidhaa zenye ubora mzuri na kwa bei nzuri?
Na kingine ningependa kujua kati ya china, bangkok au hongkong ni wapi muafaka kuchukulia mzigo?
 

1. Jeans - zipo nyingi sana pale guangzhou. Lakini jeans nyingi za Guangzhou zipo na madoido ya west africa. Ukitulia katika masoko na maduka ya pale Guangzhou unaweza pata jeans nzuri sana.

2. Kila eneo lina taste zake
China - kuna kila aina ya products NZURI na MBAYA zoote zipo na unazipata kwa urahisi

Thailand - Huwa naenda kula bata, sijui kuhusu nguo za kule.

Hongkong - Iko poa sana, ina nguo nzuri sana, lakini bei zake ziko juu kidogo.


Ushauri:
- Nenda China kupitia hongkong, nunua mzigo pale. Waachie ma-agent wa kutuma mizigo kwenda TZ. Usiingie na mizigo mingi kwenda China, ni risk
- Kamata train ya haraka pale Hongkong ingia China-Guangzhou fanya manunuzi yako pale
- Nenda shenzhen mji karibu na Guangzhou fanya manunuzi yako pale, kisha rudi Guangzhou
- Funda mizigo yako, rudi Tanzania kaanze kuuza
 
Nashukuru sana kiongozi nitalifanyia kazi hili.
 
Asante mkuu. Ameen

Mkuu Kipilipili,

Nikushukuru kwa maelezo na majibu mazuri ktk thread hii. Nimesoma pages nyingi tu za uzi huu lakini naomba nikuulize maswali yafutatyo hata kama kuna sehemu (nyuma) mmezungumzia ila mimi sijaona:

1. Container dogo ili lijae linahitaji mzigo mkubwa kiasi gani na gharaza za container kutoka China mpaka Dsm ni kiasi gani kwa makadirio?
2. Kwa uzoefu wako,ni mji gani una supply stationery goods (& its accessories)+ ream papers karibia za aina zote na zinapatikana hapo kwa pamoja ikiwa ni pamoja na computer accessories, photocopiers. + wino mbali mbali (brand and used)
3. Kwa bidhaa za stationeries tajwa hapo juu nikiandaa mil.20 (ya mzigo tu) china nitapata mzigo wa kuniwezesha kuja kuuza kama supplier/wholesaler (quantity) au ni mzigo unaofaa kuuweka dukani na kuuza kama Retailer? Nataka kufahamu ni mtaji kiasi gani unaweza ukawa mzuri kufanyia biashara ya aina hii kama wholesaler (niuze kwa bei ya jumla) aua kama retailer (kununua mzigo kwa ajili ya kuuza rejareja tu)
4. Kwa uzoefu wako, ni nchi gani nje na china ambazo zina produce products tajwa hapo (with quality) juu kwa friendly price? which country between them ni nzuri kwa wajasiliamali wa kitanzania?

Mwisho, nikuombe uniPM contacts zako kama hutojali.
Thank you in advance.
 
Tumsubiri Kipilipili
 
Mkuu, je bidhaa kufuata China au kununua ktk tovuti kama Alibaba.com ipi gharama ni nafuu?
 
Gachuma jr,
Huu hapa sasa.
 
