China kupeleka chombo Mars na kuanzisha space station inawauma sana Marekani na washirika wake

Marekani na washirika wake wanaumia sana China kuja juu katika anga za mbali. Wanatamani tu wafeli au vyombo walivyo tuma vilipuke.

Mwezi huu wa tano chombo cha China kitatua Sayari ya Mihiri Mars. Tayari kimeshaingia Orbit ya Mars ikiizunguka nakuchagua sehemu muafaka ya kutua.

Pia tayari jana China imeshatuma kipande cha kwanza cha space station capsule. Zoezi hili lingeanza mapema lakini Janga la Corona limeichelewesha. China inataka kujenga space station yao ambayo itakuwa tofauti na ile international space station.

Mafanikio haya makubwa ya China katika anga za mbali inawaumiza nakuwauma sana Marekani hawana cha kufanya. Hata kwenye vyombo vyao vya habari kimya.

Elon musk na NASA kelele mingii lakini mwanaume China anafanya mambo ya uhakika kimya kimya.

Sasa hivi wanaombea tu chombo cha China kisifike salama sayari ya Mars.

Mungu ibariki China katika harakati zake za kuchana mbuga kwenye technology

Waamerika wataunda kirusi kingine cha mafua na safari hii watakitupa Beijing sio Wuhan.
 
Mkuu unajua chombo cha kwanza cha US kilitua mwaka gani Mars?
Kumbuka pia mwaka huu chombo cha Wamarekani kingine kiko Mars ikiwemo mink helcopter.
Elon Musk yeye anachotaka kufanya ni kufanya usafiri wa anga za mbali uwe kama utalii na affordable.

Ila hata mimi ninakubaliana na wewe kuwa Wachina ni noma. US na wivu wake akishirikiana na nchi za ulaya walimshinda kauli mrusi eti mchina asishiriki nao kwenye matumizi ya space station. Mchina now one man show anatengeneza yake, na bado chombo chake alichotuma mwezini kimefika sehemu ya mbali zaidi ambayo haikuwahi kuchunguzwa kabla.
 
Wakati unaponda unatakiwa ukumbuke uchumi wa dunia ya leo umetengenezwa na kushikiliwa na Marekani. Marshall plan iliokoa uchumi wa dunia na bado nchi za Asia karibu zote ni Marekani ndio amezibeba kuwa hapo zilipo. China yenyewe unayoimwagia sifa imeendelea kwa sababu Marekani iliamua kuwekeza viwanda vyake pale na hadi leo bado vipo.

China ni kinara wa wizi wa intellectual property kutoka makampuni ya magharibi. Siku Marekani akiondoka soko la China anawabana tu kutumia teknolojia yake na huo ndio utakuwa mwisho wao.

China amesaidia nini dunia hadi sasa?
Kataa ukubali, haijalishi nini America imefanya lakini nchi iliyokuwa almost na uchumi unalingana na Tanganyika leo kuwa nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani ni jambo ambalo linastahili pongezi.

Pia wawe wnaiba technology au hawaibi nako kuiba kunahitaji maarifa, sisi hata tupewe formula bado tutafail.
 
Mleta mada anavyowapamba wachina kana kwamba wamekuja kutuokoa kutoka kwa mmarekani wakati ni washenzi tu.

mkuu hatukuwahi kuwakaribia china kiuchumi. Huo ni uongo ambao umerudiwa sana sasa unaonekana kama ukweli.
 
Marekani na washirika wake wanaumia sana China kuja juu katika anga za mbali. Wanatamani tu wafeli au vyombo walivyo tuma vilipuke.

Mwezi huu wa tano chombo cha China kitatua Sayari ya Mihiri Mars. Tayari kimeshaingia Orbit ya Mars ikiizunguka nakuchagua sehemu muafaka ya kutua.

Pia tayari jana China imeshatuma kipande cha kwanza cha space station capsule. Zoezi hili lingeanza mapema lakini Janga la Corona limeichelewesha. China inataka kujenga space station yao ambayo itakuwa tofauti na ile international space station.

Mafanikio haya makubwa ya China katika anga za mbali inawaumiza nakuwauma sana Marekani hawana cha kufanya. Hata kwenye vyombo vyao vya habari kimya.

Elon musk na NASA kelele mingii lakini mwanaume China anafanya mambo ya uhakika kimya kimya.

Sasa hivi wanaombea tu chombo cha China kisifike salama sayari ya Mars.

