China na Russia kamwe hawawezi kutumia hiyo chanjo ya mRNA ya kampuni ya Pfizer (Billgate) na BioNTech (Mjerumani): Kwa nini Afrika tulazimishwe?

China na Russia kamwe hawawezi kutumia hiyo chanjo ya mRNA ya kampuni ya Pfizer (Billgate) na BioNTech (Mjerumani): Kwa nini Afrika tulazimishwe?

Sasa kwa nini tusinunue chanjo toka China? Kwanza ni rafiki zetu wa damu na juzi tu Waziri wao wa mambo ya nje alikuwa Chato. Wao kazi yao ni kutupiga ban kwenye nchi zao.

Bidhaa zetu nyingi zinatoka China. Kwa nini hii bidhaa ya mRNA tulazimishwe kuinunua kutoka kwa mabeberu hawa trna kwa bei yao kubwa mara 100 ukilinganisha na ile chanjo ya China? Halafu ya China ni original, haina RNA.
Hakuna nchi yoyote iliyolazimishwa kutumia chanjo moja, nchi nyingi zina mpaka chanjo tatu zinatumiwa leo tu nimesoma UAE wamepitisha chanjo nyingine ya India. na ziko nchi wanatumia za Russia. China chanjo yao imepitishwa nchi nyingi tu hata hapa tutaishia China na India.
 
Si mtengeneze yenu! China wanatengeneza yao na Russia pia wanatengeneza yao. Tanzania si mmetengeneza nyungu. Nyie pambaneni na nyungu yenu
 
Kwani mmekatazwa? Huwa nashangaa sana when the educated become so easily consumed by conspiracy theorists
Sijasema tumekatazwa bali kwa sasa hivi hatuna mpango huo.
 
Hata India wanayo ya kwao na wanawachanja watu wao! Irani ameagiza dozi kutoka China na Rwanda ameagiza kutok USA.... Sasa shida nini! Mleta mada ni kichaaa
Wewe ni mbumbumbu. Chanjo ya India ni ya Oxford/AstraZeneca waliotengeneza viwanda vyao huko wakitambua population ya India ni 1.3 billion people, hivyo soko ni kubwa. Rwanda hawawezi kuagiza chanjo ya USA kwani hawana uwezo wa kuitunza. Inahitaji majokofu ya minus 94 degrees F.
 
Hakuna ugonjwa mbaya kama hofu watu hivi sasa tumejazwa hofu kubwa, tena tunaambiwa hii covid ya sasa ni hatari kuliko ile ya kwanza, cha ajabu wao bado ligi na michezo inaendelea kule kwao. Hapa ndio utagundua kwa nini walitaka idadi ya wagonjwa iwe inatangazwa kila siku tena iwe inatajwa kila siku badala ya kurecord kimya kimya kama inavyofanyika kwa magonjwa mengine, tena idadi ya wagonjwa iwe inaongezeka badala ya kushuka, na pia utashanga kwa nini mke wa Bilgate alitabiri Africa tutakufa kama kuku na pia utajiuliza ni kwa nini Biligate amekuwa akizungumzia utishio wa covid utadhani yeye ni waziri wa afya.

Mimi napongeza msimamo wa Mh. Rais asikubali kufuata mkumbo, wananchi tunapaswa kuchukua tahadhari na kuendelea na shughuli zetu kama kawaida. Ni ajabu kuona nchi za Africa zimeshindwa kuthibiti vifo vinavyotokana na malaria, njaa, mafuriko, na ajali za barabarani ambavyo ndio vinagharimu maisha ya raia kwa wingi eti leo wanatumia njia za matajiri wa magharibi kudhibiti na kujikinga na covid.