1. A) Kontena dogo ni takriban 68CBM. Hivyo ili ulijaze linahitaji CBM hizo. mfano: kwa bidhaa ya ‘rimu’ za karatsi za A4, wanafungasha rim 5 katika kila boksi 1. kwenye kontena la 20FT huwa zinaingia boksi 1,680 . Ama kama mzigo wako ni mchanganyiko yaani karatatasi na bidhaa nyinginezo kama computer nk basi zingatia tu idadi ya CBM.
B). Gharama za kontena kwa makadirio:
Hapa kuna mambo mawili; MOS, ama upeleke mzigo wako kwenye shipping company ambayo inafanya kila kitu na utapokea mzigo wako kwenye ghala lao DSM. Yaani ukishawapa mzigo China, basi wewe huhangaiki na lolote unasubiri tu mzigo wako ofisini kwao Dsm. Gharama za hii hutofautiana kutoka kampuni hadi kampuni, na pia kutoka bidhaa moja hadi bidhaa nyingine. Yaani hakuna bei jumuishi (flat rate) kwa bidhaa zote, kila bidhaa huwa na gharama yake. mfano anaeleta kontena la milango kodi yake na gharama nyingine zitakuwa tofauti na anaeingiza kontena la viatu au vifaa vya kilimo.
PILI, ‘supplier’ akusafirishie mzigo hadi bandarini Dsm na kisha wewe ufanye mwenyewe ‘clearance’.
Njia zote mbili zina faida na hasara. Njia ya kwanza faida yake ni kuwa unaepukana na usumbufu wa clearance na pia unakuwa umeshajua gharama kamili ya kusafirisha mzigo na kukitokea chochote ama gharama bandarini kupanda au vipi , wewe unakuwa huhusiki na lolote. Hivyo huwi na presha! Hasara ya njia ya kwanza ni kwamba wakati mwingine (si mara zote) gharama unayolipa inaweza ikawa kubwa kuliko kama ungefanya clearance mwenyewe. Gharama hapa najumlisha pia na gharama za usumbufu!
Ama njia ya pili, uzuri wake ni kuwa unaweza kuokoa pesa kwa gharama kuwa nafuu ukilinganisha na njia ya kwanza.
Hasara ya njia hii ni kuwa risk zote za mzigo huwa unazibeba wewe, na wakati mwingine kuna ibuka gharama nje ya mahesabu uliyopiga kabla na ndio hapo unaposikia watu wameacha mizigo yao mpaka inapigwa ‘sadakalau[emoji16]’. Pia jiandae na usumbufu na pia uwe tayari na ’KUFUNIKA KOMBE...’ (nadhani umenielewa, kama hukuelewa rudi darasani kwa mwl wako wa kiswahili[emoji16])
Ushauri wangu: Sitatoa gharama za makadirio hapa, mwanzo wa uzi niliweka mawasiliano ya makampuni, wasiliana nao ujue bei zao za sasa zikoje na ufanye ulinganifu. Pia tafuta supplier kama watatu alibaba wakupe quotations, halafu hizo quotations tafuta clearing agents bongo wakupe makadirio ya kusafirisha na kodi ikiwa utasafirisha mwenyewe. kisha fanya ulinganifu wa njia ya kwanza na ya pili.
2. Mji: Guangzhou utapata vyote ila kama unataka bidhaa nzuri nenda Yiwu.
3. Mara nyingi huwa nakwepa sana kujibu kuhusu MTAJI. Nahofia kumkatisha mtu tamaa au kumpa matumaini makubwa. 20M ni kubwa na pia ni ndogo! Itategemea wewe mwenyewe! Mfano wewe umetaja vifaa tofauti vya stationaries kama unataka ununue vyote hivyo kwa 20M basi ni ndogo na utauza rejareja tu TZ na China hutapata bei nzuri kwa sababu utakua unanunua kidogo kidogo. Lakini, kama 20M ni ya bidhaa AINA moja tu basi huwenda ukapata bei ya jumla China na ukauza jumla TZ. mfano kama utanunua rim moja china kwa dola 1, maana yake kontena dogo itakuwa lina rim 1680 X 5=8400, hivyo utalipa $8400 (sawa tsh 19,320,000) hii ni kwa bidhaa moja tu na ni EXW price yaani bei ya kiwandani tu, haujautoa mzigo hata nje ya geti la kiwanda. Pata picha sasa unataka ununue wino, computer nk.
ZINGATIA: Watanzania tumezoea ukinunua pc 2 au 3 za bidhaa tunataka tupewe bei ya jumla. China ni tofauti. Kila kiwanda huwa na Minimum Oder Quantity (MOQ), usipoifikisha hupewi bei ya jumla. Mfano wakikwambia MOQ ni rim 2000 basi hata ukinunua 1000 watakupa bei ya rejateja, wakati kwa TZ mteja hapo ni bonge la wholesaler[emoji16]!
Hivyo suala la mtaji kiasi gani, siwezi sema, itategemea wewe unataka nini na ni kwa kiwango gani! hata milioni 1 ni mtaji pia, inategemea tu na scale of business unayotaka kufanya.
4. Kuhusu nchi mbali na China, sina ufahamu wa kutosha, japokuwa Wahindi nao wamekuwa na bidhaa nzuri katika baadhi ya bidhaa.
ZINGATIA: Wengi wanataka bidhaa BORA halafu ziwe ‘friendly price’. HILI HALIWEZEKANI.
Kuna mitazamo potofu kuhusu bidhaa za china kuwa ni FAKE au za ubora wa chini. China ina bidhaa zote BORA SANA na MBAYA SANA, akili yako ukiiweka kwenye BEI TU basi utaangukia kwenye bidhaa MBAYA SANA, ukibadili vigezo vyako vya ununuzi na kuiweka akili yako kwenye UBORA wa bidhaa basi utapata bidhaa nzuri japo BEI inakuwa imechangamka kidogo.
Wafanyabiashara wengi wanataka wanunue vya bei rahisi ili waje TZ wauze bei pendwa (rahisi) bila kujua wanaharibu brand zao na watauza mwanzoni tu ila baadae wateja huambiana kuwa kwa fulani vitu vyake hovyo tu na hutawaona tena.
Za kuambiwa changanya na zako mkuu (naamini umenielewa)! Wakati mwingine kujipambanua kitofauti kibiashara ni bora kuliko kufuata mkumbo! Jifunze kupitie kampuni ya APPLE hawana presha! bidhaa yao iko ghali na wakitoa tolea jipya watu wanakesha usiku kucha kwenye foleni ili wawe wakwanza kununua! Linganisha na wale wanaouza simu ina kila kitu mpyaaaa kwa elfu 70 tu! [emoji16]
Mchina kasoma wateja na amefanya makert segmentation! Mfuko wako ndio utaamua ujiweke kwenye tapo lipo la soko ama mzingatia bei au ubora! vyote anakupa, chaguo ni lako! Nawe wasome wateja wako!
Nakutakia mafanikio mema. Pole kwa gazeti na some spelling errors muda wa kuedit sina.
 
