China(PRC) na Taiwan(ROC) bado wapo kwenye civil war

Hao wote uliowataja mkuu ni wavamizi wa maeneo ya China wauighurs ni wavamizi wa kituruki, watibet waliowengi ni wavamizi kutoka mongolia
Waturuki wote asili yao ni Asia ya kati. Ambako ndiko huko Xinjiang na nchi zingine za Asia ya kati. Hao ni watu wa Asili hapo. Watibet ndiyo kabisa. Ni watu wa Asili hapo. Unataka kusema maeneo ya Waighur, watibet na Taiwan ni maeneo ya asili wa wa-Han?
 
Apa nitarudi asee maana si kwa povu hili
 
Mjaaa wa Kisasa: Hivi kweli unataka tutumie Ancient History leo? Hitler alipoanza kurudi kwenye Ancient History ndio akaja na theory ya Master Race nadhani unajua kilichofuata! Wachina wakianza kutatua matatizo yao le kwa kurudi enzi za Qin dynast au Han dynasty kaa ulewe Taiwan itakuwa ni mwanzo tu! Watapigana na nchi nyingi sana.

Labda nikuulize nini kiliwashinda kuichukua Taiwan baada kuichukua China Mainland wakati huo...kazi iliyowashinda wakati ule sidhani wataiweza leo, kwa sasa tusubiri tuone, maana bado wameizunguka Taiwan wanarusha mizinga baharini sijui watamaliza lini.....
 
Patachimbika ipo siku kuna moshi mweusi unafukuta hapo
 
Uko sahihi, hili suala China na Taiwan ni tata sana kutokana na historia yake.
 
Hilo halikubaliki, hakuna Wataiwan wataukubali huo ujinga kirahisi.
 
Siku China ikiwa ya kidemokrasia na utawala wa CCP kufika mwisho wake labda Wataiwan watakubali kujiunga nao.
 
Sasa kila mtu akisema aanze kudai ardhi ya mababu zake toka ancient times katika hii dunia kwa sasa si dunia nzima patageuka uwanja wa fujo na vurugu tupu!
 
Unaamini haya pia kwa dikteta Putin na Russia yake??
Shida ya Hawa mainland China Ni ule ukoloni wa chama kikuu Cha China na umungu mtu wake wa kulazimisha kila kitu. Kwanza hawaamini kwenye Uhuru wa kuabudu na tamaduni tofauti kwa raia wake.
 
Huo ndio mtizamo wa Dikteta Putin kule Ukraine pia.
 
Siku China ikiwa ya kidemokrasia na utawala wa CCP kufika mwisho wake labda Wataiwan watakubali kujiunga nao.
Kwani sababu ya Kuomitang kukimbilia Kisiwan [ Taiwan ] ili kuwa kwenda kuiishi kwenye demokrasia?🤔
 
Sawa tusubiri tuone nini kitakacho jili baada ya mazoezi ya PLA kukamilika.
 
Sasa kila mtu akisema aanze kudai ardhi ya mababu zake toka ancient times katika hii dunia kwa sasa si dunia nzima patageuka uwanja wa fujo na vurugu tupu!
Kama ramani mnayo hakuna anaye wazuia kudai kilicho chenu.

NB: Ila Afrika hamna Cha kudai maana mligawanywa pale mjini Berlin kabla ya kuja kuwatawala😄.
 
Angalia uchaguzi wao kama wagombea walio Pro union wanashinda kwa kiasi gani
Umesema hakuna Wataiwan watakao kubali Peacefully Unification🤔.
Ila kumbe Kuna kiwango cha Wataiwan kinachounga mkono peacefully Unification.
 
Sijawelewa point yako kuhusu ramani. Ujerumani wanayo Ramani ya Prussia iliyokuwa inajumuisha Poland,Lithunia,Czech,sehemu za Russia.

Mongolia wanayo ramani ya Mongol empire ya Genghis ambayo ilikuwa inajumuisha sehemu kubwa ya China na Russia.

Waturuki wanayo ramani ya Ottoman Empire ambayo ilikuwa inajumuisha hadi sehemu za North Africa.

Waitalia wanayo ramani ya Roman Empire
Saudi Arabia wanayo ramani ya Umayyad Caliphate

Zimbabwe wanayo ramani ya Ufalme wa Mwenemutapa ambayo ilikuwa inajumuisha hadi Msumbiji, Zambia na Malawi.

Sasa hawa wote kila mtu akianza kudai "ardhi ya mababu zake" si itakuwa vurugu ya kuimaliza dunia ??!
Kama ramani mnayo hakuna anaye wazuia kudai kilicho chenu.

NB: Ila Afrika hamna Cha kudai maana mligawanywa pale mjini Berlin kabla ya kuja kuwatawala[emoji1].
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…