This time naona hujafanya utafiti wa kutosha;
Serikali ya china wana Computer operating system Original from China inaitwa "Kylin" na hii inawasaidia kuepuka udukuzi wa kimtandao. Inatumika kwa wingi inchini humo na huwa wanai market kama "OpenKylin"
Hii ndio operating system inayotumika kwa komputer karibia zote za Serikali lakini pia inatumika kwa wingi kwa raia wake japo zipo pia operating system nyingine orginal from china ambazo sio maarufu
Kuhusu Simu; China pia ina operating System orginal from China tena ni nzuri sana ufanyaji kazi wake ni somewhere btn Androd and iOS ambayo ni vigumu sana kuidukua
Inaitwa "Harmony". Nakumbuka mwishoni mwa mwaka jana walitoa latest version yake inaitwa "HarmonyNEXT" hii ni habari nyingine kabisa....
Sijui kama unafaham kuwa China wanazalisha Internet yao wenyewe.....
Lakini pia; Kuna vitu vingi sana vya technologia vipo within china kwa sababu, zaidi ya robo ya watu wa Dunia wapo kule hivyo hawatumii nguvu kubwa kutangaza huku nje....
CHINA IPO MBALI SANA NA NDIO INAWANYIMA USINGIZI WAMAREKANI.....
Hongera kwa kueleza vizuri, niliamua kuiweka mada kama ilivyo kwa makusudi kabisa.
Lakini ngoja nikwambie, simu sio vile vifaa vya nje au jina la simu. Simu ni operating system iliyopo ndani. Simu bila operating system in sawa na kopo. Hali kadhalika computer sio vile vifaa vya nje bali ni operating system iliyopo ndani. Computer bila operating system ni sawa na kopo. Simu zinazo support mfumo wa Google play service ndizo zinazo uzika kwa haraka kwenye soko la kimataifa. Na computer zinazo support mfumo wa Microsoft ndizo zinazo uzika haraka kwenye soko la kimataifa. Huawei wana simu nzuri lakini hazi support Google play service haziwezi kuuzika sana kwenye soko la nje ya China.
Ni kweli kabisa China ina mifumo yake mbadala kama ulivyo eleza na wanaitumia huko China. Lakini kwa biashara ya kimataifa ili makampuni yake ya teknolojia yafanye vizuri kwenye soko la kimataifa, bado yanategemea Google na Microsoft kwa kiwango fulani.
Google Play Store ndio jukwaa kuu la kusambaza programu kwa watumiaji wa Android duniani. Mfano ingawa Huawei imekuja na AppGallery, bado haina idadi kubwa ya programu kama Play Store.
Huduma kama
Google Maps, Gmail, YouTube, na Google Search ni muhimu kwa watumiaji wengi nje ya China. Matokeo yake, simu za Huawei na Xiaomi zinazouzwa nje ya China mara nyingi zinahitajika kuwa na huduma za Google ili kuwavutia wateja.
Windows ndiyo mfumo wa uendeshaji unaotumiwa na 70% ya kompyuta duniani. Microsoft Office ni programu muhimu kwa wafanyabiashara, wanafunzi, na mashirika duniani kote. Hivyo ingawa China ina mifumo mbadala kama NeoKylin, bado haina ushawishi mkubwa nje ya China.
Lakini sio hivyo tu, seva nyingi zinazoendesha huduma kubwa za kimataifa zinategemea teknolojia za Marekani. Hata kampuni za Kichina, kama TikTok, zimejaribu kuweka data nje ya China ili kuendana na mahitaji ya soko la kimataifa.
Hivyo simu na computer zinazo milikiwa na makamapuni ya kichina zenye mifumo kama HarmonyOS na AppGallery na
NeoKylin ili ziweze kushindana na simu na computer zenye mifumo ya Google Play Store na Microsoft Windows, hapo inawahitaji makampuni ya kichina yatengeneze programu itakayo ungwa mkono katika masoko yote ya kimatiafa. Mbali na hivyo lazima waende wakapige magoti kwa Marekani kutumia mifumo yao ya Google play service, apple store, na Microsoft.
Na hiyo sio kazi ya kitoto kwenye biashara Mabadiliko ya tabia za watumiaji huchukua muda, na wengi tayari wamezoea Google, Microsoft na apple.
Hivyo China inaweza kuishi bila Google na Microsoft ndani ya mipaka yake, lakini ili kushindana kimataifa, bado inahitaji kushirikiana na wamarekani. Ikiwa China itafanikiwa kufanya mifumo yake mbadala iwe ya kimataifa, basi inaweza kupunguza utegemezi wake zaidi kwa teknolojia za Marekani. Kwa sasa, ushindani huu unaendelea, lakini Google na Microsoft bado zina ushawishi mkubwa duniani.
NOTE:
Yaani leo nmegundua China hamiliki kampuni yoyote ya simu wala computer kwasababu simu zake ili zifanye kazi lazima zikaruhusiwe na watu wa Google huko Marekani. Yaani Google ndio wadhibiti wa simu za China.
Computer pia lazima aende Marekani kwa watu wa Microsoft Marekani ili waziruhusu kutumia Microsoft.
Mpaka hapo naona kabisa China hawezi kugombana na Marekani kwa upande wa teknolojia.
Najua ni watu wachache sana watanielewa nilicho andika
Lakini ngoja nikufungue akili kile nilicho lenga.
Hakuna binadamu kwasasa anaweza kutumia simu isiyo na Google Play Service hayupo.
Hakuna binadamu anaweza kutumia computer isiyo na Microsoft.