Bwana Utam
JF-Expert Member
- Feb 15, 2016
- 20,546
- 38,093
Mkiambiwa Mlete Habari kamili Nazenye Ukweli Mnakimbia
Sent using My COVID-19
Mkiambiwa Mlete Habari kamili Nazenye Ukweli Mnakimbia
No,siku 19Walijenga hospitali ya watu buku kwa siku sita hii ni record kubwa sana
Nimemuuliza mtu mwingine,sio wewe!
Sasa kupeleka madaktari 9 ndo bonge la msaada?
Wenzako wanacheza na media na positive stories kwa sababu Corona imeharibu sana image ya chama cha kikomunisti ndani na nje ya China.
Hebu angalia hii video hapa chini, kama hali ni shwari na serikali imefunga zile hospitali za muda kwa sherehe mbona inajenga hospitali nyingine ya aina hiyo huko wuhan kimyakimya sasa?
Acha kuogopesha Uma mkuu, habaHizi habari umezipata wapi?
Kama Sio propaganda toka kwa maadui na mahasimu wa China tuziitaje?
Ndio hivyo mkuu,I have "a man " on ground in Wuhan. Hali imerejea kawaida. Watu wanaruhusiwa kupunga upepo nje bila bughuza!!!
Waandishi wa NYT waliandika habari za kizandiki dhidi ya serikali ya China katika kushughulikia tatizo ala ugonjwa wa corona....walipotakiwa kuomba radhi wakakataa...ndiyo maana China imewafurusha.Mpangumbe,
Taarifa ni kuwa wamewaua watu wote wenye maambukizi na ndiyo maana wanawafukuza waandishi wa NYT/waandishi wa habari toka USA kutoka nchini humo ili wafiche kinachoendelea katika kuukabiri ugonjwa huo
HUKU KWETU TUNAPASWA KUFAHAMU KWAMBA, KWA SASA KUPOKEA WAGENI KUTOKA WANHU CHINA NI BORA, KULIKO KUPOKEA WAGENI KUTOKEA NCHI ZA BARA ULAYA.Wakati nchi nyingi zikiingiwa na taharuki kutokana na kuenea kwa virusi vya corona nchini China katika jimbo la Guizhou Kusini-Magharibi mwa nchi hiyo wanafunzi wameanza kurejea mashuleni kama kawaida pasi na vilinda pua na midomo (mask).
Taarifa hii ni kwa Mujibu wa kituo cha habari cha Taifa la Uchina (CCTV)
Azam TV.
Je, tatizo limepatiwa ufumbuzi?
-----
Shughuli zimeanza kurudi kama kawaida nchini China, katika ishara kuwa nchi hiyo imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona licha ya kuwa kiini cha mlipuko vya virusi hivyo.
Migahawa imeanza kufunguliwa huku idadi ya watu wakikusanyika tena katika mabustani, hiyo yote ikionyesha ishara kuwa China inaibuka na ushindi katika vita vyake dhidi ya virusi vya Corona ambavyo vimeutikisa ulimwengu.
Kwa wakati huu, China imeweka mikakati ya kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo kwa kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kuvaa barakoa na pia kupima viwango vya joto mwilini kwa watu wanaoingia katika maeneo ya umma.
Pia migahawa imeweka sheria za kuwazuia watu kukaribiana wanapokula ndani ya migahawa hiyo. Mikakati yote hiyo, licha ya ugumu wake katika utekelezaji lakini inaonekana kuzaa matunda.
Sehemu kubwa ya nchi hiyo sasa imeondoa vikwazo na watu wameanza kurudi kazini, tofauti na nchi za magharibi ambapo serikali zimeanzisha marufuku ya usafiri.
Cao Wei ambaye ni naibu mkurugenzi katika hospitali ya ushirika ya Peking amesema:
"Kwa sasa baada ya miezi mitatu kupambana na mlipuko huu, tunakaribia kufikia mwisho wake. Hata hivyo, tunasubiri angalau kwa mwezi mmoja mwengine kutathmini hali kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho. Lakini hata mlipuko ukatokea tena kwa mara ya pili, sidhani kama utatusumbua kama vile mwanzo."
Kadhalika mji wa kibiashara wa Shanghai pia umeanza kunawiri huku watu wakiendelea na biashara zao kama awali. Hata hivyo, wakaazi wa mji huo wanatakiwa kuwa na kitambulisho maalum kwenye simu zao chenye kuonyesha iwapo wako salama kuingia katika sehemu zenye watu wengi.