Mkuu, je bidhaa kufuata China au kununua ktk tovuti kama Alibaba.com ipi gharama ni nafuu?
Siwezi kutoa jibu la moja kwa moja hapa mana swali lipo ‘too general’. mfano: kuna vitu vya kujiuliza kwanza kama AINA ya bidhaa, kuna aina za bidhaa unaweza kuja China mwanzoni tu na ukishaweka mambo sawa na supplier na mtu wa kukagua mzigo wako kabla haujatumwa TZ basi huwi na haja tena ya kuingia gharama za kusafiri kila mara, Au pia ukipata supplier muaminifu unaweza ukawa unanunua mtandaoni tu na huwi na haja ya kusafiri.
KIWANGO cha bidhaa. Kama kiwango cha bidhaa ni kidogo hakuna haja yakusafiri, ni bora ununue tu mtandaoni
Njia nyingine ya manunuzi ni kupitia kampuni za kitanzania zinazofanya huduma ya sourcing kutoka China. Kampuni/watu binafsi waliopo China na wana maduka/ofisi TZ unaweza kuwatumia wakakununulia na kukuletea hadi ulipo Tanzania ama kwa kukupa bei ya kiwandani kisha unawalipa service fee ya kukuhudumia na mzigo ukifika TZ unautoa mwenyewe bandarini au uwanja wa ndege AU wakununulie na kukusafirishia kila kitu na wao kuweka faida yao kidogo. Cha msingi angalia njia ipi ina nafuu kwako! Ila hakuna jibu la moja kwa moja kwamba ukinununua alibaba ni rahisi kuliko ukija china (au kinyume chake). itategemea Aina ya bidhaa, kwango cha bidhaa, njia unayotaka kusafirisha bidhaa, ukubwa wa bidhaa yenyewe , kundi la bidhaa katika malipo ya kodi (inalipiwa kodi au ina msamaha wa kodi), nani atakaehusika kusafirisha mzigo nk, haya ni mambo ya msingi kuyajua na ndio ukiyafanyia uchambuzi utabaini njia gani ni nafuu ama kununua mtandaoni au kuja mwenyewe china.