Mungu ibariki China katika harakati zake za kuchana mbuga kwenye technology
Ok
 
China has always been a great nation on the planet, ni watu wachache wasiofahamu ndiyo huwa wanapingana na hili. Mnamo karne ya 18 na 19 Uchina ndiyo lilikuwa taifa kubwa na tajiri likifuatiwa na India. Mnamo miaka ya 1800's Uchina alikuwa anamiliki zaidi ya asilimia 30% ya Uchumi wa dunia.

Uchina, Uajemi (Iran) na Israeli ndiyo jamii kongwe zaidi duniani ambazo tamaduni zao zina miaka zaidi ya 6000 na bado ziko vilevile na kwenye maeneo yaleyale. Professor Ian Morrisson kwenye kitabu chake cha WHY THE WEST RULES FOR NOW, anaelezea kwamba The Ming Dynasty ya Uchina ndilo taifa lililokuwa na teknolojia ya kisasa duniani pia taifa lililokuwa limestaarabika sana mnamo karne ya 14.

Walo ndiyo walikuwa wa kwanza kufika pwani ya Afrika Mashariki miaka 90 kabla ya bwana Vasco Da Gama. Zheng He alipewa meli mia tatu na mabaharia 27000 ili afanye safari za majini na kutengeneza mahusiano ya kidiplomasia duniani kote. Lakini bahati mbaya wafalme wa Uchina waliamini kwamba wao hawaihitaji dunia na wakaanza kuchoma manowari moto ili kuzuia safari za nje, Ulaya ikawakuta kiteknolojia, kuwapita na kuwatala.

Lakini ukweli ni kwamba Uchina imegundua mambo mengi sana hapa duniani. Gobole la kwanza lilitengenezwa Uchina mnamo karne ya 11, pia unga wa bunduki (gun-powder) iligunduliwa Uchina. Teknolojia ya kutengeneza majahazi ya kisasa kabisa kwa kipindi hicho ilikuwa Uchina. Ulaya iliiba teknolijia nyingi sana nza Uchina na kuzitumia kuvuruga dunia nzima.

Sasa leo unapoona wachina wanafanya haya, siyo jambo la kushangaza kabisa. Wamekuwa hivi vizazi na vizazi, na wao ni watu wanaomini kwamba nchi yao ndiyo kitovu cha dunia (Center of the world). Mwanajiografia wa Kiitaliano, Bwana Mateo Ricci alipelekea kwa mfalme wa Uchina ramani ya dunia ambayo tunaitumia leo itokanayo na The Mercator Projection, ambayo inaonyesha Ulaya na Afrika zikiwa katikati. Mfalme wa Uchina na baraza lake walighafirika sana ikabidi jamaa abadilishe haraka sana.

Ramani za kale za Uchina zinaonyesha kwamba Uchina iko katikati ya dunia, yaani wao ndiyo The Middle-Kingdom. Haka kaugonjwa wanako mpaka leo hii na sumu yake inasambazwa na chama cha kikomunisti cha Uchina. Marekani na Ulaya wanafahamu dhahiri kwamba siku Uchina akiwashinda nguvu basi lazima atawaumiza na kulipiza waliomfanyia mnamo karne za 18 na 19: Wazungu wanaogopa mnoo.

Ukiwafuatilia wataalamu wa Ulinzi na Usalama wa Marekani na Ulaya wanasema Uchina ndiyo tishio kubwa kuwahi tokea kwa ustaarabu wa Magharibi kwa kipindi cha miaka 500. Maana kipindi hicho chote wamekuwa wakipigana wazungu kwa wazungu. Yaani Saxons-Romans-Slavs ambayo ni mataifa ya Ujerumani, Uingereza, Marekani, Urusi, Ufaransa, Uhispania, Ureno n.k ambayo yana mila na tamaduni zinazofanana. Lugha zao zina mizizi ya Kigiriki na Kilatini (Greco--Romano), dini yao ni Ukristo wa Kiyahudi (Judeo-Christian)

Pia kibaolojia wao ni watu weupe wenye macho ya kijani na bluu (Caucasians). Lakini Wachina ni ustaarabu mwingine kabisa ambao haushabihiani kabisa na chochote kile cha Ulaya, kuanzia lugha, dini, mfumo wa maisha na hata maumbile ya kibaolojia. Nchi za Magharibi zinaogopa kabisa kutokewa na kile ambacho Karne za nyuma zilinusurika kuwakuta kupitia The Mongols na Ottomans ambao walitaka kuvuruga kabisa tamaduni zao.