"Nahisi kuwa watu walioambukizwa virusi hivi hawawezi kutoka nje na kutangamana na wenzao, kwa hio sisi ambao tuko nje tuko salama", amesema Lai Jinfeng mwenye umri wa miaka 41.
Mnamo Machi 10 Rais Xi Jinping alitangaza wakati wa ziara yake katika mji wa Wuhan ambao ulikuwa kitovu cha mlipuko wa virusi vya Corona, kuwa nchi hiyo inakaribia kupata ushindi dhidi ya janga hilo la COVID-19 huku nao wachambuzi wa kiuchumi wakisema kuwa asilimia 90 ya biashara katika eneo la Hubei zimerudia hali yake ya kawaida.
Chanzo: DW Swahili
Haya
Unaijua Italy?Panic iliyopo China huwezi linganisha na nchi yoyote...
Hizi habari umezipata wapi?
Kama Sio propaganda toka kwa maadui na mahasimu wa China tuziitaje?
Walipitia haya miezi mitatu iliyopita, sasa ni wakati wetu, tuombe isichukue muda mrefu. Hata hiyo habari ya DW inadai Magharibi bado inazuia shughuli mbalimbali, shirika kubwa la habari hawakumbuki kuwa China ilianza kushambuliwa na kuchukua hatua hizi hizi, miezi mitatu iliyopita? Inapodhihirika kuwa maambukizi mapya hamna au yamepungua sana , ndio jamii hurudi tena katika pilika zake za kawaida.Inapendeza....I wish I could be in China this time... Huku ni mapresha na mafake news ya kishenzi tu.
Sio wanaweza, dawa waliyoigundua ndio Wachina wanayoitumia tangu January.Mh? Cuba tena. Kwakuwa wasosharisti ndio unahisi wanaweza kutengeneza
Sent using Jamii Forums mobile app
Hii taarifa ni propaganda tupu!Shughuli zimeanza kurudi kama kawaida nchini China, katika ishara kuwa nchi hiyo imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona licha ya kuwa kiini cha mlipuko vya virusi hivyo.
Migahawa imeanza kufunguliwa huku idadi ya watu wakikusanyika tena katika mabustani, hiyo yote ikionyesha ishara kuwa China inaibuka na ushindi katika vita vyake dhidi ya virusi vya Corona ambavyo vimeutikisa ulimwengu.
Kwa wakati huu, China imeweka mikakati ya kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo kwa kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kuvaa barakoa na pia kupima viwango vya joto mwilini kwa watu wanaoingia katika maeneo ya umma.
Pia migahawa imeweka sheria za kuwazuia watu kukaribiana wanapokula ndani ya migahawa hiyo. Mikakati yote hiyo, licha ya ugumu wake katika utekelezaji lakini inaonekana kuzaa matunda.
Sehemu kubwa ya nchi hiyo sasa imeondoa vikwazo na watu wameanza kurudi kazini, tofauti na nchi za magharibi ambapo serikali zimeanzisha marufuku ya usafiri.
Cao Wei ambaye ni naibu mkurugenzi katika hospitali ya ushirika ya Peking amesema:
"Kwa sasa baada ya miezi mitatu kupambana na mlipuko huu, tunakaribia kufikia mwisho wake. Hata hivyo, tunasubiri angalau kwa mwezi mmoja mwengine kutathmini hali kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho. Lakini hata mlipuko ukatokea tena kwa mara ya pili, sidhani kama utatusumbua kama vile mwanzo."
Kadhalika mji wa kibiashara wa Shanghai pia umeanza kunawiri huku watu wakiendelea na biashara zao kama awali. Hata hivyo, wakaazi wa mji huo wanatakiwa kuwa na kitambulisho maalum kwenye simu zao chenye kuonyesha iwapo wako salama kuingia katika sehemu zenye watu wengi.
"Nahisi kuwa watu walioambukizwa virusi hivi hawawezi kutoka nje na kutangamana na wenzao, kwa hio sisi ambao tuko nje tuko salama", amesema Lai Jinfeng mwenye umri wa miaka 41.
Mnamo Machi 10 Rais Xi Jinping alitangaza wakati wa ziara yake katika mji wa Wuhan ambao ulikuwa kitovu cha mlipuko wa virusi vya Corona, kuwa nchi hiyo inakaribia kupata ushindi dhidi ya janga hilo la COVID-19 huku nao wachambuzi wa kiuchumi wakisema kuwa asilimia 90 ya biashara katika eneo la Hubei zimerudia hali yake ya kawaida.
Chanzo: DW Swahili
umeridhika kabisa kuwa huu ndiyo ushahidi wa kubeba hoja yako!!! Muda ni mwamuzi mzuri, narudia.