China kuipatia silaha Russia dhidi ya Ukraine

China kuipatia silaha Russia dhidi ya Ukraine

🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Anakopesha au anauza kwa discount, tofautisha hayo mawili.
Vyovyote iwavyo hataziba pengo la ulaya, ulaya na marekani ndio iliyokuwa inaipa utajiri Russia sasa India yenyew taaban china pia, tutegemee anguko la urusi kubwa la kiuchumi
 
Vyovyote iwavyo hataziba pengo la ulaya, ulaya na marekani ndio iliyokuwa inaipa utajiri Russia sasa India yenyew taaban china pia, tutegemee anguko la urusi kubwa la kiuchumi
We tegemea hilo tu. Yajayo yanafurahisha.
 
Sasa silaha zako utatumia zote kabla ya vita halafu vita ikianza utumie nini? 🤣 Urusi sio mjinga kama unavyofikiri. Anapoomba silaha maana yake hataki bank yake ya masilaha iende chini ya kiwango. Kuna level ambayo unatakiwa ku maintain mda wote kwa ajili ya kujiandaa na vita.
Ukiona superpower ndani ya mwaka mmoja hana tena silaha zaidi ya kujilinda yeye mwenyewe jua hilo Taifa walipiga mdomo mwingi sana kujipaisha hawana kitu russia.,

Mkuu NATO wana uwezo kupigana hata kwa miaka 30 none stop na hutawasikiapo wakilalamika na kukopa silaha kwa jirani
 
Heheheh sasa hao majirani zao sindio NATO. Wewe silaha combined za nchi 30 utafananisha na silaha za nchi 5?
All in all NATO watapigwa kama ngoma. Mi nataka wamuanzishie Mrusi kwamba vita inakuwa rasmi halafu tuone show.
 
Mkuu vita kamili urusi ameshindwa mwenyewe
*Putini alisema nchi yoyote itakayoisaidia Ukrean ama kuingia au kuwasaidia kwa silaha yeye angetumia nuclear kuelekeza mashambulizi kwenye hizo nchi lakini Austin waziri wa mambo ya ndani ya Marekani alimjibu kwamba sisi Marekani tunaisaidia Ukraine usiku na mchana na tutahikikisha Ukrean inakuwa huru na mipaka yake yote na unaona toka vita imeanza urusi alipovamia Kyiv Marekani ndio walimtoa adui Kyiv.
*Putin alisema Ukraine ikijaribu tu kujiunga na ulaya basi atapiga nuclear katikati ya kitovu cha nchi za ulaya lakini kama unafuatilia Ukrean wamefanyama maombi ya kujiunga na ulaya mchana kweupe jua linangaa lakini kama haitoshi karibuni walipeleka rasmi maombi ya Nato.
*Putin pia alisema nchi za Finland na Sweden wakijaribu kupeleka maombi kujiunga na Nato pia angeshambulia kitovu cha nchi za Ulaya lakini maombi yalifanyika kwa uwazi zaidi lakini Urusi haijafanya chochote.
*Kama vile China aliposema kiongozi wa Marekani Pelosi akijaribu kwenda Taiwan ataishambulia Taiwan lakini yule mama alienda mchana kweupe kwa Air Force One ya Marekani na akaweka mkutano wa wazi zaidi China hakufanya chochote.

Na mengi yamefanyika ambayo Putin aliweka ndaro ataanzisha vita kamili lakini ameshindwa
*Pia Putin alisema endapo Ukrain watashambulia majimbo aliyoyapigia kura kuyapeleka urusi atakuwa ameshambuliwa Urusi na sasa atajibu kwa nuclear lakini kama unavyoona jimbo lile Kherson limerudi Ukraine putin hana nuclear wa mavi yoyote.

Sasa US na magharibi wamejua udhaifu wa Putin kwa nyanja zote wananfanya wanavyotaka, Biden juzi kaenda kutembelea Kyiv kwa mbwembwe zote, mkuu US ni taifa baya sana kwa technologia na wale jamaa kwenye hii vita wanatumai science sana kumdhoofisha Putin, Putin hakuwa calculation nzuri kuivamia Ukrean kwa sababu waliomshawishi walirudi nyuma sana walimuacha mkono sasa urusi inakufa peke yake.

China na India nchi ambazo zinapata msaada sana kutoka US kuanzia wataalamu wa kiuchumi, viwanda, silaha lakini na kila kitu ndio maana China akijaribu kutaka kujiengua na US huwa anashindwa, Marekani aliitawala dunia muda mrefu sana ni shida sana taifa kama Marekani kulipigia mahesabu ya kuliangusha kama alivyojaribu putin
 
Kama nchi za Magharibi zimeamuwa kupigana vita ya mawakala na Urusi kupitia Ukraine basi washirika wa Urusi wana haki ya kumsaidia mshirika wao.
Supa pawa anasaidiwa tena? Au maji shingoni?
 
Kitu kizuri kuhusu China ni kuwa ana viwanda vingi, ana workforce kubwa, ana vyuma aina zote. Ni rahisi kutengeneza silaha kwa upesi.

Artillery kwake hazitakuwa na faida maana adui yuko mbali
 
Kugawanyika kiitikadi ni jambo la kawaida sana. Lakini kupambana waziwazi kivita kwa kugawa silaha maeneo ya vita na katika kipindi cha vita kwa makundi hasimu ni jambo jipya.
Utakuwa umezaliwa jana wewe sio Bure. Misaada ya kijeshi kwa wapinzani Kati ya Hao jamaa haijaanza Leo. Vita vya Korea (1950-1953) nchi za Magharibi ziliisaidia Korea kusini kijeshi huku USSR, China ziliisaidia Korea kaskazini. Vita vya Vietnam mpaka Warusi na WA China waliingiza wanajeshi wao kuisaidia Serikali ya Viet Congo. Kwahiyo sioni jipya hata China ikipeleka Silaha kuisaidia Urusi.
 
Majadiliano yanaendelea
Screenshot_20230222-151104.jpg
 
China na India nchi ambazo zinapata msaada sana kutoka US kuanzia wataalamu wa kiuchumi, viwanda, silaha lakini na kila kitu ndio maana China akijaribu kutaka kujiengua na US huwa anashindwa, Marekani aliitawala dunia muda mrefu sana ni shida sana taifa kama Marekani kulipigia mahesabu ya kuliangusha kama alivyojaribu putin
Aiiise hizi taarifa zako unapata wapi ?
 
*Kama vile China aliposema kiongozi wa Marekani Pelosi akijaribu kwenda Taiwan ataishambulia Taiwan lakini yule mama alienda mchana kweupe kwa Air Force One ya Marekani na akaweka mkutano wa wazi zaidi China hakufanya chochote.
Sio kweli
 
Waukrain huko wamepoteana maeneo yote manne kayadibithi nyie pambananeni na keyboard
 
Back
Top Bottom