Bila Mungu kuingilia kati na kumuondoa Mongke Khan ambaye alikuwa anapeleka jeshi lake Vatican basi leo hii Ulaya ingekuwa ni ya tofauti sana. AU waturuki wakina Mehmed wangefanikiwa kupandisha Ulaya na kufika Urusi, basi Ulaya ingeweza kuwa ni bara la kiislamu. Sasa mambo kama haya yamewakaa sana Ulaya na kuwaogopesha.

Lakini kubwa ambalo linawatatiza ni kwamba tofauti kabisa na Afrika na Marekani, bara la Asia halikuzikubali tamaduni za Magharibi kirahisi. Ukristo upo lakini siyo kwa kiwango kama cha Afrika au Marekani Kusini, lakini pia tamaduni za wenzetu zimekuwa na nguvu kuliko ushawishi wa Magharibi. Ukienda Korea, Japan, India, Thailand na kwingineko, tamaduni zao zina nguvu sana.

NIKIRUDI KWENYE HILI LA UCHINA NA TEKNOLOJIA YA ANGA SASA:
Marekani na Urusi walianza kuwafanyia figisu Uchina tangu miaka ya 70 kwa kuzuia wachina wasitengeneza satelaiti zao na kuzirusha angani. Aliweka vikwazo vizito kwa Uchina, lakini wachina wakarusha The Dong-Fang 1 bila msaada wa nchi yoyote ile. Tena inasemekana ile satelaiti ilikuwa na uwezo mkubwa kwenye baadhi ya mambo kuliko nchi nyingine.

Miaka ya tisini wamarekani walifanya figisu sana lakini bahati mbaya Urusi ikawa imeanguka na teknolojia yake iliibwa sana na Uchina, hasa ile ya anga. Alifanikiwa sana kupiga hatua kali kiteknolojia miaka ya tisini kuliko kipindi chochote kile. Marekani chini ya George Bush Sr walikosea kuweka vipaumbele vyao kiulinzi, waliamini adui mkubwa ambaye anafaa kushughulikiwa mapema ni mataifa ya Kiislamu.

Ametumia pesa nyingi mno kupambana mashariki ya kati huku Uchina anapiga hatua kimya kimya. Ukisoma majarida ya miaka ya tisini na kuwauliza wataalamu wa Magharibi kuhusu matishio ya Usalama kipindi hicho wangekuambia ni Sadam Hussein, Mullah Omar, Slobodan Milosevic na Mohamed Rasfanjani. Ila Jiang Zemin na Hu Juntao walidhaniwa kuwa wanaongoza A Bamboo Nation ambalo litaanguka muda wowote ule.

Mwaka 1996 (Taiwan Strait Crisis) Clinton alimfurumusha Jiang Zemin kule Taiwan baada ya kupelekea manowari kubwa za kijeshi hadi Uchina akaufyata, alikuwa hana uwezo kama alionao leo. Lakini leo hii Marekani hana huo msuri wa kumtisha kabisa na akijaribu yanaweza kumkuta makubwa, A genie is out of the bottle.

Uchina anaongoza kwenye 5G na 6G mpaka sasa, na kama akifanikiwa kupeleka Kituo chake cha anga basi tegemea kituo hicho kutumika kama sehemu ya biashara ya usafiri wa anga, maana hiki kilichopo sasa wanataka kukifanyia marekebisho makubwa sana ambayo yatahitaji gharama. Kituo cha Uchina kitakuwa na zaidi ya tani 66 na kikubwa sana kiasi ambacho kinaweza kutumiwa hadi na wanasayansi kutoka NASA.

Space-Programme ya Uchina ikiwa Commercialised basi utasikia mataifa mengi ambayo hata hayana uwezo mkubwa yanajiunga nayo. Hili litapunguza Monopoly ambayo Marekani na Urusi wamekuwa nayo kwa miaka mingi. Uchina ana pesa na teknolojia ya kuwezesha haya kufanyika kwa haraka, na Marekani analifahamu hilo......

Walipofika Uchina leo, Marekani ameshachelewa sana cha msingi ni kujenga ushirikiano kwenye mambo muhimu na kubakiza ushindani kwingine. Ambaye anatakiwa kulaumiwa kwa Uchina ilipofika hapa ni Richard Nixon na Henry Kissinger.......

AU NASEMA UONGO NDUGU ZANGU............
Asante kwa darasa ulilotupa.
 
Mkuu wewe umeniathiri sana!
Nilianza kukufuatilia 2010 au na 11 natumia simu ya mzazi. Nipo kidato cha 4. Safari inaendelea mpaka nafika Chuo nakufuatilia tu ikafika mahala Nikaanza kumfuatilia Prof. Stephen Cohen (ambaye ni marehemu kwa sasa). Nikaanza kufuatilia haya mambo kwa kadri nilivyoweza.