Corona itakuja na mengi, binafsi naiona kama hii issue imekaa kibiashara zaidi, sikatai kwamba hakuna coron, corona ila kwa jinsi inavyopaishwa wengi warakufa na kwa hofu. Embu tujiulize, mbona mafua yamekuwa tishio kwa wazungu miaka nenda rudi mbona hakuna chanjo yake? Sisi wa Afrika tukiugua mafua ndani ya siku saba yanaisha yenyewe. Kumbe kuna uwezekano wazungu wangeamua kututia hofu kwenye mafua basi na sisi tungeanza kufa kwa hofu ya mafua then tungeambiwa tumekufa kwa mafua.

Ifike mahala viongozi wetu wajitambue, kwa mujibu wa maandiko mamlaka yeyote yametoka kwa Mungu, tuliona awamu ya kwanza Mh. Rais alikataa lockdown dunia ikamshanga lakini baadae karibu dunia nzima ilifuata njia zake lakini sijaona hao WHO wakimpa tuzo. Naamini na kwenye hii awamu ya pili ataibuka kidedea tena.
Sifa na kuabudu kama kawa
 
Wewe ni mbumbumbu. Chanjo ya India ni ya Oxford/AstraZeneca waliotengeneza viwanda vyao huko wakitambua population ya India ni 1.3 billion people, hivyo soko ni kubwa. Rwanda hawawezi kuagiza chanjo ya USA kwani hawana uwezo wa kuitunza. Inahitaji majokofu ya minus 94 degrees F.
Mpuuzi wa mwisho wewe, Niko Rwanda usibishe ujinga!
 
Umeongea Sana lakini la barakoa umeongea Kama mtoto wa shule ya vidudu (nursery). Nimeita shule ya vidudu makusudi.

Kama unaweza kuzuia maambukizi hata by 5% inatosha. Condom nyingi zinazuia up to 95% Kama utafuata procedure zote. Pamoja na mapungufu yake watu bado wanaambiwa wavae condom. Na tumeona matokeo.

Sasa we Naomi lakini unaponda uvaaji wa barakoa? Yaaani watu wake tu Kama wanyama pori wapeaani maambukizi hivyo hivyo pasipo na kinga yeyote? Wakati wakivaa barakoa wanaweza kupunguza hata kwa kiasi kidogo ulichosema hapo.

Siasa zisikuondolee elimu na uwezo wako wa kufikiri. Matamanio ya vyeo yasikufanye uwe kipofu wa kuona ukweli
Soma vizuri nilichoandika kuhusu masharti ya uvaaji barakoa na PPEs iliziweze kukukinga angalao kwa hiyo asilimia niliyoitaja. Usipotimiza hayo masharti hizo barakoa na PPEs zinageuka kuwa ni chanzo (reserveur) ya maambukizi na usambaaji wa hivi virusi. Unapaswa kuzibadili (dispose) kila baada ya saa moja. Maana yake ni shillingi zisizopungua elfu tatu kila saa. Nani mwenye uwezo wa kufanya hivyo hapa Tanzania? Halafu barakoa ukishaivaa haitakiwi kuwa unaikamata kamata na ndiyo maana watoto wadogo hawapaswi kuvyalishwa barakoa kwani zitawaambukiza corona badala ya kuwakinga. Halafu mijitu kama nyie utakuta limevaa barakoa lakini pua yake iko nje. Hii ni sawa na kuvaa chupi lakini nyeti zako ziko nje ya chupi! Unategemea hiyo chupi imesitiri kitu gani hapo kama nyeti zimeachwa nje?
 
Hiyo tunayoiita chanjo inayotengenezwa na kampuni ya Pfizer ikishirikiana na kampuni ya BioNTech ya ujerumani si sawa na chanjo zinazojulikana ambazo hutumia virusi vya ugonjwa huo huo vilivyopunguzwa makali (attenuated live viruses). Hawa wanatumia genetically engineered manufactured synthetics za genetitically coded mRNA to instruct our DNA in the genes of our cells (nucleas chromosomes) to produce certain proteins which are thought to be protective or curative of certain diseases including cancer diseases.

