China kuivamia Taiwan muda wowote - Makamu Wizara NJE Taiwan

China kuivamia Taiwan muda wowote - Makamu Wizara NJE Taiwan

Pale NYUMBU production zinaendeleje? Tuuzeni SILAHA jamani biashara imechangamka.
 
Uongo mkuu,China haina uoga wowote ule dhidi ya USA.
Hata kama wamezungukwa hizo nchi hazina ubavu wa kuruhusu Dongefeng ballistic missiles zitue katika ardhi zao sio Phillipines wala nchi yeyote hapo.
Isipokuwa China imejikita katika vitisho na diplomasia zaidi maana Taiwan ni sehemu ya China,China haina sababu ya kutumia mabavu.
Kama hao USA wa maana sana kwanini hawakumsaidia Phillipines arejeshe visiwa vyake vilivyotekwa pale South China Sea!?
Hadi leo hii Philippines wanalilia hivyo visiwa na ni mwaka juzi tu China ameviteka kwao.
China hapendi kuendekeza vita ila haogopi vita.
Huyo USA anajua mziki wa China mwaka 1959 pale Jangsari Korea.
Umesema vyema mkuu
 
Sidhani kama vita itatokea, China wako makini sana linapokuja suala la Vita, hasa kipindi hichi wanachopambana kupandisha uchumi wao na teknolojia yao ili kui overtake USA, xi jinping si tahira kama Trump
 
Jamaa kasema majukwaa yapo mengi chagua moja uende huko sio unavamia sehemu usizozijua nimemuelewa sana wacha mimi Mchina wa Kimara Suca niende zangu huko..
 
Hii kauli mwaka wa ngapi sasa
 
1950 isingekuwa Korean war hawa walikuwa wanavamiwa mpaka huko kisiwani walipo kimbilia
Jinping lazima atairufisha tu, ndugu zao wa dsmu kabosa hawa
 
Jinping lazima atairufisha tu, ndugu zao wa dsmu kabosa hawa
Mwaka 2027 PLA inatimiza miaka 100 na mwaka 2049 Jamhuri ya watu wa China inatimiza miaka 100 kabla ya 2027 au 2049 kabla hii miaka kuna harufu ya Taiwan kuunganishwa.

Marekani wenyewe wanasema wana jiandaa na vita na China 2027 wanasema ndio mwaka China itafanya uvamizi sijui ni kweli ama laah! Pentagon wanajua zaidi mambo mengi kuliko mimi tusubiri hiyo 2027

Lakini nina uhakika kabla ya 2049 Taiwan itaunganishwa
 
naunga mkono
 
Washirika wa Taiwan wapo hoi na vita vya Ukraine.... Pale Taiwan patakua pepesi sababu ni kisiwa, hivyo itawekwa marufuku ya meli yoyote kuja Taiwan au ndege kutua huku jicho la beidui likiwa linamulika chochote kinachojaribu kuingia Taiwan.

Hii mechi naitamani kwelikweli sababu naamini yataanza mazoezi ya kijeshi ya wafalme wawili wa mashariki yatakayoishia kukifunga hiki kisiwa
Kwani yule mwanamama aliingiaje Taiwani baada ya China kupiga biti asitembelee Taiwani? Nakumbuka aliingia kwa ndege na akatoka kwa ndege, hivyo hivyo na silaha zitakuwa zinaingia Taiwani kama vita vitatokea.
 
Back
Top Bottom