Athari niliyopata mambo mengi ya ujana yamenipita. Sijui mambo mengi sana ya ujana mpaka wezangu wananishangaa! Nikichangia WhatsApp wenzangu wananishangaa nashindwa kifupisha maneno. Kingine kufuatilia hizi mada zimenifanya nafikiri na nazungumza kiutuuzima kuliko umri wangu. Sikuligundua ila nimemabiwa!

Kingine kwa kile nilichokijua kwa kujifunza kupitia kwako na kwa wa mfano wako naona kama nimejitwisha mzigo mzito sana! Mfano kama ulichochangia kwenye Uzi wa Chige huwa najiuliza unawezaje kuhimili mambo makubwa mnoo kwenye moyo!Samahani kwa kutoka nje ya mada!

Kwa sasa nahangaika kurudisha ujana wangu.

AU NASEMA UONGO NDUGU ZANGU!
 
Mkuu unajua chombo cha kwanza cha US kilitua mwaka gani Mars?
Kumbuka pia mwaka huu chombo cha Wamarekani kingine kiko Mars ikiwemo mink helcopter.
Elon Musk yeye anachotaka kufanya ni kufanya usafiri wa anga za mbali uwe kama utalii na affordable.

Ila hata mimi ninakubaliana na wewe kuwa Wachina ni noma. US na wivu wake akishirikiana na nchi za ulaya walimshinda kauli mrusi eti mchina asishiriki nao kwenye matumizi ya space station. Mchina now one man show anatengeneza yake, na bado chombo chake alichotuma mwezini kimefika sehemu ya mbali zaidi ambayo haikuwahi kuchunguzwa kabla.
Halafu watu bado wanamkataa mchina
 
Hahaha Ustaadh umezingua sana, hizi ni mbwembwe tu jamaa yangu!
Unafikiri!

Vuta picha niliacha kusikiliza mziki, radio na vipindi vingi vya local channels tangu nina miaka 19. Nikawa nasoma mambo yenu na kujishughulisha nayo mpaka nafika miaka 26. Ikipita siku bila kusoma sipati raha kabisa! Umri huo nasoma gazeti kwa sana nafuatilia taarifa za habari plus makala tofauti tofauti. Namkubali sana Nikola Tesla nikawa namsoma na kusikiliza documentary zake. Nikahamia kwa wazee wa dunia flat huko nikakesha mpaka basi!

Sasa nina miaka 28 kila vijana wenzangu wanachozungumza sikielewi!

Waliniambia unasikikiza singeli? Masikini ya Mungu hata maana yake sikuwa najua! Wakasema ngoja tukutoe ushamba wakanipeleka viwanja, loooh! Kumenishinda! Ni hatari mnoo! Kwangu kasi waliyonipeleka niliiona ni kubwa mnoo!

Nimemeamua kurudi tu kuanza kutafuta vitabu vya wanafalsafa wa west na wa east. Pembeni namsikilza Mex Cortez.
 
Wakati unaponda unatakiwa ukumbuke uchumi wa dunia ya leo umetengenezwa na kushikiliwa na Marekani. Marshall plan iliokoa uchumi wa dunia na bado nchi za Asia karibu zote ni Marekani ndio amezibeba kuwa hapo zilipo. China yenyewe unayoimwagia sifa imeendelea kwa sababu Marekani iliamua kuwekeza viwanda vyake pale na hadi leo bado vipo.

China ni kinara wa wizi wa intellectual property kutoka makampuni ya magharibi. Siku Marekani akiondoka soko la China anawabana tu kutumia teknolojia yake na huo ndio utakuwa mwisho wao.

China amesaidia nini dunia hadi sasa?
aache kujisaidia mwenyewe aisaidie dunia ili iweje

us atoe mambo yake ili UCHINA ianguke na kila mmoja ajisaidie mwenyewe

mbna UCHINA inawatesa[emoji38][emoji38]
 
Mkuu wewe umeniathiri sana!
Nilianza kukufuatilia 2010 au na 11 natumia simu ya mzazi. Nipo kidato cha 4. Safari inaendelea mpaka nafika Chuo nakufuatilia tu ikafika mahala Nikaanza kumfuatilia Prof. Stephen Cohen (ambaye ni marehemu kwa sasa). Nikaanza kufuatilia haya mambo kwa kadri nilivyoweza.

