China kuipatia silaha Russia dhidi ya Ukraine

China kuipatia silaha Russia dhidi ya Ukraine

Kama unaikubali urusi sasa wanaomba silaha kutoka China na Iran kwisha habari yao, tuliambiwa ni superpower vita ata miaka 2 haijaisha wanakopa silaha
Sasa silaha zako utatumia zote kabla ya vita halafu vita ikianza utumie nini? 🤣 Urusi sio mjinga kama unavyofikiri. Anapoomba silaha maana yake hataki bank yake ya masilaha iende chini ya kiwango. Kuna level ambayo unatakiwa ku maintain mda wote kwa ajili ya kujiandaa na vita.
 
Mafuta wamejipangia wenyewe wa magharibi na wafanyabiashara wao.....mrusi anaendelea kuuza mafuta kwa bei zake na tena soko lake limekua sana hasa china na india.......ndo maana kwa sasa ana jeuri ya kuagiza silaha nje badala ya kuzalisha mwenyewe ndani, pesa anapata na anaenda kuchukua silaha kwa wale ambao anawauzia mafuta kwa bei ya chini, kwahio upande mmoja unafanya production upande mmoja unanunua vita inaendelea,,,,,shida kwa nato gharama za uzalishaji zimeshakua kubwa ulaya nzima nafuu ipo marekani tu vita ikiendelea stock zao kuzirudishia itakua ngumu ndo maana mjerumani alikua anajikuna kichwa kwenye vifaru,,,kuzalisha silaha zinazotoka ulaya kwa rate ya kuendana na vita ukraine kwa sasa ni ngumu, tena wakihamia kwenye hizi silaha modern shida itakua kubwa zaidi gharama za uzalishaji zinaenda kua chini india na china sababu wanauziwa mafuta na gesi kwa bei ndogo sana kulinganisha masoko mengine, mrusi anajua anachofanya.........................na ujinga mwingine india na china wananunua mafuta bei chee urusi halafu na wao wanakuja tena kuwauzia ulaya kwa gharama kubwa anaeumia anajulikana ila bado anajikazaView attachment 2524334View attachment 2524336
India anawapiga hela Europe kwa mafuta yale yale waliokataa kununua bei chee kwa Mrusi 🤣🤣🤣
 
Nchi gani ulaya ina nguvu kijeshi na kiuchumi kuliko china?? China size yake ni marekani na Russia. China sio aliogopa kumpa Russia silaha kwa sababu ya vikwazo, muda wa kumpa Russia silaha ulikuwa bado na utakapofika hakuna nchi yoyote itakayoweza kumzuia. Jambo ambolo wengi wenu hamlifahamu ni kwamba china na Russia ni kitu kimoja. China ilikuwa inafahamu kila kitu kuhusu hii operation kabla hata haikuanza
Waambie hao, hili jambo lilifanywa kwa timming na ndio maana linakwenda vizuri tu. 😀 😀 😀 Watu wanahisi Urusi alikurupuka tu.
 
Najiulizaga sana US wanajiamini nini kumnyooshea kidole kila mtu.
Waxenge tu wanategemea TAG team. Bila ushirika US ni mwepesi mno na hilo analijua. Ila kwa Russia ni moto wa tipa yani halitaisha kirahisi lazma atalamba lolo.
 
Hakuna nchi rafiki ambazo zitaweza kuziba pengo la soko la Ulaya Urusi alilokuwa nalo sasa anakopesha India labda na china kwa hasara zaidi, tutegemee anguko kubwa zaidi la urusi kiuchumi
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Anakopesha au anauza kwa discount, tofautisha hayo mawili.
 
Ni Sawa tu,
Bado KK nayo itaipa Urusi silaha,Iran tayari.
Hii maana yake Kila mtu na maswahiba wake.
N ndivyo hata NATO wakiingiza majeshi kamili nao wachina watatia timu uwanjani,bila kumsahau kiduku na marafiki wengine.
Ndio hapo Urusi yenu itachakazwa kama kumbusu msichana. Putin siku zinahesabika za kuokotwa kwenye shimo la maji taka
 
Kama china anamsaidia Urusi ndio mwisho wa china. Trust me
Jiongopee hivyo hivyo wakati kuna miradi kibao ya SINO inaendelea nchini. Electronics zilizojazana Kariakoo ni za kichina. Maguta mapikipiki, malori ya FAW, Howo, SHACMAN yamejazana mjini.. Viwanda vya mabati, Mashine kibao za kichina, Motor, Pump, diesel engine. Endeleeni kujidanganya hivyo hivyo.

Jiulize china amezifikia nchi ngapi Africa?
 
Kuna mahali watu walishabikia urusi kupotea nikawaambia
Urusi pia ana washirika naye atapata misaada pale anapohitaji vita bado ni ngumu
 
Putini anazo hizo ndoto kweli kuzima ya magharibi lakini amechelewa sana mkuu., Putin alijua atawaparaganya wa magharibi lakini ndio kwanza zile nchi 30 na nyengine nyingi zimo mbioni kuungana na Nato tena ndio nchi mataifa yenye nguvu zaidi duniani.

