China(PRC) na Taiwan(ROC) bado wapo kwenye civil war

Na mwaka huohuo 1927 vikaanza Vita vya wenyewe kwa wenyewe baina ya wachina wanaounga mkono chama cha kikomunisti cha China [ CPC ] na wachina wanaounga mkono chama cha Kuomitang . CPC ikiwa na jeshi la ukombozi wa watu wa China [ PLA ]likipambana na Kuomitang ikiwa na jeshi la China Nationalist Army Vita vikapiganwa kwa awamu ya kwanza mpaka 1937 na 1945 wakati wa Vita vya pili vya dunia wote kwa pamoja waliungana ili kupambana na kumtoa Japan ndani ya maeneo ya China baada ya kumshinda na kumtoa japan china wakati wa Vita vya pili vya dunia . Mnamo mwaka 1947 Vita vya wenyewe kwa wenyewe vikarudi tena na hii ikiwa ni awamu ya pili ya Vita kwa nguvu na kwa umoja jeshi la watu wa China [ PLA ] chini ya wanachama wa CPC na wachina wanaounga mkono sera za kijamaa lilipigana mpaka mwaka 1949 na kuwashinda jeshi la China Nationalist Army chini ya Kuomitang na waka kimbilia Kisiwani na ndipo ikazaliwa Jamhuri ya watu wa China [ PEOPLE'S REPUBLIC OF CHINA ] chini ya chama cha kikomunisti cha China [ CPC ] chini ya mwenyekiti Mao Zedong na Rais wa Jamhuri ya watu wa China.
 
Nakubaliana na wewe, waliokimbia kwa sasa, yaani Taiwan hawadai chochote cha Mainland China,sasa kwa nini China itake kutawala mstakabali wao? Umeshinda umechukua sehemu kubwa, sasa kwa unifuate na kutaka kuchukua changu? Kwangu mimi is not fair.
 
China wanachotaka ni peacefully Unification na Taiwan kwa kuwa wao PRC ndio walioshinda Vita hivyo ardhi yote ya China wao ndio wenye mamlaka nayo . China hawataki kuwaua wala kuwafukuza ndugu zake kule kisiwani Ila China wanataka Kisiwa chao cha Taiwan kurudi katika himaya yao China Beijing huku wakiendelea kuwaacha Taiwan katika mfumo wao wa kiutawala Kama ilivyo Macau na Hongkong.
 
Pia unapaswa ufahamu hata Taiwan [ ROC ] nao pia wanaitaka China mainland ndio maana wao kisiwa wanajiita Taiwan na mainland wanaiita west taiwan😀 kwa hiyo wanaamini pia ile ni ardhi yao nao pia wanaitaka ili kurudisha REPUBLIC OF CHINA mpaka Mainland.
 
Sikujua kama ni policy ya Taiwan...
 
Mkuu me nainawanachelwa tu wachapane ili wajue nani mbabe
 
Kesi Hongkong naona tofauti, China wanataka hovyo, lakini kushinda vita hakuwapi haki! Ni nguvu ndio iliyotumika.Wachina wanataka hivyo, what is wrong na Wataiwan wakitaka wanavyotaka! Sioni egitimacy ya madai ya China kwa Taiwan, kama ambavyo sitaona madai ya Taiwan kwa Mainland China pia, walichukua path tofauti,kila kundi kina uhuru wa kuamua path yake. Kwangu mimi naona China naye anaamua kuwa beberu.
 
Jambo la kwanza tunapaswa kufahamu kuwa China[ PRC ] ndio mshindi wa Vita na ndio mwakilishi wa China UN kwa hiyo ana mamlaka yote ya kudai na kulinda ardhi yake hata angekuwa China [ ROC ] mshindi wa Vita naye angekuwa na mamlaka hayo. Pia tunapaswa kufahamu kuwa kisiwa cha china [ Taiwan ] kilikuwa chini ya koloni la Japan licha ya kuwa Japan alishindwa Vita lakini alikiacha huru Ila hakukirudisha chini ya himaya ya China mainland kwa hiyo China mainland pia inamamlaka ya kurudisha kisiwa chake chini ya himaya yake.
 
