China kuendesha TAZARA kwa miaka 27, Uwekezaji wa dola bilioni 1.4 kuanza

China kuendesha TAZARA kwa miaka 27, Uwekezaji wa dola bilioni 1.4 kuanza

Nitajie muwekezaji wa ndani mwenye mtaji wa kuweza kukarabati hiyo railway line? Kuifanya irudi kwenye ubora wake kunahutaji USD 1.0 Billion sawa na Tsh 2.7 Trillion!! Nani ana hela hiyo?

Kuendesha TAZARA siyo sawa na kuendesha mabasi ya Kimbinyiko. Acheni mizaha
Tunapoongelea uwekezaji wa ndani sio lazima tu awe bosi mmoja vipi kama kukawa na partnership ya makampuni kadhaa? Mbn nchi nyingine wameweza tatizo letu wabongo ujuaji mwingi lakin usio na tija sawa?
 
Tunapoongelea uwekezaji wa ndani sio lazima tu awe bosi mmoja vipi kama kukawa na partnership ya makampuni kadhaa? Mbn nchi nyingine wameweza tatizo letu wabongo ujuaji mwingi lakin usio na tija sawa?
Sure kuna bond ambazo watu haya lefu moja wanauwezo wa kupata hiyo trolioni 3..
 
Watanzania wao kila kitu wanakosoa,kisa tu Rais mwanamke na si wa upande ule
 
Nakumbuka jinsi lile jengo la abiria la TAZARA lilipokamilika lilivyobadilisha kabisa taswira ya jiji la Dar es salaam. Eneo lile liling'aa utadhani uko China. Lilisifiwa kuwa jengo la abiria la mfano Afrika Mashariki.... Kilichofuata hakieleweki hadi leo. TAZARA imekuwa mali ya wapigaji yaani wafanyakazi wa ngazi zote kazi ni moja tu Chukua Chako Mapema.

Muonekano wa stesheni kuu ya treni ya reli ya TAZARA jijini DSM mwaka 2024

View: https://m.youtube.com/watch?v=fROw17CEmCY
 
Hakuna watu watalia kama wafanyabiashara wa malori.kila siku wanaambiwa hii fursa wao wanakomaa na malori ya kutoka kwao..kifupi paka kapewa kulinda samakai.

Ni ubunifu tu, hata wenye malori watafurahia mizigo mingi, reli haifiki hadi katika milango ya wateja ( door to door), ni suala la kuunganisha usafiri wa reli na malori katika shughuli ya ugavi hadi kwa mteja

View: https://m.youtube.com/watch?v=SA4hYpW10RE
 
Nitajie muwekezaji wa ndani mwenye mtaji wa kuweza kukarabati hiyo railway line? Kuifanya irudi kwenye ubora wake kunahutaji USD 1.0 Billion sawa na Tsh 2.7 Trillion!! Nani ana hela hiyo?

Kuendesha TAZARA siyo sawa na kuendesha mabasi ya Kimbinyiko. Acheni mizaha
Sisi kazi yetu kuua mashirika. Kuwapa Wachina ndiyo suluhisho, sisi wazawa HATUWEZI.
💀 mungu tu atulinde the next 5 years mambo yatakuwa magumu sana
Bora waendeshe wao

Wabongo kazi yao ni kuvuna wasipopanda
Kiwango cha kujali vitu na uwajibikaji kwetu sisi kipo chini sana.

"Mwendokasi" ya juzijuzi tu, inayofanya kazi baadhi ya maeneo tu hapo Dar nayo inaonekana itarudi kwa mwekezaji. Unabaki unajiuliza "uhuru" tulioupigania ilikuwa ni kwa ajili ya nini hasa!

"Black people are good for nothing apart from indulging in sex, dancing and having so many wives."

Pieter W. Botha, a former President of South Africa during the Apartheid era.
 
