China inaonekana kuibuka na ushindi dhidi ya janga la Corona

China inaonekana kuibuka na ushindi dhidi ya janga la Corona

Kwahyo hata wale drs waliopelekwa Italy ni kanjanja?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sasa kupeleka madaktari 9 ndo bonge la msaada?
Wenzako wanacheza na media na positive stories kwa sababu Corona imeharibu sana image ya chama cha kikomunisti ndani na nje ya China.

Hebu angalia hii video hapa chini, kama hali ni shwari na serikali imefunga zile hospitali za muda kwa sherehe mbona inajenga hospitali nyingine ya aina hiyo huko wuhan kimyakimya sasa?

 
Mpangumbe,
Taarifa ni kuwa wamewaua watu wote wenye maambukizi na ndiyo maana wanawafukuza waandishi wa NYT/waandishi wa habari toka USA kutoka nchini humo ili wafiche kinachoendelea katika kuukabiri ugonjwa huo
 
Shughuli zimeanza kurudi kama kawaida nchini China, katika ishara kuwa nchi hiyo imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona licha ya kuwa kiini cha mlipuko vya virusi hivyo.

Migahawa imeanza kufunguliwa huku idadi ya watu wakikusanyika tena katika mabustani, hiyo yote ikionyesha ishara kuwa China inaibuka na ushindi katika vita vyake dhidi ya virusi vya Corona ambavyo vimeutikisa ulimwengu.

Kwa wakati huu, China imeweka mikakati ya kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo kwa kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kuvaa barakoa na pia kupima viwango vya joto mwilini kwa watu wanaoingia katika maeneo ya umma.

Pia migahawa imeweka sheria za kuwazuia watu kukaribiana wanapokula ndani ya migahawa hiyo. Mikakati yote hiyo, licha ya ugumu wake katika utekelezaji lakini inaonekana kuzaa matunda.

Sehemu kubwa ya nchi hiyo sasa imeondoa vikwazo na watu wameanza kurudi kazini, tofauti na nchi za magharibi ambapo serikali zimeanzisha marufuku ya usafiri.

Cao Wei ambaye ni naibu mkurugenzi katika hospitali ya ushirika ya Peking amesema:

"Kwa sasa baada ya miezi mitatu kupambana na mlipuko huu, tunakaribia kufikia mwisho wake. Hata hivyo, tunasubiri angalau kwa mwezi mmoja mwengine kutathmini hali kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho. Lakini hata mlipuko ukatokea tena kwa mara ya pili, sidhani kama utatusumbua kama vile mwanzo."

Kadhalika mji wa kibiashara wa Shanghai pia umeanza kunawiri huku watu wakiendelea na biashara zao kama awali. Hata hivyo, wakaazi wa mji huo wanatakiwa kuwa na kitambulisho maalum kwenye simu zao chenye kuonyesha iwapo wako salama kuingia katika sehemu zenye watu wengi.

"Nahisi kuwa watu walioambukizwa virusi hivi hawawezi kutoka nje na kutangamana na wenzao, kwa hio sisi ambao tuko nje tuko salama", amesema Lai Jinfeng mwenye umri wa miaka 41.

Mnamo Machi 10 Rais Xi Jinping alitangaza wakati wa ziara yake katika mji wa Wuhan ambao ulikuwa kitovu cha mlipuko wa virusi vya Corona, kuwa nchi hiyo inakaribia kupata ushindi dhidi ya janga hilo la COVID-19 huku nao wachambuzi wa kiuchumi wakisema kuwa asilimia 90 ya biashara katika eneo la Hubei zimerudia hali yake ya kawaida.

Chanzo: DW Swahili
 
Mpangumbe,
Taarifa ni kuwa wamewaua watu wote wenye maambukizi na ndiyo maana wanawafukuza waandishi wa NYT/waandishi wa habari toka USA kutoka nchini humo ili wafiche kinachoendelea katika kuukabiri ugonjwa huo
Inapobidi kwenye taifa hilo jambo kufanyika hufanyika
Kama ni mpenzi wa movie kwenye series za 24hrs ilitokea kwenye hotel moja maana hapakua na tiba
Si kwamba China anaweza tenda ubaya kwa watu wake
Wamejitahidi kwa uwezo wao na swala la nchi linabaki kuwa la nchi

Fahamu inawaumiza sana
Wasingejenga hospital kama issue ni kuwaua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna cha ushindi

Hawatoi data za ukweli.

