China inaonekana kuibuka na ushindi dhidi ya janga la Corona

China inaonekana kuibuka na ushindi dhidi ya janga la Corona

Wakati nchi nyingi zikiingiwa na taharuki kutokana na kuenea kwa virusi vya corona nchini China katika jimbo la Guizhou Kusini-Magharibi mwa nchi hiyo wanafunzi wameanza kurejea mashuleni kama kawaida pasi na vilinda pua na midomo (mask)
Taarifa hii ni kwa Mujibu wa kituo cha habari cha Taifa la Uchina (CCTV)
Azam TV.
Je tatizo limepatiwa ufumbuzi?

nani kakudanganya hawatumii vilinda-pua?
CBCD7E18-1B45-43B7-8C7A-6E912E3BC2EE.png
 
Shughuli zimeanza kurudi kama kawaida nchini China katika ishara kuwa nchi hiyo imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona licha ya kuwa kiini cha mlipuko wa virusi hivyo.

Kwa mujibu wa matangazo ya Idhaa ya kiswahili ya Sauti ya Ujerumani, DW mchana wa leo, wametangaza Migahawa imeanza kufurika, Mabustani yamepokea idadi kubwa ya watu na sehemu kubwa ya nchi hiyo sasa imeondoa vikwazo huku Wafanyakazi wakianza kurudi makazini.
 
Hakuna cha ushindi

Hawatoi data za ukweli.

Kuna baadhi ya watu wana symptoms zote huko Wuhan lakini hawawapimi, wanawakatalia vipimo

Baadhi ya wagonjwa waliokuwa kwenye zile hospitali walizojenga ndani ya siku chache wamewaacha kwenda nyumbani bila kupona.

Kuna maagizo kutoka serikalini yaliyokuwa yakiagiza vituo vya tiba katika baadhi ya majimbo kuharibu data kuhusu wagonjwa wa Corona

Kwa sasa serikali ya china iko interested kwenye kufanya damage control ya uchumi zaidi huku wakisikilizia huko duniani situation itaunfold vipi
 
Ili kuwepo ushindi wa janga hili,inapaswa kusiwepo hata nchi moja yenye maambukizi haya, hii ni Kwa sababu hata sasa mtu yeyote akiwa na maambukizi ya ugonjwa wa Corona anakuwa sababu ya kuwaambukiza tena wengine hata hao waliopona, maana hakuna uthibitisho kwamba aliyeugua na akapona hawezi kuamvukizwa tena
 
Mkuu mbona kama hujajipa muda mzuri kufikiri kabla ya kupost? Kama kweli wanafanya hivo si matokeo yake ni vifo tena kwa hao raia! Sasa hapo nchi itanyanyua vp uchumi huku raia wanakufa? Hizi habari nyingine naona source utakuwa we mwenyewe
Mkuu wengine huwa ni waropokaji sijui inawezekana vipi kuachia wagonjwa wakaambukize raia wengine! Kila mtu atazungumza lake mengine ya kupuuza Kama hili halina miguu wala kichwa!
 
Tatizo waliidharau China kuwa haitaweza kukabiliana na changamoto ya ugonjwa huu kwa ufanisi.
 
Mkuu wengine huwa ni waropokaji sijui inawezekana vipi kuachia wagonjwa wakaambukize raia wengine! Kila mtu atazungumza lake mengine ya kupuuza Kama hili halina miguu wala kichwa!
Dah huyu jamaa anashangaza
 
Back
Top Bottom