China itapata wakati mgumu sana kwa Taiwan kuliko Russia kwa Ukraine

Kama marekani kaufyata, namuunga mkono katika hili,ashughulike na urusi kwanza,kujiunga katika vita pande mbili kwa wakati mmoja ingemuhathiri sana,
 
Hakuna mtu mwenye akili timamu anaeweza kuamini ku Mmarekani anaweza kuingia vita na China kwa sababu ya Taiwan.
 
Wewe mchambuzi kutoka (Yombo Vituka Institute for International and Strategic Studies) kitu ambacho hujui ni kwamba hizo silaha unazozitaja ni silaha ndogo sana kwa taifa kama Marekani.

Mataifa kama Russia na China yana tabia ya kuonyesha silaha zao kwenye sherehe zao za kitaifa kitu ambacho hakipo kwa nchi za magharibi, kwa hivyo huwezi kujua silaha zao.

Na kama unafikiri ni mchezo basi Russia ijaribu kuishambulia nchi yoyote ya Nato ndio utaona silaha ambazo hata huzijui japo nashangaa unasema hawana silaha hizo ulizozitaja lkn zote zina majina ya kiingereza na wala hujazitaja kwa kichina wala kirusi..!!
 
Ubaya wa mambo kwa china ni kwamba technologia yao yote asili yake ni Marekani ndio ujinga mkubwa wa hawa China walioufanya miaka nenda miaka rudi,

Mchina amekuwa akipewa watalaamu kutoka US na mambo mingi ya technologia wataalam wametoka US
 
Ha ha ha ha ha ha ha ha eti wakatoa copy nyingi zaidi hata za HIMARS. Moja ya kitu ambacho China amekosa pia ni experience ya modern warfare.
 
Nipo nyuma yako bro [emoji41][emoji41][emoji41]

Ukizingatia us amechoka mbinu zake nyingi wadau wameshazishtukia na ndio maana maeneo mengi tu wadau wanamdindia anaishia kuweka vikwazo.

Kipind ipo kwenye ubora alikua anatoa maelezo machache eidha uunge mkono au uwe mpinzan lkn sasa hv hana ubavu wa kutoa kaul za kibabe hivyo
 
China bado yaihesabia Taiwan kuwa ni moja ya majimbo yake na yaweza kuivamia siku moja ili kutimilisha hiyo kauli yao.

Pia China hawajachelewa yaweza kuichukua Taiwan kwa bila kutumia nguvu ya kijeshi kwa kushindilia ushirikiano wa kuchumi kama ambavyo imefanya majuzi pale Xi alipotembelea kisiwa cha Hong Kong tena kwa njia ya reli.

Lakini pia China yaweza kuivamia Taiwan wakati wowote ikitaka na marekani isifanye lolote kwa kuzingatia kuwa hivi karibu ndege za kivita za China zimekua zikifaya doria la anga zima la eneo hilo bila shida.

Na kama ikitokea China kuvamia Taiwan basi kisiwa hicho hakitakuwa na uwezo wa kujilinda na jeshi lake litamezwa mara moja. China ni nchi pekee duniani ukiondoa marekani ambayo ina matumizi makubwa ya fedha kwenye jeshi na ikitokea yaivamia Taiwan basi utashuhudia China ikitumia nguvu zake kwenye jeshi la maji, anga, ardhini, makombora ya kisasa, ndege za kisasa za kivita (ambazo hizijawahi kutumika) na pia mashambulizi ya mitandao au "Cyber-attacks".

Hata hivyo, bado Taiwan na jeshi lake la watu 80,000 kulinganisha na China yenye jeshi la watu zaidi ya milioni mbili, wanaweza kupunguza makali ya mashambulizi kwa kiasi fulani kwa kuzuia askari wa miamvuli na wanamaji (amphibious forces) na kuanzisha mashambulizi kama yale ya Vietnam yaani kulala kikambare na kushambulia kwa kustukiza huku wakingojea msaada wa kijeshi kutoka nje kwa Marekani na washirika wake hususan Korea Kusini na Japan.

Taiwan yapokea silaha nyingi inouziwa na Marekani hivyo inaweza kuwa na akiba ya kutosha kwa kujihami pale mwanzo wa vita.

Lakini bila shaka kama kawaida ya wamarekani kwenye masuala ya diplomasia na sera ya nje yaani "foreign policy", bado yaitambua sera ya China isemayo "One- China policy" yaani Marekani kuitambua China na serikali yake moja tu yenye makao makuu Beijing na ina ushirikiano nayo China na sio Taiwan.

Ndio kusema kuwamba Marekani imekuwa ikitoa kauli tata za kindumilakuwili kuhusu kuingia vitani kuisadia Taiwan endapo itavamiwa na China lakini hapohapo washauri wa serikali wakisema hilo halitakuwa jambo sahihi.

Hata hiyo ziara ya huyo bibi mchokozi Nancy Pelosi ambayo anaanzia Singapore na kuishia Japan sidhani kama atathubutu kutua Taipei kwani wachina wameishasema Marekani isicheze na moto.

Mwisho nikuulize hivi wadhani hayo yote ulosema ya Taiwan kujiandaa hayajaonwa na satellite za mchina?
 
Ubaya wa mambo kwa china ni kwamba technologia yao yote asili yake ni Marekani ndio ujinga mkubwa wa hawa China walioufanya miaka nenda miaka rudi,

Mchina amekuwa akipewa watalaamu kutoka US na mambo mingi ya technologia wataalam wametoka US
Kifupi ni kwamba, ANACOPY TEKNOLOJIA KUTOKA MAGHARIBI.
 
Kwanini nchi za NATO zisiishambulie RUSSIA ambayo inaonesha silaha zake hovyo hovyo
Imeivamia UKRAINE imeingia SYRIA iliingilia VENEZUELA
Imefanya majeshi ya FRANCE yasepeshwe kule MALI
taifa pekee lakuivamia RUSSIA ni RUSSIA yenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwanini nyie msianze pale Moscow? Russia anaingia nchi yoyote ya NATO na hakuna kitu wanafanya. Mbona lithuania mmeachia??[emoji23][emoji23]
 
Kiazi nyingine hii unaisi vita inapiganwa Kwa mihemko nchi yoyote itakayoatarusha usalama WA Rusia itapigwa Tu alafu labda nikwambie Tu ule muungano WA NATO ni kwaajili ya nchi NNE Tu Marekani, France, uingereza na kidogo Germany awoo wengine ni kama chambo usitegemee vita vikizuka Marekani ataaribu uchumi wake Kwa kuipigania Poland au Latvia au Lithuania iloo sahau watatoa silaha Tu Ila kwenda front sahau
 
DuDuh muuza kahawa mbona hainekani nataka kahawa anichanganyie na tangawizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…