China(PRC) na Taiwan(ROC) bado wapo kwenye civil war

China(PRC) na Taiwan(ROC) bado wapo kwenye civil war

Hao wote uliowataja mkuu ni wavamizi wa maeneo ya China wauighurs ni wavamizi wa kituruki, watibet waliowengi ni wavamizi kutoka mongolia
Waturuki wote asili yao ni Asia ya kati. Ambako ndiko huko Xinjiang na nchi zingine za Asia ya kati. Hao ni watu wa Asili hapo. Watibet ndiyo kabisa. Ni watu wa Asili hapo. Unataka kusema maeneo ya Waighur, watibet na Taiwan ni maeneo ya asili wa wa-Han?
 
Apa nitarudi asee maana si kwa povu hili
 
Ndugu usichukulie China Kama maeneo ya Afrika yaliyogawanywa Mjini Berlin China hipo mda Sana na hapa duniani na ramani ya Ancient China ipo na ndio hii wanayotumia Sasa hivi kudai maeneo yao. China inahistoria ya miaka 5000 jiulize taifa lako Tanganyika Lina miaka mingapi la uwepo wake hapa duniani?🤔😀
Mjaaa wa Kisasa: Hivi kweli unataka tutumie Ancient History leo? Hitler alipoanza kurudi kwenye Ancient History ndio akaja na theory ya Master Race nadhani unajua kilichofuata! Wachina wakianza kutatua matatizo yao le kwa kurudi enzi za Qin dynast au Han dynasty kaa ulewe Taiwan itakuwa ni mwanzo tu! Watapigana na nchi nyingi sana.

Labda nikuulize nini kiliwashinda kuichukua Taiwan baada kuichukua China Mainland wakati huo...kazi iliyowashinda wakati ule sidhani wataiweza leo, kwa sasa tusubiri tuone, maana bado wameizunguka Taiwan wanarusha mizinga baharini sijui watamaliza lini.....
 
Uko sahihi, hili suala China na Taiwan ni tata sana kutokana na historia yake.
Aleyn: China na Taiwan ni nchi moja, lakini kisiasa walichukua nji tofauti, upande wa utawala wa zamani, yaani wa Chang Kai Shek,waliamua kumpisha Mao mainland China na kwenda Taiwan. Ungekua labda ulifanyika uchaguzi na kundi moja likashinda angalau upande ulioshinda ninge sympathize nao, Mao aliingia kwa nguvu,Wachina hawakushirikishwa kuwa wanataka Ukomunisti, ambao hawautaki wakaenda Taiwan,sasa nani mwenye haki dhidi ya mwenzie.Na hata ukifanya referendum leo,watu wa Mainland China wataitaka Taiwan, na watu wa Taiwan hawataitaka Mainland China.Ndio maana kwa upande claims za China zinaweza kuwa pia za Taiwan.
 
Hilo halikubaliki, hakuna Wataiwan wataukubali huo ujinga kirahisi.
China wanachotaka ni peacefully Unification na Taiwan kwa kuwa wao PRC ndio walioshinda Vita hivyo ardhi yote ya China wao ndio wenye mamlaka nayo . China hawataki kuwaua wala kuwafukuza ndugu zake kule kisiwani Ila China wanataka Kisiwa chao cha Taiwan kurudi katika himaya yao China Beijing huku wakiendelea kuwaacha Taiwan katika mfumo wao wa kiutawala Kama ilivyo Macau na Hongkong.
 
Siku China ikiwa ya kidemokrasia na utawala wa CCP kufika mwisho wake labda Wataiwan watakubali kujiunga nao.
Mkuu China inahistoria ya miaka 5000 hapa duniani ile ni ardhi yao kwa hiyo lazima wahakikishe wanaitunza na wanailinda ndio maana Tibet ilirudi, Macau ilirudi, Hongkong ilirudi bado tu Taiwan irudi kwenye himaya ya mababu zao pale ambapo ipo forbidden City Beijing mamlaka ya China yote yanatokea Beijing ilipo Forbidden city makao makuu ya Han Dynasty.
 