Utafiti wa kutumia synthetic mRNA kutibu au kukinga magonjwa ya cancer, rabies, zika etc ni wa siku nyingi. Hata hivyo dawa au chanjo za magonjwa hayo zinazotumia genetic mRNA hazikuweza kupata approval ya kutumika kwa binadamu kutoka FDA. Kwa sababu ya taharuki, hofu na wasiwasi wa janga hili la covid - 19 FDA imezipa emergency approval dawa/ chanjo hizo za mRNA. Hazijapitia hatua zote za kimchakato za usalama kama inavyotakiwa kisayansi. Inaelekea waafrika baada ya kujazwa hofu na pesa kupenyezwa walitumika kama guine pigs katika utafiti wa usalama na uwezo wa dawa hizi. Utafiti huo haukuoneshwa kwani ulikuwa unethical.

Chanjo za covid 19 zinazotengenezwa China na Urusi ndizo chanjo halisi zinazotumia live attenuated sars- cov-2, kirusi kinachosababisha covid-19. Urusi na Uchina kamwe haziwezi kutumia hizo chanjo za mRNA kutoka Pfizer/ BioNTech. Ni kipi cha ajabu Tanzania chini ya rais mwanasayansi wa level ya PhD kuzikataa au kuzitilia mashaka hizo chanjo zao za mRNA. Kama tutaamua kuchanja tutatumia chanjo toka China au Russia kwani hizo hazichezi na DNA zetu. Chanjo zinazotumia live attenuated viruses ni rahisi kuzi verify. Hizo za mRNA huwezi ukatambua code (ujumbe) zilizobebeshwa hizo RNA.

Halafu ukweli ni kuwa Afrika ugonjwa huu si tishio hata kidogo. Takwimu ambazo tumelazimishwa na WHO kwamba hata wale ambao hawana ugonjwa lakini wame test positive kwa baadhi ya antigens za cov-2 tuwahesabu kama ni wagonjwa (covid-19), ni kitu ambacho si sahihi na hakikubaliki kisayansi. Unachokonolewa pua kutafuta kama una hizo antigen wakati antigen hizi ungaliweza kuzipata kwenye kinyesi au kwa kuchokonolewa kwenye mkundu. China sasa hivi wanatumia kipimo cha kinyesi au rectal swab which is easier and more convinient. Halafu WHO inatulazimisha tupimane sana na vipimo hatupewi bure, ni za ghari takribani Tsh laki moja kila kipimo - wanatukopesha.

Takwimu wanazozitaka siyo za prevalence wala incidence ya ugonjwa au wa virusi hao wa cov-2 kiepidemolojia nakisayansi. Ndiyo maana Trump aliiondoa USA kwenye shirika hili la WHO kwa kuvurunda kwake kuhusu suala hili. Kama ni kutaka kujua prevalence ya virusi hivi ni vyema a scientific prevalance survey of an unbiased sample population ikafanyika. Si hizi takwimu za kujumlisha contact tracing, patients and carriers.Virusi hivi vimekuwapo duniani tangia zaidi ya miaka million 50 iliyopita. Binadamu amekuwapo hapa duniani kwa miaka million tano tu. Dunia imekuwapo kwa miaka billion tano (after the Big - Bang)!

Hata kwa hizo takwimu tulizolazimishwa kukusanya bado Afrika corona si tatizo la kutufanya tutaharuki. Kwa mfano Kenya ambayo population yake ni 55 million kwa kipindi cha mwaka mmoja ni watu elfu 90 tu ndiyo wame test kuwa na antigen za corona kwenye pua zao, yaani elfu nane tu kwa mwezi! Na wanaofikiriwa kufa kwa corona (kama primary cause of death) hawazidi elfu moja kwa mwaka. Na wengi wa hawa waliokufa walikuwa na magonjwa yao mengine kama kisukari, pressure, congestive cardiac failure, renal failure, cor pulmonary, bronchoathma (pumu) etc. Wala corona haikuwa the primary cause of death. Kwa sababu ya woga na taharuki iliyojengwa kuhusu corona wagonjwa wote hawa wenye changamoto la upumuaji (dypsnoea and tachpnoea) wamekuwa wakikimbiwa au kuogopwa na wauguzi/ madaktari na kupelekea wasipate huduma sahihi ya magonjwa yao na kusababisha vifo vyao. Tumeshuhudia hadi migomo ya wauuguzi, madaktari na watoa huduma za afya wengine.