Athari niliyopata mambo mengi ya ujana yamenipita. Sijui mambo mengi sana ya ujana mpaka wezangu wananishangaa! Nikichangia WhatsApp wenzangu wananishangaa nashindwa kifupisha maneno. Kingine kufuatilia hizi mada zimenifanya nafikiri na nazungumza kiutuuzima kuliko umri wangu. Sikuligundua ila nimemabiwa!

Kingine kwa kile nilichokijua kwa kujifunza kupitia kwako na kwa wa mfano wako naona kama nimejitwisha mzigo mzito sana! Mfano kama ulichochangia kwenye Uzi wa Chige huwa najiuliza unawezaje kuhimili mambo makubwa mnoo kwenye moyo!Samahani kwa kutoka nje ya mada!

Kwa sasa nahangaika kurudisha ujana wangu.

AU NASEMA UONGO NDUGU ZANGU!
Wewe umejijuaje kwamba unayozungumza ni makunwa zaid ya umri wako
 
Marekani na washirika wake wanaumia sana China kuja juu katika anga za mbali. Wanatamani tu wafeli au vyombo walivyo tuma vilipuke.

Mwezi huu wa tano chombo cha China kitatua Sayari ya Mihiri Mars. Tayari kimeshaingia Orbit ya Mars ikiizunguka nakuchagua sehemu muafaka ya kutua.

Pia tayari jana China imeshatuma kipande cha kwanza cha space station capsule. Zoezi hili lingeanza mapema lakini Janga la Corona limeichelewesha. China inataka kujenga space station yao ambayo itakuwa tofauti na ile international space station.

Mafanikio haya makubwa ya China katika anga za mbali inawaumiza nakuwauma sana Marekani hawana cha kufanya. Hata kwenye vyombo vyao vya habari kimya.

Elon musk na NASA kelele mingii lakini mwanaume China anafanya mambo ya uhakika kimya kimya.

Sasa hivi wanaombea tu chombo cha China kisifike salama sayari ya Mars.

Mungu ibariki China katika harakati zake za kuchana mbuga kwenye technology
sasa nini amekifanya Marekani hadi ukajua kuwa roho inamuuma?
 
tunamshukuru kaleta tecno
Simu hizi za kujiwasha tochi ukiweka mfukoni? Hizi hizi ambazo hazina update? Km unatumia Lolipop ni hiyo hiyo hakuna update? Watu wapo android version 11 nawe upo 5.
Acha kumshirikisha Mungu kwenye vitu vya kijinga.
 
sasa nini amekifanya Marekani hadi ukajua kuwa roho inamuuma?
Sijaona hata makala inayoongelea kuwa wamerakani wamekereka.
Hao ni askari wa Jihad, wala usishangae maana muda wote wamejaa sumu kama wale wa Msumbiji.
Huko kwenye nyumba zao wameambiwa Marekani ni mbaya wao. Kwahiyo wanapoteza machungu
 
Marekani na washirika wake wanaumia sana China kuja juu katika anga za mbali. Wanatamani tu wafeli au vyombo walivyo tuma vilipuke.

Mwezi huu wa tano chombo cha China kitatua Sayari ya Mihiri Mars. Tayari kimeshaingia Orbit ya Mars ikiizunguka nakuchagua sehemu muafaka ya kutua.

Pia tayari jana China imeshatuma kipande cha kwanza cha space station capsule. Zoezi hili lingeanza mapema lakini Janga la Corona limeichelewesha. China inataka kujenga space station yao ambayo itakuwa tofauti na ile international space station.

Mafanikio haya makubwa ya China katika anga za mbali inawaumiza nakuwauma sana Marekani hawana cha kufanya. Hata kwenye vyombo vyao vya habari kimya.

Elon musk na NASA kelele mingii lakini mwanaume China anafanya mambo ya uhakika kimya kimya.

Sasa hivi wanaombea tu chombo cha China kisifike salama sayari ya Mars.

Mungu ibariki China katika harakati zake za kuchana mbuga kwenye technology
Sioni lolote la kipekee kwenye hili.. Watu wanapeleka orbiters na landers Mars kwa miongo kadhaa sasa..

Voyager 1&2 zipo nje ya solar system.. Kupeleka orbiter/lander kwa sayari iliyopo karibu zaidi na dunia haiwezi kuwa agenda kuu..

Kuhusu station yao; kwa namna ilivyo expensive ku-run ISS, nahisi hiyo itakuwa satellite ya kawaida tu kama zilivyo zingine.

Ngoja tuisome hiyo habari kwa kina.
 
Back
Top Bottom