China na Afrika zajivunia matunda ya ushirikiano wake kwenye vyombo vya habari

China na Afrika zajivunia matunda ya ushirikiano wake kwenye vyombo vya habari

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
8fe0a234a6a1533084c2cba7f8b85ab3.jpg



Kuanzia Agosti 19 hadi 21, Beijing ilipokea ugeni mzito kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Ugeni huu ulikuja kuhudhuria Mkutano wa 7 wa Ushirikiano wa Vyombo vya Habari kati ya China na Afrika, ambao uliandaliwa na Idara ya Taifa ya Redio na Televisheni, Serikali ya Manispaa ya Mji wa Beijing, na Umoja wa Mashirika ya Utangazaji Afrika.

Wakati mwaka 2026 ni wa maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Umoja wa Afrika, na pia ni Mwaka wa Mawasiliano baina ya Watu na Mawasiliano ya utamaduni baina ya China na Afrika; hivyo mkutano huu unaofanyika chini ya kaulimbiu“Kutumia pamoja Fursa Mpya za Maendeleo; Kuleta Mustakabali Mpya wa Vipindi vya Redio na Televisheni”, pia umejumuishwa kwenye shamrashamra mbalimbali za maadhimisho haya.

Likiwa ni jukwaa muhimu la kuimarisha mazungumzo na ushirikiano kati ya vyombo vya habari vya China na Afrika, mwaka huu ilifanyika mijadala ya kina kuhusu ubunifu wa maudhui na ushirikiano wa kiteknolojia, na kuhimiza utekelezaji endelevu na thabiti wa "Mpango wa Ushirikiano wa Ubunifu wa maudhui ya Redio, Filamu na Televisheni wa China-Afrika". Kuhimiza mawasiliano baina ya watu wa China na Afrika kupitia redio na televisheni, kuimarisha uwezo wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, na kufufua mawasiliano baina ya vijana.

Ikumbukwe kwamba mwaka 2022, Rais Xi Jinping alituma barua ya pongezi kwenye Mkutano wa Tano wa Ushirikiano wa Vyombo vya Habari kati ya China na Afrika, hatua ambayo ilitandika njia ya kuimarisha kwa kina ushirikiano huu. Kwani ilipofika mwaka 2024, Idara ya Utangazaji ya Taifa ilisaini mikataba ya ushirikiano na nchi za Afrika kama vile Côte d'Ivoire, Gabon, na Tunisia.

Ofisi ya Redio na Televisheni ya Manispaa ya Mji wa Beijing, kwa upande wake, ilianzisha sera ya kwanza ya ngazi ya mkoa, ambayo ililenga matangazo ya kimataifa ya maudhui ya video, pamoja na mfuko maalum wa kwanza wa ngazi ya mkoa nchini ili kusaidia matangazo ya kimataifa ya programu hizi.

Kutokana na juhudi hizi, tamthilia za kuvutia kama vile “Karibu katika Kijiji cha Milele” zimepata mafanikio makubwa kwenye skrini za nchi za Afrika, huku programu za burudani zilizoandaliwa kwa ushirikiano, kama vile “Sing for Africa”, zikiwaleta watazamaji karibu zaidi. Kati ya Septemba 2024 na mwishoni mwa Juni mwaka huu wa 2026, tamthilia 133 na makala 60 za maisha halisi zinazohusu kilimo zilitiwa sauti au kuwekewa maandishi kwa lugha za Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, na Kiswahili, na kutangazwa katika nchi kadhaa za Afrika.

Yakizingatiwa mafanikio ya mikutano 6 iliyopita, mkutano wa 7 unaofanyika mwaka huu unalenga kuunganisha rasilimali za sekta ya tamthilia na makala za maisha halisi baina ya China na Afrika, kuimarisha ushirikiano wa kivitendo, kuzidisha mawasiliano baina ya watu, na hatimaye kudumisha urafiki kati ya pande hizi mbili kupitia televisheni ambao utachangia katika ujenzi wa jumuiya iliyo karibu zaidi yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika.

Katika muongo mmoja uliopita yameshuhudiwa mabadiliko makubwa tangu ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya China na Afrika uanzishwe, Mkurugenzi Mkuu wa Umoja wa Mashirika ya Utangazaji (AUB) Afrika Grégoire NDJAKA amesema awali mwaka 2012 ilikuwa ni ndoto tu, lakini sasa kuna matokeo yanayoonekana dhahiri.

“Unapokwenda Afrika unaona filamu na habari za China kwenye skrini za Afrika. Halikadhalika unapokuja Beijing unaona habari nyingi za Afrika katika skrini za China. Kwa hiyo ushirikiano unasonga mbele. Pia waandishi wengi wa habari wamekuwa wakipatiwa mafunzo hapa China na hata Afrika. Kwa mfano katika AUB mwanzoni mwa mwaka huu, tulikuwa na mafunzo kuhusu namna ya kutumia Akili Bandia kuzalisha maudhui. Mafunzo hayo yalifanyika Banjul Gambia. Hata hivyo tunaona bado kuna maeneo mengine mengi ambayo ni lazima tuyaboreshe zaidi.”

Mada nyingine iliyotiliwa mkazo zaidi ni usimamizi wa Akili Bandia (AI) kwa kuzingatia msimamo wa pamoja wa nchi za Dunia ya Kusini na matumizi yake kwenye uundaji wa maudhui. Alhaji Mohamed Sarjoh Bah Mwakilishi wa Umoja wa Afrika (AU) nchini China, akizungumza wakati wa mkutano huo alisema, hivi sasa AU inaandaa mikakati ya usimamizi wa AI, ambapo Afrika itachambua kwa kina maslahi, wasiwasi na mahitaji yake halisi kuhusu usimamizi wa AI.

“Tunaona juhudi za China kama sehemu muhimu ya utetezi wake kwa nchi za Dunia ya Kusini katika sekta ya AI, Afrika iko tayari kushirikiana kwa karibu na China, ili kuhakikisha matakwa ya nchi za Dunia ya Kusini yanazingatiwa kikamilifu katika mifumo ya kimataifa ya usimamizi wa AI, na sauti za Dunia ya Kusini zinasikika kwa pamoja na kwa uwazi katika jamii ya kimataifa” .

Mkutano wa mwaka huu tunaweza kusema kwamba umefanyika kwa mafanikio makubwa kwani takriban wawakilishi 400 walihudhuria, wakiwemo maafisa kutoka idara za serikali zinazosimamia redio na televisheni za China na nchi 45 za Afrika, wawakilishi kutoka vyombo vya habari vya utangazaji na filamu, mashirika ya kimataifa, wajumbe wa kidiplomasia nchini China, makampuni husika, na jumuiya za washauri bingwa za vyuo vikuu.
 
Matunda yao tunayaona sasa wapo mpaka huku maporini "wanavuna dhahabu" za bwerere nimewakuta mpka kwenye ile migodi isiyo rasmi. Waafrika kama tuna laana fulani hivi
 
Back
Top Bottom