China has always been a great nation on the planet, ni watu wachache wasiofahamu ndiyo huwa wanapingana na hili. Mnamo karne ya 18 na 19 Uchina ndiyo lilikuwa taifa kubwa na tajiri likifuatiwa na India. Mnamo miaka ya 1800's Uchina alikuwa anamiliki zaidi ya asilimia 30% ya Uchumi wa dunia.
Uchina, Uajemi (Iran) na Israeli ndiyo jamii kongwe zaidi duniani ambazo tamaduni zao zina miaka zaidi ya 6000 na bado ziko vilevile na kwenye maeneo yaleyale. Professor Ian Morriss kwenye kitabu chake cha WHY THE WEST RULES FOR NOW, anaelezea kwamba The Ming Dynasty ya Uchina ndilo taifa lililokuwa na teknolojia ya kisasa duniani pia taifa lililokuwa limestaarabika sana mnamo karne ya 14.
Wao ndiyo walikuwa wa kwanza kufika pwani ya Afrika Mashariki miaka 90 kabla ya bwana Vasco Da Gama. Zheng He alipewa meli mia tatu na mabaharia 27000 ili afanye safari za majini na kutengeneza mahusiano ya kidiplomasia duniani kote. Lakini bahati mbaya wafalme wa Uchina waliamini kwamba wao hawaihitaji dunia na wakaanza kuchoma manowari moto ili kuzuia safari za nje, Ulaya ikawakuta kiteknolojia, kuwapita na kuwatala.
Lakini ukweli ni kwamba Uchina imegundua mambo mengi sana hapa duniani. Gobole la kwanza lilitengenezwa Uchina mnamo karne ya 11, pia unga wa bunduki (gun-powder) iligunduliwa Uchina. Teknolojia ya kutengeneza majahazi ya kisasa kabisa kwa kipindi hicho ilikuwa Uchina. Ulaya iliiba teknolijia nyingi sana za Uchina na kuzitumia kuvuruga dunia nzima.
Sasa leo unapoona wachina wanafanya haya, siyo jambo la kushangaza kabisa. Wamekuwa hivi vizazi na vizazi, na wao ni watu wanaomini kwamba nchi yao ndiyo kitovu cha dunia (Center of the world). Mwanajiografia wa Kiitaliano, Bwana Mateo Ricci alipelekea kwa mfalme wa Uchina ramani ya dunia ambayo tunaitumia leo itokanayo na The Mercator Projection, ambayo inaonyesha Ulaya na Afrika zikiwa katikati. Mfalme wa Uchina na baraza lake walighafirika sana ikabidi jamaa abadilishe haraka sana.
Ramani za kale za Uchina zinaonyesha kwamba Uchina iko katikati ya dunia, yaani wao ndiyo The Middle-Kingdom. Haka kaugonjwa wanako mpaka leo hii na sumu yake inasambazwa na chama cha kikomunisti cha Uchina. Marekani na Ulaya wanafahamu dhahiri kwamba siku Uchina akiwashinda nguvu basi lazima atawaumiza na kulipiza waliomfanyia mnamo karne za 18 na 19: Wazungu wanaogopa mnoo.
Ukiwafuatilia wataalamu wa Ulinzi na Usalama wa Marekani na Ulaya wanasema Uchina ndiyo tishio kubwa kuwahi tokea kwa ustaarabu wa Magharibi kwa kipindi cha miaka 500. Maana kipindi hicho chote wamekuwa wakipigana wazungu kwa wazungu. Yaani Saxons-Romans/Latins-Slavs ambayo ni mataifa ya Ujerumani, Uingereza, Marekani, Urusi, Ufaransa, Uhispania, Ureno n.k ambayo yana mila na tamaduni zinazofanana. Lugha zao zina mizizi ya Kigiriki na Kilatini (Greco--Romano), dini yao ni Ukristo wa Kiyahudi (Judeo-Christian)
Pia kibaolojia wao ni watu weupe wenye macho ya kijani na bluu (Caucasians). Lakini Wachina ni ustaarabu mwingine kabisa ambao haushabihiani kabisa na chochote kile cha Ulaya, kuanzia lugha, dini, mfumo wa maisha na hata maumbile ya kibaolojia. Nchi za Magharibi zinaogopa kabisa kutokewa na kile ambacho Karne za nyuma zilinusurika kuwakuta kupitia The Mongols na Ottomans ambao walitaka kuvuruga kabisa tamaduni zao.
