Danielmwasi
JF-Expert Member
- May 3, 2021
- 2,329
- 4,203
đź’€ mungu tu atulinde the next 5 years mambo yatakuwa magumu sana
Walikabidhi zamani tu, ofisi hata ya hapo Dar wako wachina wanaongoza.nao wenzetu wa zambia kwani nao wanasemaje juu ya hilo?
Na ukikumbuka tuliachiwa na hadi kiwanda Cha kukata Almasi - TANCUT Iringa, unachoka kabisa. Baadhi ya majengo yake ndio hiyo Mahakama Kuu Iringa.Miaka hiyo tupo Uchindile huko ndani ndani,unakwea zako Tazara,mwendo wa Ngiri,chuma inatembea mbayaaaa....
Kaja Mtu mweusi,ng'oa ng'o vitu....mamaeee,ndio black people life....
Kila kitu ukiwaza roho inaumaa
Mimi nilidhani tungezungumza na Zambia kubadilli mfumo wa uendeshaji ili tuwe na sauti upande wetu,pia Reli hiyo ingewekwa chini ya TRC kwa Tanzania.Kuwapa wachina sio suluhisho pekee ni kufeli kunakoendelea.Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) imetangaza kuwa Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) itachukua usimamizi na uendeshaji wa reli hiyo kwa kipindi cha miaka 27.
Makubaliano haya, yenye thamani ya Dola bilioni 1.4 yatatoa fursa ya kurekebisha miundombinu ya reli na kuboresha ufanisi wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA, Mhandisi Bruno Ching'andu amesema sehemu ya uwekezaji utajumuisha ukarabati wa reli, pamoja na ununuzi wa vichwa vipya na mabehewa. Hatua hii inatarajiwa kuboresha usalama na kupanua uwezo wa usafirishaji wa abiria na mizigo.
Mkataba huu wa miaka 30 utalenga kutoa huduma bora zaidi na kudumisha operesheni za TAZARA. Serikali za Tanzania na Zambia zinatarajia kuwa mradi huu utaongeza biashara na kuimarisha usafiri kati ya nchi hizi mbili.
Kampuni ya CCECC itasimamia uendeshaji wa reli hiyo kwa miaka 27 ijayo, huku TAZARA ikifanya kazi kwa karibu kuhakikisha utekelezaji mzuri wa mradi huu.
Chanzo: Habari Leo
We unataka apewe nani aiendeshe....Mimi nilidhani tungezungumza na Zambia kubadilli mfumo wa uendeshaji ili tuwe na sauti upande wetu,pia Reli hiyo ingewekwa chini ya TRC kwa Tanzania.Kuwapa wachina sio suluhisho pekee ni kufeli kunakoendelea.
Kwani TRC nani anaendesha?We unataka apewe nani aiendeshe....
Ova
Kiwango cha kujali vitu na uwajibikaji kwetu sisi kipo chini sana.Katika vitu ambavyo wazungu wana haki ya kusema sisi Waafrika hatuna akili, wazembe, mafisadi na tumekalia uzinzi na ulevi, ni jinsi Zambia na Tanzania tulipoifikisha TAZARA
Kuna maeneo mengi sana ambayo yalikuwa bora zaidi mkoloni alipoondoka Tanganyika kuliko yalivyo sasa. Ngozi nyeusi haina ustaarabu wa kukarabati na ku-maintain, si nyumba zetu binafsi au miradi ya umma. Mtu anakaa nyumba yake miaka zaidi ya 10 hata kurudishia rangi haoni uhitaji, kuta chafu, chooni hakufai, na ni nyumba yake binafsi. Tazara siku hizi chooni unawekewa ndoo za maji. Hata SGR baada ya muda itakuwa hivyo hivyo.
Wazungu waliondoka Zimbabwe wakaacha iko safi kama Ulaya. Nenda leo ukaone mitaa na majengo ya Harare yalivyo machafu. Johannesburg hivyohivyo, sio ile tena iliyokuwa ya Kaburu.