Taharuki hii kwa nchi za Afrika ndiyo wazungu wanataka ili wapate watu wa kujaribia dawa au chanjo za ugonjwa huu na pia kupiga pesa. JPM kawagusa penyewe. Ndiyo maana hawakuchelewa kuwawaya - mara oh jiandae kupokea chanjo za msaada (lakini mkopo) za mRNA etc.

Inasikitisha sana Kanisa katoliki kupitia Padre wake machachari wa Baraza la Maaskofu Tanzania, anayeitwa Kitima, bila ushahidi wa kisayansi wala ridhaa ya malaka husika, ghafla kwa taharuki limeamua kuvunja utulivu wa nchi yetu uliokuwapo dhidi ya virusi hivi. Nchi ilikuwa imetulia chini ya ulinzi wa Mungu kwa kutambua kuwa ugonjwa huu hauna tiba wala kinga na kwamba kinachoua kwenye ugonjwa huu hasa ni ile hofu na taharuki na si ukali wa virusi hivi. Hizo barakola, social distancing na lockdown hazisaidii cho chote (useless) na hapa kwetu zina madhara zadi (dangerous) au haviwezekani. Wazungu wamefanya hivyo hazikusaidia chochote. Sweden hawakufanya hivyo kama sisi and are much better! Waafrika waliouawa kwa risasi kwa sababu ya kukiuka masharti ya lockdown ni wengi kuliko waliouawa na corona.

Hata hizo barakola za grade ya juu zinazouzwa Sh elfu kumi kwa moja ambazo zinapaswa kubadilishwa kila baada ya nusu sasa, bado uwezo wake wa kuzuia virusi hivi ni 60% tu. Hivi vya nguo vikibadilishwa kila nusu saa uwezo wake ni 20%. Ukikaa nayo muda murefu (zaidi ya saa)yenyewe ndiyo inakuwa source ya kukuambukiza. Hizo PPEs wanazotakiwa kuvaa watoa huduma wa afya bei yake ni sh laki tano, na zinatakiwa kubadilishwa kila saa moja (disposable).

Na bado udhibiti wake wa virusi hivi ni kama 80% tu! Haya mambo si rahisi scientifically. Isitoshe barakola nyingi zinazoingizwa nchini zinaelekea zilishapandikizwa virusi vya corona. Barakola hizi zinasaidia tu kupunguza hofu kwa wasiojua lakini ni more risk na hatari sana hasa zinapotumika visivyo. Kumuamini Mungu kunatoa hofu hii bila risk yo yote. Na hichi ndicho rais wetu alichokuwa amekifanya kuanzia mwezi April 2020. Vifo vya corona vilitoweka baada ya wananchi kuondokewa na hofu. Walimuamini Mungu, waliamini nyungu na dawa zingine za asili. Sasa kanisa katoliki limeturudisha tulikotoka - kwenye hofu na taharuki. Vyama vya upinzani na mabeberu wame take advantage. Tusikubali.

Social distancing kwa mazingira yetu ni next to impossible na lockdown ndiyo balaa zaidi.

Vita vya dunia ya sasa zinatumia silaha za kibiolojia za mRNA.


Acha kupotosha mkuu!hakuna nchi iliyolazimishwa kununua hizo chanjo za wazungu, mbona algeria wameagiza chanjo za kutoka china??wengine wameagiza kutoka RUSSIA!!Mambo mengine jamani wala hayahitaji propaganda, na mimi nakwambia hizo chanjo haziepukiki, hasa kwa wale wasafiri safiri!!bora hata mkulima kijiji!!
 