Zingatio: watanzania baadhi wanaweza wasimwamini mtanzania mwenzao aliepo china na ana kampuni TZ iliyosajiliwa halali na ana physical address Tanzania LAKINI wakamwamini mchina waliemuona alibaba tu akawatumia quotation nje ya alibaba, wakalipana nje ya alibaba, halafu mambo yakiwa hayakwenda sawa wanarudi sasa kwa watanzania waliopo china ili wasaidiwe kuwatafuta hao supplier wakichina kusolve tatizo. Yote hii wanaoana wakiwatumia wachina wanakwepa gharama!
Nashauri sana tena sana TUJIFUNZE biashara hizi za online kwanza kabla ya kuamua kuzifanya.
Pia kama zipo kampuni za kitanzania zinazosource kutokea china moja kwa moja na zenye physical address Tanzania basi ni bora kuzifanyia utafiti, na ukijiridhisha ingia nao mikataba ya kisheria na agiza kupitia wao ikiwa huna uwezo wa wewe mwenyewe kuja china.
Cases za mitandaoni zimekuwa nyingi!
 
huu uzi ni mzuri sana na nimejifunza kitu kikubwa ikiwa tunaweza kufanya export nje itakuwa tija maradufu hasa tukisafirisha bidhaa zilizo kamilika au kusafirisha bidhaa ambazo tumeziongezea thamani,mkuu keep it going
 
huu uzi ni mzuri sana na nimejifunza kitu kikubwa ikiwa tunaweza kufanya export nje itakuwa tija maradufu hasa tukisafirisha bidhaa zilizo kamilika au kusafirisha bidhaa ambazo tumeziongezea thamani,mkuu keep it going
mkuu, unachosema ni sahihi. Export watanzania wengi bado tuko nyuma, na mara zote tumekuwa watu wa kulalamika au akionekana mmoja amejaribu basi ataandamwa na ‘nipe michongo basi’, ‘ulifanyaje?’ ‘nipe deal basi’. Cha kushangaza hata ukiwapa watu taarifa hakuna anaekuwa tayari kukomaa nazo na kuzifanyia kazi ipasavyo.
Kingine ni kwamba , wengi wetu tunataka kila mtu atoke kivyake..hakuna anaeamini on joint venture wala patnership. Na ukiona imefanywa patnership basi ni ya ‘kujuana’ na mara nyingi si ya kisheria na mwisho wake watu wanashikana uchawi. udugu na urafiki unakufa.
Ngoja nikupe mfano wa wakenya jinsi walivyojiongeza kwenye export, sisi tupo tu tunabaki kulalamika ohooo sijui sera zetu za export sijui zina nini...blah blah nyiiiingiiii...
Angalia Wakenya ‘walivyojiongeza’!
Tuliowengi tunapenda shortcut! Hatuko tayari kufuata utaratibu wala "compliance". Tukipewa utaratibu tunaona mlolongo ni mreeeeefu na tunaachana nao mapema! Tumeridhika na changamoto za shamba na soko la ndani, hatujawa na utayari wa kutosha kuzikabili changamoto za nje! Wapo wachache tu, ila tuliowengi hatutaki
"kusumbuka".
Ukimtumia mkulima wa TZ file lenye kurasa 30 tu umwambie asome humo kuna fursa ya masoko ya nje, kwanza ANAWEZA HATA ASISOME KABISA! Na akisoma basi atasoma kurasa mbili tatu ataachia hapo hapo!
Halafu na yeye nae atatuma kwenye group jingine aonekane na yeye "wamo"!