Kuna baadhi ya watu wana symptoms zote huko Wuhan lakini hawawapimi, wanawakatalia vipimo

Baadhi ya wagonjwa waliokuwa kwenye zile hospitali walizojenga ndani ya siku chache wamewaacha kwenda nyumbani bila kupona.

Kuna maagizo kutoka serikalini yaliyokuwa yakiagiza vituo vya tiba katika baadhi ya majimbo kuharibu data kuhusu wagonjwa wa Corona

Kwa sasa serikali ya china iko interested kwenye kufanya damage control ya uchumi zaidi huku wakisikilizia huko duniani situation itaunfold vipi
Ila mkuu hapa umewashambulia sana jamaa...

Tuna ukimwi huku zaidi ya miaka 35

Nyomi imeangamia

Hawa China sidhani ni wa hovyo wasijue wafanyacho

Hili jambo la virus lina mambo mengi sana,ni lazma uweze kupigana uwezavyo

Shutuma za kuwaachia wagonjwa bado natafakari ili iweje, ila kumbuka wanapigana kujitoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I have "a man " on ground in Wuhan. Hali imerejea kawaida. Watu wanaruhusiwa kupunga upepo nje bila bughuza!!!
 
Mpangumbe,
Taarifa ni kuwa wamewaua watu wote wenye maambukizi na ndiyo maana wanawafukuza waandishi wa NYT/waandishi wa habari toka USA kutoka nchini humo ili wafiche kinachoendelea katika kuukabiri ugonjwa huo
Hizi propaganda za China kuua wagonjwa sio za kuamini kabisa.

Ingekua ni kweli hawa mabeberu wangewashikia bango kweli kweli.

Hao waandishi wamefukuzwa ili kulipa kisasi kitendo cha Marekani kuwapiga marufuku waandishi wa China kufanya kazi kwenye mashirika yao.
 
Hakuna cha ushindi

Hawatoi data za ukweli.

Kuna baadhi ya watu wana symptoms zote huko Wuhan lakini hawawapimi, wanawakatalia vipimo

Baadhi ya wagonjwa waliokuwa kwenye zile hospitali walizojenga ndani ya siku chache wamewaacha kwenda nyumbani bila kupona.

Kuna maagizo kutoka serikalini yaliyokuwa yakiagiza vituo vya tiba katika baadhi ya majimbo kuharibu data kuhusu wagonjwa wa Corona

Kwa sasa serikali ya china iko interested kwenye kufanya damage control ya uchumi zaidi huku wakisikilizia huko duniani situation itaunfold vipi
Sasa wakifanya hivyo si ugonjwa utalipuka tena? Kwahiyo mkuu unafikiri China ni wajinga hivyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna cha ushindi

Hawatoi data za ukweli.

Kuna baadhi ya watu wana symptoms zote huko Wuhan lakini hawawapimi, wanawakatalia vipimo

Baadhi ya wagonjwa waliokuwa kwenye zile hospitali walizojenga ndani ya siku chache wamewaacha kwenda nyumbani bila kupona.

Kuna maagizo kutoka serikalini yaliyokuwa yakiagiza vituo vya tiba katika baadhi ya majimbo kuharibu data kuhusu wagonjwa wa Corona

Kwa sasa serikali ya china iko interested kwenye kufanya damage control ya uchumi zaidi huku wakisikilizia huko duniani situation itaunfold vipi
Hizi habari umezipata wapi?

Kama Sio propaganda toka kwa maadui na mahasimu wa China tuziitaje?
 
Hii naona ni kama biashara flani hivi, maana USA anasema dawa anayo wkt jana amepandikiza virus kwa raia wake ili ajaribu dawa anayosema anayo na mchina naye anasema ana dawa that`s inaonekana ni vita hii.
 
Back
Top Bottom