Mpuuzi wa mwisho wewe, Niko Rwanda usibishe ujinga!
Hata mimi niko Rwanda acha ujinga. Chanjo za covid zinazoletwa Africa kwa mpango wa WHO unaoitwa COVAX ni za kampuni ya AstraZeneca zilizotengenezwa kutokana na attenuated live chimpanzee adenovirus kwa utalaam wa Oxford University ya UK. Hizi zinatumia jokofu la kawaida kama chanjo zingine na zinaweza kutunzwa kwa miezi 6 kwenye hizo cold chain zetu za chanjo. Hizi ndizo wanatumia South Africa, India, Ulaya na kwingineko duniani ukiacha USA, China na Russia. Rwanda hamuna uwezo wa kuzitunza chanjo hizo za USA kwenye hizo -94 degrees F hadi kwa mchanjwaji huko vijijini. Achilia mbali hiyo cost ya USD 33 per dose ikilinganishwa na USD 4 per dose ya AstraZeneca. Achilia mbali uwezo wa wanasayansi wenu kutokuwa nayo ku verify hizo genetical instructions zilizobebwa na hao messenger RNA!

Mimi ni scientist mbobezi, ninajaribu kuwaelimisha kuhusu ugonjwa huu, wewe unaleta ujinga wako wakati hujui cho chote kuhusu sayansi hii. Jukwaa la Jf pia ni la kuelimisha jamii ya watanzania. Wewe wa Rwanda usitake kutuvuruga. Au kuna waliokutuma? Nyie huko endeleeni kuwekwa lockdown na kuchanjwa madawa msiyoyajua na kuvalishwa barakoa zilizobebeshwa corona na hao mabepari ili muweze kukopeshwa tu USD. Umeniudhi sana, ninamwomba rafiki wa taifa letu Mh. Paul Kagame anisamehe kwa kusema haya niliyoyasema. Na uwezekano ni mkubwa kuwa hili linalojiita Shift ni jitu la hapa hapa ufipa linalotafuta kick ya kisiasa kwenye kila jambo.
 
Kwani (kwa Mujibu wa Mleta mada) kuna tatizo Tanzania ikiamua kununua chanjo za Urusi au China!? Zenye teknolojia ambayo tunaweza kui-decode na kujua kilichomo!? Kuliko hizi mpya za Kimarekani!

BTW... Chanjo si ipo!? Unadol
kwamba urusi na china watakupa patent ya kufanya hiyo kitu ? vinalindwa na hati miliki.

Hizo za urusi na china zenyewe pia ni mpya.
hazikuwepo before.
 
Ni wakati sahihi kwa serikali yetu kuanzisha kitengo kikubwa cha biological warfare ndani ya JWTZ military intelligence unit.

Ni wakati sahihi wa kusomesha wataalamu wa hali ya juu wa microbiology, biotechnology, synthetic biology na vitu kama hivyo.
Huko tuendako sio kuzuri.

Tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye sayansi kwa ajili ya usalama wetu siku za usoni.

La mgambo hili!
kwanza kaka umechanganya mafile Jwtz military intelligence inafanya kazi nyingine kabisa.
hawahusiani na biological warfare
kuna kitengo maalumu kipo japo hakina makali.
 
Dr Uchwala:
China wameagiza 51 million doses za Ujerumani/Pfizer - (Fosun)
Westerners hawajaagiza hata dose moja iliyotengenezwa na China
Wachina wanagomea kuchanjwa vaccine yao wanataka imported kwa sababu yao haiko transparent
Brazil announces 50.4% efficacy of Chinese vaccine

Nyie mnakaa kupotosha tu!! Are you paid by Russian and Chinese? blood communist
brother uko attentive to details. na hizi ni latest details.
 
Msipende uongo. Hamna taifa linalolazimishwa kununua chanjo yeyote. Kila mtu anajua kuwa kwa Afrika hizo za Ujerumani na Marekani hazifai kutokana na mahitaji yake ya utunzaji.