Bila Mungu kuingilia kati na kumuondoa Mongke Khan ambaye alikuwa anapeleka jeshi lake Vatican basi leo hii Ulaya ingekuwa ni ya tofauti sana. AU waturuki wakina Mehmed wangefanikiwa kupandisha Ulaya na kufika Urusi, basi Ulaya ingeweza kuwa ni bara la kiislamu. Sasa mambo kama haya yamewakaa sana Ulaya na kuwaogopesha.
Lakini kubwa ambalo linawatatiza ni kwamba tofauti kabisa na Afrika na Marekani, bara la Asia halikuzikubali tamaduni za Magharibi kirahisi. Ukristo upo lakini siyo kwa kiwango kama cha Afrika au Marekani Kusini, lakini pia tamaduni za wenzetu zimekuwa na nguvu kuliko ushawishi wa Magharibi. Ukienda Korea, Japan, India, Thailand na kwingineko, tamaduni zao zina nguvu sana.
NIKIRUDI KWENYE HILI LA UCHINA NA TEKNOLOJIA YA ANGA SASA:
Marekani na Urusi walianza kuwafanyia figisu Uchina tangu miaka ya 70 kwa kuzuia wachina wasitengeneza satelaiti zao na kuzirusha angani. Aliweka vikwazo vizito kwa Uchina, lakini wachina wakarusha The Dong-Fang 1 bila msaada wa nchi yoyote ile. Tena inasemekana ile satelaiti ilikuwa na uwezo mkubwa kwenye baadhi ya mambo kuliko nchi nyingine.
Miaka ya tisini wamarekani walifanya figisu sana lakini bahati mbaya Urusi ikawa imeanguka na teknolojia yake iliibwa sana na Uchina, hasa ile ya anga. Alifanikiwa sana kupiga hatua kali kiteknolojia miaka ya tisini kuliko kipindi chochote kile. Marekani chini ya George Bush Sr walikosea kuweka vipaumbele vyao kiulinzi, waliamini adui mkubwa ambaye anafaa kushughulikiwa mapema ni mataifa ya Kiislamu.
Ametumia pesa nyingi mno kupambana mashariki ya kati huku Uchina anapiga hatua kimya kimya. Ukisoma majarida ya miaka ya tisini na kuwauliza wataalamu wa Magharibi kuhusu matishio ya Usalama kipindi hicho wangekuambia ni Sadam Hussein, Mullah Omar, Slobodan Milosevic na Mohamed Rasfanjani. Ila Jiang Zemin na Hu Juntao walidhaniwa kuwa wanaongoza A Bamboo Nation ambalo litaanguka muda wowote ule.
Mwaka 1996 (Taiwan Strait Crisis) Clinton alimfurumusha Jiang Zemin kule Taiwan baada ya kupelekea manowari kubwa za kijeshi hadi Uchina akaufyata, alikuwa hana uwezo kama alionao leo. Lakini leo hii Marekani hana huo msuri wa kumtisha kabisa na akijaribu yanaweza kumkuta makubwa, A genie is out of the bottle.
Uchina anaongoza kwenye 5G na 6G mpaka sasa, na kama akifanikiwa kupeleka Kituo chake cha anga basi tegemea kituo hicho kutumika kama sehemu ya biashara ya usafiri wa anga, maana hiki kilichopo sasa wanataka kukifanyia marekebisho makubwa sana ambayo yatahitaji gharama. Kituo cha Uchina kitakuwa na zaidi ya tani 66 na kikubwa sana kiasi ambacho kinaweza kutumiwa hadi na wanasayansi kutoka NASA.
Space-Programme ya Uchina ikiwa Commercialised basi utasikia mataifa mengi ambayo hata hayana uwezo mkubwa yanajiunga nayo. Hili litapunguza Monopoly ambayo Marekani na Urusi wamekuwa nayo kwa miaka mingi. Uchina ana pesa na teknolojia ya kuwezesha haya kufanyika kwa haraka, na Marekani analifahamu hilo......
Walipofika Uchina leo, Marekani ameshachelewa sana cha msingi ni kujenga ushirikiano kwenye mambo muhimu na kubakiza ushindani kwingine. Ambaye anatakiwa kulaumiwa kwa Uchina ilipofika hapa ni Richard Nixon na Henry Kissinger.......
AU NASEMA UONGO NDUGU ZANGU............