Sasa kila mtu akisema aanze kudai ardhi ya mababu zake toka ancient times katika hii dunia kwa sasa si dunia nzima patageuka uwanja wa fujo na vurugu tupu!
Mkuu ile ardhi ya mababu zao ileyopo kwenye ramani zao kabisa since ancient time china Ni taifa kongwe hapa Duniani sio rahisi wao kuruhusu ardhi ya mababu zao iondoke bila sababu za msingi . Kama unazungumzia sovereignty states hata Macau ilikuwa chini ya ureno na ureno alikuwa na uwezo wa kuipatia Uhuru Macau na kuwa nchi Ila china ilipigania macau mpaka ikarudi nyumbani hivyo hivyo kwa Hong Kong Napo ilikuwa kabisa inaweza kuwa nchi huru Ila china ilipinga Hilo mpaka ikarudi nyumbani kwa sababu ile Ni ardhi ya mabibi na mababu zao inayotambulika kabisa katika ramani zao hata za kale hivyo hivyo kwa Tibet nayo Taiwan ile Ni ardhi yao China inq kila sababu kutetea ardhi ya mababu zao isipotee iwe kwa amani au hata kwa Vita lazima watete ardhi yao . Hata ingekuwa sisi Tanzania tungefanya hivyo hivyo anavyofanya China [ PRC ] kuruhusu Taiwan kuwa huru na kuondoka na kupotea mikononi mwa Beijing ni kuwakosea heshima wafalme wote wa China waliofariki. Ile ni ardhi yao na wao pekee wachina ndio wenye mamlaka juu ya Taiwan na wala sio mtu mwingine.
 
Unaamini haya pia kwa dikteta Putin na Russia yake??
Shida ya Hawa mainland China Ni ule ukoloni wa chama kikuu Cha China na umungu mtu wake wa kulazimisha kila kitu. Kwanza hawaamini kwenye Uhuru wa kuabudu na tamaduni tofauti kwa raia wake.
 
Huo ndio mtizamo wa Dikteta Putin kule Ukraine pia.
Mtazamo wa kiimla Sana huu. Hawa Taiwan wamekuwa Taifa kwa miongo zaidi ya 7 (miaka 70) hiyo. Hapo kuna vizazi vimepitia falsafa na Sera mbalimbali. Simple tu, wafanye referendum na wananchi wenyewe wa Taiwan waamue, Kama Wanataka kuwa sehemu ya China au Taiwan yao yenye mamlaka kamili na utambulisho kimataifa iendelee.
 
Siku China ikiwa ya kidemokrasia na utawala wa CCP kufika mwisho wake labda Wataiwan watakubali kujiunga nao.
Kwani sababu ya Kuomitang kukimbilia Kisiwan [ Taiwan ] ili kuwa kwenda kuiishi kwenye demokrasia?🤔
 
Mjaaa wa Kisasa: Hivi kweli unataka tutumie Ancient History leo? Hitler alipoanza kurudi kwenye Ancient History ndio akaja na theory ya Master Race nadhani unajua kilichofuata! Wachina wakianza kutatua matatizo yao le kwa kurudi enzi za Qin dynast au Han dynasty kaa ulewe Taiwan itakuwa ni mwanzo tu! Watapigana na nchi nyingi sana.

Labda nikuulize nini kiliwashinda kuichukua Taiwan baada kuichukua China Mainland wakati huo...kazi iliyowashinda wakati ule sidhani wataiweza leo, kwa sasa tusubiri tuone, maana bado wameizunguka Taiwan wanarusha mizinga baharini sijui watamaliza lini.....
Sawa tusubiri tuone nini kitakacho jili baada ya mazoezi ya PLA kukamilika.
 
Sasa kila mtu akisema aanze kudai ardhi ya mababu zake toka ancient times katika hii dunia kwa sasa si dunia nzima patageuka uwanja wa fujo na vurugu tupu!
Kama ramani mnayo hakuna anaye wazuia kudai kilicho chenu.

NB: Ila Afrika hamna Cha kudai maana mligawanywa pale mjini Berlin kabla ya kuja kuwatawala😄.
 
Angalia uchaguzi wao kama wagombea walio Pro union wanashinda kwa kiasi gani
Umesema hakuna Wataiwan watakao kubali Peacefully Unification🤔.
Ila kumbe Kuna kiwango cha Wataiwan kinachounga mkono peacefully Unification.
 
Sijawelewa point yako kuhusu ramani. Ujerumani wanayo Ramani ya Prussia iliyokuwa inajumuisha Poland,Lithunia,Czech,sehemu za Russia.

Mongolia wanayo ramani ya Mongol empire ya Genghis ambayo ilikuwa inajumuisha sehemu kubwa ya China na Russia.

Waturuki wanayo ramani ya Ottoman Empire ambayo ilikuwa inajumuisha hadi sehemu za North Africa.

Waitalia wanayo ramani ya Roman Empire
Saudi Arabia wanayo ramani ya Umayyad Caliphate

Zimbabwe wanayo ramani ya Ufalme wa Mwenemutapa ambayo ilikuwa inajumuisha hadi Msumbiji, Zambia na Malawi.

Sasa hawa wote kila mtu akianza kudai "ardhi ya mababu zake" si itakuwa vurugu ya kuimaliza dunia ??!
Kama ramani mnayo hakuna anaye wazuia kudai kilicho chenu.

NB: Ila Afrika hamna Cha kudai maana mligawanywa pale mjini Berlin kabla ya kuja kuwatawala[emoji1].
 
Back
Top Bottom