FURSA KWA SEKTA YA RELI NA UGAVI (SUPPLY) KUWA TIMU MOJA, TAZARA KUFANYA KAZI KWA UKARIBU NA WENYE MALORI


View: https://m.youtube.com/watch?v=8Kc4I7rFDkk
Shirika la reli ya KRC lilikuja na dhana ya RORO, ambapo lori zilizopakiwa kuwekwa kwenye mabehewa ya wazi na kusafirishwa kwa treni. Hii imesaidia katika kuokoa mafuta, kupungua kwa uchakavu injini za lori na uchakavu wa jumla wa lori (malori), unafuu kwa madereva wa kuepuka kuendesha gari katika mazingira hatarishi, malori yanaweza kufikia na kurudi mapema. Hii pia husaidia kupunguza msongamano wa barabarani na kupunguza uchafuzi wa mazingira. Dhana hii imekuwa ya manufaa kwa makampuni ya waendeshaji lori na shirika la reli KRCL.


RORO means Roll-on/roll-off, where loaded trucks are directly carried by railway wagons to their destination. Konkan Railways passes through tough terrains of India. There is NH-17 passing through same route. Truck drivers find it extremely difficult to drive loaded trucks through ghats, undulating surfaces, narrow roads and poor road and weather conditions. The KRC came with concept of RORO, where loaded trucks are moved on wagons and are travelled by train. This has helped in saving of fuels, decrease in wear and tear of lorries (trucks), relief to drivers of driving in extreme conditions, can reach faster to destination. This also helps in decongestion of roads and lowering of pollution. This concept has been beneficial for both truck operators and KRCL.
 
JF unakuta mada ambayo mjadala wake michango husika inatakiwa kujikita kwenye investment appraisal na justification ya decision based on mutual benefits za mwekezaji na serikali.

Sasa soma michango husika ya mada, daah the nonsense.

Elimu ya Tanzania ni shida

Sisemi naafiki TAZARA kugawa miundombinu yake kirahisi hivyo, kwa mkataba ambao probably mmbaya.

Worst China ni nchi ambayo kipindi cha nchi tajiri kiliamua kusamehe madeni ya Africa hasa nchi zilizokuwa zimezidiwa na madeni kama Tanzania ili zifanye restructuring ya madeni.

Ni China na wanachama wa Paris Club (private institutions). Serikali za wazungu walifuta madeni yao, serikali ya China ilisema no kwa deni lao la ujenzi wa TAZARA tumemaliza kuwalipa kwenye 2010’s. Sasa ni vipi watu hawa-hawa tunawaalika wavune leo kirahisi.

Ni watu wa hovyo tu ndio awakumuelewa Magufuli.
 
Tunapoongelea uwekezaji wa ndani sio lazima tu awe bosi mmoja vipi kama kukawa na partnership ya makampuni kadhaa? Mbn nchi nyingine wameweza tatizo letu wabongo ujuaji mwingi lakin usio na tija sawa?
Haya niunganishie matajiri 5 wazawa wanaoweza ku-raise hiyo Tsh 2.5 Trillion halafu na kubeba risk ya railway management
 
Haya niunganishie matajiri 5 wazawa wanaoweza ku-raise hiyo Tsh 2.5 Trillion halafu na kubeba risk ya railway management
Kwahiyo unadhani CCM ikialika wawekezaji wazawa kwny hiyo railway Metl,Motisun,Asas,Bakhresa watashindwa?
 
Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) imetangaza kuwa Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) itachukua usimamizi na uendeshaji wa reli hiyo kwa kipindi cha miaka 27.

Makubaliano haya, yenye thamani ya Dola bilioni 1.4 yatatoa fursa ya kurekebisha miundombinu ya reli na kuboresha ufanisi wake.

Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA, Mhandisi Bruno Ching'andu amesema sehemu ya uwekezaji utajumuisha ukarabati wa reli, pamoja na ununuzi wa vichwa vipya na mabehewa. Hatua hii inatarajiwa kuboresha usalama na kupanua uwezo wa usafirishaji wa abiria na mizigo.

Mkataba huu wa miaka 30 utalenga kutoa huduma bora zaidi na kudumisha operesheni za TAZARA. Serikali za Tanzania na Zambia zinatarajia kuwa mradi huu utaongeza biashara na kuimarisha usafiri kati ya nchi hizi mbili.

Kampuni ya CCECC itasimamia uendeshaji wa reli hiyo kwa miaka 27 ijayo, huku TAZARA ikifanya kazi kwa karibu kuhakikisha utekelezaji mzuri wa mradi huu.

Chanzo: Habari Leo
Mungu atunusuru, hivi sisi tutaweza kipi ili nasi tukaishangaze dunia?
 