Hivi unaona UN ilikuwa right? Mara ngapi UN imetoa maamuzi sio sahihi! Uamuzi sahihi ulikuwa zote ziingizwe UN kama mataifa tofauti.Taiwan haikuwa right kuiwakilisha China nzima.Ukiikubalia China lazima uje na sera ya mwenye nguvu mpishe!.Nashangaa kwa nini husemi Taiwan ina mamlaka ya kuirudisha China kwenye mamlaka yake!
 
Nmekusoma mkuu
 
Mja
Na wewe umeingizwa kwenye propaganda za peacefully Unification! Haya mabomu na mameli ya Kavita yayoizunguka Taiwan leo ndio kutaka "Peacefully Unification " Please Ndugu ya Mjamaa wa kisasa kubali China ana elements zote za Imperialistic nation, na hapo bado hajawa sole super power
 
Nmekusoma mkuu
Mkuu, Taiwan na China waliisha chukua njia tofauti, kuna kipindi mwanzoni Mainland China ilipokuwa shaghala bagala wakati wanajenga ujamaa, Taiwan ilikuwa juu na mjanja mpaka ikapewa kiti UN kuwakilisha China nzima,kwangu mimi hiyo pia haikuwa sawa, wao hawakuwa na legitimacy ya kuiwakilisha China mainland.
Kwa kutaka kurebisha kosa hilo,UN ikafanya kosa tena, ikamwondoa Taiwan na kuiingiza China, kwa nini wasiwaingize kama mataifa mawili tofauti! Ukiwauliza UN leo je China wana haki ya kuichukua Taiwan,hawana jibu! Kama Palestine ina uwakilishi UN why Taiwan.
China inaidanganya dunia na "Peacefully Unification " angalia ilivyokuja juu Pelosi aliposema anaenda Taiwan. Hili jambo ni kitendwawili cha kihistoria, ndio, na China inataka kutumia nguvu tu, na itaweza siku Marekani ikianguka chali, na dunia tutakua tumepata beberu mwingine.
 
Nakubaliana na wewe, waliokimbia kwa sasa, yaani Taiwan hawadai chochote cha Mainland China,sasa kwa nini China itake kutawala mstakabali wao? Umeshinda umechukua sehemu kubwa, sasa kwa unifuate na kutaka kuchukua changu? Kwangu mimi is not fair.
Nasoma posts zako kwa makini na ninakuelewa sana yaani.
 
Huu ni ujinga anaofanya China, utake unification ya nini wakati ulishampiga na yeye akaamua kukimbilia mbali na wewe? Mtu ameenda mbali kwa ajili ya kujisalimisha, sasa unamfatilia wa nini, si umuache na maisha yake? Kwa kweli kwa hili Taiwan yupo sahihi kabisa.
 
Ndo zichapwe sasa, mshindi abebe ardhi.
 
Wachina hawajawahi kumshinda mjapan chief wamshukuru Mmarekan na nyuklia yake mpaka leo wangekuwa wamekaliwa.
 
Wachina hawajawahi kumshinda mjapan chief wamshukuru Mmarekan na nyuklia yake mpaka leo wangekuwa wamekaliwa.
Kitali: Kama Mmarekani asingemtwanga na Atomic mjapani au Mjapani asingeanzisha Vita na Mmarekani, labda China ingepata uhuru wake miaka ya 60! Japan was more advanced nation miaka ya 1930 na China ilikuwa primitive kwa maana ya primitive licha ya historia yao ndefu.
Huwezi kuamini Japan iliitawala China na kuinyanyasa vibaya, Kuingia kwa Mmarekani kuliikata nguvu ya Japan ndio kina Mao wakapata nguvu.Damu nyingi mno ilimwagika China kujitoa mikononi mwa Japan...
 
Jambo la msingi hapa tunapaswa kushauriana ni kuwa maamuzi ya UN yangepaswa kuwa ni :-
i, Kuvunja serikali ya Hongkong
ii, Kuvunja serikali ya Macau
iii, Kuvunja serikali ya Taiwan
Na wote hawa kwa pamoja wangeungana na China PRC kuzaa China moja isiyokuwa na serikali nyingi kitu ambacho hata serikali ya Beijing imekuwa ikipendekeza na kupigia kelele jambo hili .
 
Uko sahihi sana mkuu👍.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…