Soko la nje linahitaji kufuata vigezo na masharti yake! Sisi hatuko tayari kuendana na vigezo vya wateja wa soko la nje!
Kama wakenya wananunua bidhaa TZ, Wanachokwenda kufanya kwao ni KUONGEZA THAMANI TU ili kuendana na MATAKWA ya soko la nje! Na hapa ndipo wanapotuacha nyuma!. Nitoe mfano wa packaging.
Wakenya wana packaging nzuri MNO! sisi bado hatujawa tayari kubadilika! Tukiletewa package nzuri na zenye ubora hakuna anaenunua! Tunasingizia zinauzwa ghali na kuwalaumu wanaozileta kuwa wanataka kutajirika kwa kuwaumiza wakulima! Tumezoea zile zile "yeboyebo" za bei rahisi za sh 100-250! Lakini Package ndio inayovuta na kulinasa jicho la mteja kabla hata hajajua ubora wa kilichomo ndani!

Nafahamu changamoto za mkulima ni nyingi labda "sera", pembejeo nk lakini hizi ni changamoto karibia Afrika nzima! Ila mkulima mwenyewe akiamua kwa dhati kuwa wa tofauti na kuangazia soko la nje, basi INAWEZEKANA!
Tubadili Attitude zetu! bila ya hivyo
tutaendelea kulalamika kila siku. TUJIONGEZE! Tuache blah blah nyingi, Vitendo ndio viwe vingi kuliko maneno
#MaoniTuSioSheria
 
waswahili hasa vijana husema nakuunga mkono mpaka mguu, kitu kingine ambacho hatamie nilikuja gundua tena kwakujifanyia uchunguzi mwenyewe ni ile kudhamiria toka moyoni, hilo ni swala linalotusumbua pia mtu anaweza kuona maandiko ka ulivyoandika na kufuatilia maandiko ya wengine walochangia na kutamani sana ila akitoka hapo kwa muda anasahau na hakumbuki tena ka alisema atafanya. inakuwuwa kama habari ya mpanzi na mbegu zilizo mwagika sehemu mbalimbali. kikubwa nadhani tunakila namna yakudhamiria na kuangalia soko la utoaji wa bidhaa nje ila zilizoongezewa thamani ule ujinga wakuuza ngozi elfu 20/= then tunakuja nunua kiatu 200 000/= twapaswa kuacha sasa
 
Mkuu ukitaka kwenda china Nauli tsh. Ngapi now go and return,,na utaratibu wao upoje wa kupata visa Kipilipili Na wajuvi wengine wanaojielewa,,,nna mil 20 nataka nijilipue kufuata bidhaa
 
Mkuu Kipilipili, naweza kupata plastic pollen traps baada ya muda gani kutoka kwa jamaa zako? Naomba namba yako ya simu tafadhali.
 
Check your inbox, halafu ukiwa hapa jf uwe unatumia neno MKUU ndio title mujarab, mana jinsia za watu humu ni kitendawili
Hahaha Mi Nilivyomaliza tu kusoma nikaitambua jinsia yako ...Sema sio muhimu ....Shukran Sana kwa Taarifa iliyoshiba like hii uliyetuzawadia ...
 
Asante mkuu. Ameen
Habar yako kaka, samahan kwa usumbufu mm ni msichana naitwa Sabrina,Naishi tz ila juz kat nimepata fursa ya biashara China, yan kuchukua madera tz kupeleka China kuuza ,shida yangu ni moja jinsi ya kupeleka mzigo China na changamoto zake zipoje,na je ktk pita pita zako ushawai ona biashara ya madera huko China ,na wanauza kwa yuan ngapi?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…