Napingana na wewe kabisa.
Wapi umepata hiyo habari kuwa kuna kambi ya jeshi ya Marekani Taiwan na kuwa kuna wanajeshi wa Marekani 20,000?
Hakuna kambi ya jeshi ya Marekani Taiwan. Kuna wanajeshi 31 tu wa Marekani Taiwan. Waliongezeka mwaka jana toka 20.
Na sababu ya Marekani kutaka Taiwan isiwe sehemu ya China ni hili iweze kuweka base pale.
Na sababu pekee Marekani inaitetea Taiwan ni ili kuibana China na kuinyima access ya bahari ili kuidhibiti kiuchumi. Hakuna lingine.
Ukiangalia kwenye ramani, hapo Taiwan ndiyo sehemu pekee iliyobaki ambayo China ina control na kupitisha mizigo yake. Maana upande mwingine ni South Korea na Japan, upande mwingine ni Philippines na visiwa vyake. Taiwan ipo katikati.
Pia ndiyo sababu hiyohiyo Marekani inataka Hong Kong ijitenge Na China. Kwa kuwa ikitoka ina maana Guangzhou litakuwa hatarini kushuka sana kiuchumi.
Hakuna sijui kuitafutia uhuru Taiwan wala nini. Ni propaganda za kipuuzi tu.
Wabongo tutumie muda japo kuidogo kufungua ramani ili uweze kuelewa haya mambo.
View attachment 2307744