Covax inakusudia kununua za Astra Zeneca na hasa zile zitakazo tengenezwa under license India ambazo zitakuwa za bei nafuu. Kama tuna uwezo wa kununua za kichina au kirusi, tununue na hamna atakae tuzuia.

Kama hatutaki kabisa chanjo, hivyo hivyo. Tena wengi watafurahi maana mahitaji ya chanjo ni makubwa kuliko supply. Hizo ambazo hamzitaki watanunua na kuwachanjia raia zao. Ila tusitegemee kuwa watatupa pesa yao ili tununue dawa za kupigia nyungu. Uamuzi ni wetu, tusiwasingizie wengine.

Amandla...

Ziagizwe za Iran, China, urusi na USA... Ziwekwe ktk maduka ya dawa ya hospital mgonjwa awe huru kuchagua, kulipia dawa na huduma zingine... Kwa hiyari Yao...
 
kwamba urusi na china watakupa patent ya kufanya hiyo kitu ? vinalindwa na hati miliki.

Hizo za urusi na china zenyewe pia ni mpya.
hazikuwepo before.
Uchina ndiyo magwiji wa coronaviruses. Pandemic ya kwanza ya cov -1 aka sars covid-1 ya mwaka 2012 ilianzia China. Na pandemic hii ya sars- cov-2 ilianzia China mwaka 2020. Chanjo dhidi ya covid-19 ya China imeanza kutumika Julai 2020 na wachina wameweza kuidhibiti corona kwa kiwango kikubwa. Hizi chanjo za USA na Ulaya zimeanza mwezi January 2021 kwa kelele kibao. Hawamfikii mchina katika fani hii ya coronaviruses. Mchina ndiyo mwalimu wao!
 
Magufuli kasema hataki chanjo zozote kutoka nje. Mpaka sasa kuna chanjo kutoka USA, UK, Germany, Russia, China, India nk. Sasa kuja hapa kuipigia debe chanjo ya China na Russia huku ukiziponda chanjo za USA na ulaya chini ya mwavuli wa kauli ya Magufuli, sisi tunakushangaa.
 
Kumbuka tu, China na Russia hawataki hata kutumia Facebook na Whatsapp, wana mitandao yao tofauti kabisa.

Kuwafuata hao watu inahitaji akili fulani za kiuwendawazimu.
 
Uchina ndiyo magwiji wa coronaviruses. Pandemic ya kwanza ya cov -1 aka sars covid-1 ya mwaka 2012 ilianzia China. Na pandemic hii ya sars- cov-2 ilianzia China mwaka 2020. Chanjo dhidi ya covid-19 ya China imeanza kutumika Julai 2020 na wachina wameweza kuidhibiti corona kwa kiwango kikubwa. Hizi chanjo za USA na Ulaya zimeanza mwezi January 2021 kwa kelele kibao. Hawamfikii mchina katika fani hii ya coronaviruses. Mchina ndiyo mwalimu wao!
kuna tofauti kubwa kati ya kuwa ground zero na kuwa na dawa.
mfano. ground zero ya ebola virus ni congo river. congo ni magwiji wa kutengeneza chanjo ya ebola nope?
sars outbreak ilitokea Nov 2002 to may 19 2004.
location: foshan,china.

sars cov-1 simply ilitoweka na waliweza kwa kuwela karantini na isolation mapema. so ugonjwa haukuvuka pande zingine za dunia.

kwanza sars cov-2 ilianza 2019 wuhan china.

unasema china ndio walikuwa wakwanza kutengeneza chanjooo ? nope

30 dec 2020 china ilitangaza jaribia la tatu limeonyesha 79% ya mafanikio.

in 13 jan 2021 brazil ilisitisha matumizi ya chanjo ya china baada ya kugundua kuwa ina 50% capability na si 79% kama china ilivyotangaza before.


so hao magwiji wa corona virus wanashindwaje kuwa na chanjo isiyo aminika?
why hawakutengeneza chanjo effective 100%?

kisa ugonjwa umeanzia kwako.. haimaanishi ww ndio gwiji la madawa.
 
Back
Top Bottom