Putin alidhani ataiangusha magharibi lakini kumbe hakuwa prepared, hana uwezo sasa ni aibu nchi tuliyoambiwa ni superpower anakodi silaha kutoka Iran vita ina mwaka tu, hana jeshi anakodi makundi ya kigaidi sasa, baada jeshi lake kufyekwa akalazimisha raia wa miaka 18-50, sasa wafungwa lakini ametangaza Internationly watu ambao watajitokeza duniani wende wakasajiliwe wapewe mafunzo siku mbili tatu halafu wapelekwe chambo Ukraine. Raymond Mtanzania alienda nadhan umesikia.

Magharibi wanasema wamepata muda muafaka sana kumshughulikia Putin., pole pole taifa la Russia linaenda kupotea
Nawewr unafurahia anguko la Putin dhidi ya mashetani wa NATO?
 
Let's say Russia ameshindwa the next is China! so china asipo mpa support anajua atafata.
China lazma hii vita atapigana bega kwa bega na Urusi. Come what may but hio ndio only option atake asitake hawatamuacha. Marekani ni mchawi mkuu wa genge la NATO. Hapendi mtu ainuke zaidi yake na analiona hilo kwa China. Mbeleni pia Kiduku lazma ataingia kuongeza nguvu maana anaichukia US kama harufu ya choo.

Kwa mtazamo tu nafikiri waliona wakimuanzishia China basi Urusi angeingilia moja kwa moja kama ilivyokuwa Afghanistan kule. Wakaona bora waanze na Urusi kwa kuanzisha zogo Ukraine kwa ahadi kuwa watamuingiza NATO huku wakimchimba beat china maana hana uzoefu na vita. Ngoma inaelekea kunoga sasa.
 
Sasa si wajitokeze wazi kumsaidia?!!kama nchi za ulaya zinavyofanya?!!wanaogopa nini?
Vita haijatangazwa rasmi. Ila Marekani na Europe hashindi safari hii maana sio wote ni war mongers. Wanaeza muachia marekani na mwingereza waicheze ngoma wenyewe.
 
Huo umoja wao BRICS sasa ni miaka 22 toka wauunde kuna nini wamekifanya ili kujinusuru na hali hiyo?!!kwani wengi waliamini kuwa huo umoja ndio mwisho wa ubabe wa magharibi?sio jambo rahisi hivyo kusema kuwa eti dolar isitumike kwenye biashara za kimataifa?!!huyo mrusi wakati vita inaanza akatoa amri watumiaji wote wa gesi yake walipe kwa rubble,nchi za ulaya zikalataa alifanya nini?
Kwani anawauzia bila rubble sahizi? Wasiotaka Rubble wakanunue gesi China na India 😀😀😀
 
Mrussi afanye Kama kakosea vile adondoshe baruti pale NYC kipigo atakacho pokea wale wa mpitimbi na songoro wata saga meno
 
Sasa hiyo bricks nayo ina impact gani toka iundwe?!!lazima dunia iwe na kilanja mkuu wa kuweka mambo sawa!!hao china,urusi,iran,n.korea wao kitu demokrasia na uhuru wa watu kwao sio kipaumbele.kwakuwa UN imeshindwa kufanya majukumu yake ipasavyo ndio maana US anakuwa ndio kama UN!!Na hii dunia kama putin ndio angekuwa kilanja wa dunia kusingekuwa kuwa na dunia tena
Brics hawako kumpelekesha mtu, wanataka kila nchi ijiendeshe kivyake sio kuwe na kiranja wa kupangia wenzake kwamba sahizi hatumtaki yule tukampige. Flani ana hela sana sahizi hatuskilizi tukamuue raisi wake. Sahizi tupitishe sheria za mashoga kuoana asiyetaka tunamuwekea vikwazo. Sahizi hatutaki flani afanye biashara na flani akigoma tumpige vikwazo.

Hayo sio mambo ya BRICS. Wenyewe ni watu wa haki na usawa. Kama biashara kila mtu afanye kwa uhuru na yeyote anaeona ana maslahi kwake. Kila mtu na pesa yake sio kulazimishana kutumia dollar tu.
 
Vita haijatangazwa rasmi. Ila Marekani na Europe hashindi safari hii maana sio wote ni war mongers. Wanaeza muachia marekani na mwingereza waicheze ngoma wenyewe.
Huyu bwana putin zamu hii ameyakanyanga,NATO hawamuachi na hata hotuba ya jana ya BIDEN inaonyesha kuwa wako pamoja sana!!Putin amemuomba CHINA awe mpatanishi ili vita iishe ila hizo ni za ndaniiii
 
Huyu bwana putin zamu hii ameyakanyanga,NATO hawamuachi na hata hotuba ya jana ya BIDEN inaonyesha kuwa wako pamoja sana!!Putin amemuomba CHINA awe mpatanishi ili vita iishe ila hizo ni za ndaniiii
China huyu huyu anayetaka kutuma silaha
 
Zama za udikteta ziishe tena mkuu, putin hataki kuondoka madarakan ni kama M7 wa uganda au Kim wa North Korea
Kwani ishu ni kuondoka madarakani au ishu ni kuinfluence dunia? Mbona nyie CCM wako madarakani toka kuasisiwa kwa nchi na hamuwatoi.
 
Back
Top Bottom