Bora waendeshe waoDaaaaa tulipewa mpya imetufia mkononi....saaa baada miaka 27.....watatupa ikiwa nusu kuzeeka.....tena tunapiga 10yrs inakufa tenaaa
Mwekezaji kama Nani?Bora tu wangeitisha wawekezaji wa ndani kuliko hao wachina
Aisee..sisi tuna roho mbaya mno ni basi tuNa ukikumbuka tuliachiwa na hadi kiwanda Cha kukata Almasi - TANCUT Iringa, unachoka kabisa. Baadhi ya majengo yake ndio hiyo Mahakama Kuu Iringa.
Sisi kazi yetu kuua mashirika. Kuwapa Wachina ndiyo suluhisho, sisi wazawa HATUWEZI.Mimi nilidhani tungezungumza na Zambia kubadilli mfumo wa uendeshaji ili tuwe na sauti upande wetu,pia Reli hiyo ingewekwa chini ya TRC kwa Tanzania.Kuwapa wachina sio suluhisho pekee ni kufeli kunakoendelea.
Unaona TRC inaendeshwa kwa tija? Subiri ripoti ya CAG next monthKwani TRC nani anaendesha?
Nitajie muwekezaji wa ndani mwenye mtaji wa kuweza kukarabati hiyo railway line? Kuifanya irudi kwenye ubora wake kunahutaji USD 1.0 Billion sawa na Tsh 2.7 Trillion!! Nani ana hela hiyo?Bora tu wangeitisha wawekezaji wa ndani kuliko hao wachina
Wangekuwa wanaitumia isingefika hukoNitajie muwekezaji wa ndani mwenye mtaji wa kuweza kukarabati hiyo railway line? Kuifanya irudi kwenye ubora wake kunahutaji USD 1.0 Billion sawa na Tsh 2.7 Trillion!! Nani ana hela hiyo?
Kuendesha TAZARA siyo sawa na kuendesha mabasi ya Kimbinyiko. Acheni mizaha
Tazara na yenyewe itakua inafanya nini? Si bora ifungwe tu badala yakuendelea kutia hasara serikali zetu. Tena kama vigogo walafi wa zambia na tanzania hawataweza kuwapa wachima ushirikiano bora tu hiyo teli ifungwe maana kuiuza itakua usaliti mkubwa kwa nyerere na kaunda. Reli inahujumiwa kufanya biashara na malori ya vigogo. Wanahakikisha mizogo wa kubebwa na reli yanabeba malori yao. Uchumi unahujumiwa na gharama kubwa ambazo zingepungua kwa kutumika reli. Pia barabara zinakutikana na maisha mafupi bure kwa kubeba mizigo mizito kama madini ya vyuma na shaba ambayo yangestahili kubebwa ikibidi hata kwa sheria na reli.Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) imetangaza kuwa Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) itachukua usimamizi na uendeshaji wa reli hiyo kwa kipindi cha miaka 27.
Makubaliano haya, yenye thamani ya Dola bilioni 1.4 yatatoa fursa ya kurekebisha miundombinu ya reli na kuboresha ufanisi wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA, Mhandisi Bruno Ching'andu amesema sehemu ya uwekezaji utajumuisha ukarabati wa reli, pamoja na ununuzi wa vichwa vipya na mabehewa. Hatua hii inatarajiwa kuboresha usalama na kupanua uwezo wa usafirishaji wa abiria na mizigo.
Mkataba huu wa miaka 30 utalenga kutoa huduma bora zaidi na kudumisha operesheni za TAZARA. Serikali za Tanzania na Zambia zinatarajia kuwa mradi huu utaongeza biashara na kuimarisha usafiri kati ya nchi hizi mbili.
Kampuni ya CCECC itasimamia uendeshaji wa reli hiyo kwa miaka 27 ijayo, huku TAZARA ikifanya kazi kwa karibu kuhakikisha utekelezaji mzuri wa mradi huu.
Chanzo: Habari Leo