DENG XIAOPING
JF-Expert Member
- Mar 6, 2022
- 2,396
- 2,598
Na mwaka huohuo 1927 vikaanza Vita vya wenyewe kwa wenyewe baina ya wachina wanaounga mkono chama cha kikomunisti cha China [ CPC ] na wachina wanaounga mkono chama cha Kuomitang . CPC ikiwa na jeshi la ukombozi wa watu wa China [ PLA ]likipambana na Kuomitang ikiwa na jeshi la China Nationalist Army Vita vikapiganwa kwa awamu ya kwanza mpaka 1937 na 1945 wakati wa Vita vya pili vya dunia wote kwa pamoja waliungana ili kupambana na kumtoa Japan ndani ya maeneo ya China baada ya kumshinda na kumtoa japan china wakati wa Vita vya pili vya dunia . Mnamo mwaka 1947 Vita vya wenyewe kwa wenyewe vikarudi tena na hii ikiwa ni awamu ya pili ya Vita kwa nguvu na kwa umoja jeshi la watu wa China [ PLA ] chini ya wanachama wa CPC na wachina wanaounga mkono sera za kijamaa lilipigana mpaka mwaka 1949 na kuwashinda jeshi la China Nationalist Army chini ya Kuomitang na waka kimbilia Kisiwani na ndipo ikazaliwa Jamhuri ya watu wa China [ PEOPLE'S REPUBLIC OF CHINA ] chini ya chama cha kikomunisti cha China [ CPC ] chini ya mwenyekiti Mao Zedong na Rais wa Jamhuri ya watu wa China.Republic Of China [ ROC ] chini ya chama cha kibepari cha Kuomitang chini ya Sun Yat Sen na baadae Chiang Kai sheki ilikuwa imeoza inanuka rushwa, sera mbovu za umiliki wa ardhi, ufisadi, Uongozi mbovu ndipo Mao Zedong akachukizwa na hiyo hali akaanza kujifunza falsafa za kijamaa kupitia vitabu na magazeti yaliyokuwa yanaandika habari kuhusu nchi ya kijamaa ya Urusi chini ya Lenin ndipo Mao akajikusanya na wenzake Kumi akiwemo Zhuo Enlai na kuanzisha Chama cha kijamaa kwenye boti 1921 ili kuja kuleta ukombozi wa hayo matatizo yanayo sababishwa na chama Cha kibepari cha Kuomitang hasa hasa tatizo la umiliki wa ardhi kwa wakulima . Mao alitembea vijiji kwa vijiji kwa miguu kuwaeleza wachina dhima nzima ya kijamaa ambavyo itaweza kuwasaidia kukomesha matatizo yao chini ya serikali dhalimu ya kibepari ya Kuomitang.wachina waliowengi wakaanza kuamini falasa za kijamaa za Mao[ Maoism] na kuanza kujiunga na chama Cha kikomunisti Cha China [ CPC ] kwa ajili ya kupinga serikali ya Kuomitang . Wachina waliowengi wengi na kwa wingi waliongezeka katika kujiunga na CPC na kuunga juhudi za mapambano huku China ikiwa imepasuka vipande viwili vya kifalsafa ujamaa wale waliokuwa wanaunga juhudi za CPC na wanachama wa CPC na kipande kingine wale waliokuwa wanaunga mkono sera za kibepari za Kuomitang . Mnamo mwaka 1927 wanachama wa CPC wakaanzisha jeshi lao kwa ajili ya ukombozi waliolipachika jina la People's Liberation Army [ PLA ] kwa ajili ya kuitoa madarakani Kuomitang .