Hii sasa ina miaka 50.....unaionaje??.....hatuna akili .....hatuna uwezo ...wajinga au shida nini ?? Umasikini wa fikra ?? Miaka 30 wakitupa itakuwa nusu kufa kama tutaendelea ujinga huuu miaka 200 mwendo huo.....
Wanaweka USD 1.4 bln kuiupgrade
 
Nikiwa bado hapa duniani nitakuwa na vitukuu ndio wao wanafikiri ku renew contract
 
Tuipe SGR miaka mingapi kabla nayo hatujaikabidhi kwa Wachina?

Mwendokasi nayo bado kidooogo tuikabidhi kwa mtu wa nje!

Viwanda kama Urafiki navyo viko hoi, labda tumkabidhi Mchina!

Kariakoo nako kila kona ni Wachina!

Bandari ya Dar anayo Muarabu!

Bandari ya Bagamoyo Adani tayari alishakula dili!
IMG-20250321-WA0018.jpg


Ndiyo kusema nchi yetu tumeshindwa kabisa kuendesha miradi yetu mpaka wa nje watusaidie?

Kwa rate hii, si ndani ya miaka michache tutakuwa kama koloni tena?!

20250321_210052.jpg
 
Nitajie muwekezaji wa ndani mwenye mtaji wa kuweza kukarabati hiyo railway line? Kuifanya irudi kwenye ubora wake kunahutaji USD 1.0 Billion sawa na Tsh 2.7 Trillion!! Nani ana hela hiyo?

Kuendesha TAZARA siyo sawa na kuendesha mabasi ya Kim
😂😂
 
Inashangaza sana kwa jinsi tunavyoshindwa kuendesha mambo yetu hata yale madogo madogo na kulazimika kuwapa wale waliojenga miundombinu hivyo miaka 60 iliyopita watusaidie!
Mambo mengine yafanyie uchunguzi kwanza.
TAZARA ni ya Tanzania na Zambia.
Madhumi ya kujenga TAZARA ilikuwa kusafirisha mizigo ya Zambia kupitia Tanzania. Siku hizo Msumbiji,Zimbabwe, na Africa Kusini zilikuwa zinatawaliwa na wakoloni walioiwekea vikwazo Zambia kwa kuunga mkono juhudi za ukombozi wa nchi hizo.

Baada ya nchi hizo kupata uhuru Zambia haikuona umuhimu wa kupitisha mizigo yake TAZARA.Kibaya zaidi CEO wa Tazara anatakiwa kutokea Zambia kisheria.

Kuongeza uchungu kwenye kidonda upande wa reli ya TAZARA upande wa Tanzania reli haina michepuko.
Ndio pale Profesa Mazurui wa Kenya alipotuita Watanzania kuwa tunapenda kitu kupindukia yaani TANZAFILIA.Tuliangalia zaidi kuisaidia Zambia bila kuangalia madhara yatakayoikumba Tanzania kiuchumi.Au jinsi ya kuitumia reli hiyo kibiashara upande wa Tanzania.

Mwenyekiti Mao aliyekuwa kiongozi mkuu wa China siku hizo,alimwambia Raisi Nyerere kuwa atampa kiwanda cha kutengeneza mashine yeyote hata kifaru,na akampa wataalamu wakundesha kiwanda hicho.akuachia hapo walipelekwa maefu ya Watanzania China kujifunza nyanja mbali mbali.
Kiwanda hicho kilijulikana MMT yaani Mangula Mechanical Tools.
Kilikuwa kiwanda cha aina yake kusini mwa Sahara.Kwa sasa MMT hakipo kilikufa zamani sana.Bila MMT Tazara iligeuka yatima.

Kwa sasa Tazara ni marapu rapu,ndivyo tulivyo wabongo.kupenda kula bila kunawa.
 
Kwahiyo unadhani CCM ikialika wawekezaji wazawa kwny hiyo railway Metl,Motisun,Asas,Bakhresa watashindwa?
Kwa hiyo METL unamuona ana hela? Kama anazo mbona Simba inalialia tu ? Wala haijawahi kuvuka robo fainali ya CAF?

Asas hana hela. Bakhressa anazo lakini hilo siyo eneo lake
 
Back
Top Bottom