China yaingia rasmi soko la memory chip (DDR5) na gaming GPU. Samsung, SKhynix, Nvidia, Micron na AMD tumbo joto

China yaingia rasmi soko la memory chip (DDR5) na gaming GPU. Samsung, SKhynix, Nvidia, Micron na AMD tumbo joto

Hivi karibuni China imeandika historia mpya ya teknolojia duniani.

Kwa miaka mingi Marekani, South Korea na Taiwan zilikuwa The Big 3 Cartel walitawala GPU na memory chips. Wakiamua supply, wakipandisha bei, na dunia nzima ikalazimika kufuata.

Sasa China imevunja ukuta huo. Enzi ya kutegemea kampuni chache duniani inaanza kufika mwisho.

China imelazimisha dunia ya semiconductor kuingia era mpya
.​
Akina nvidia, amd na micron hawawez pata tumbo joto, hawategemei mauzo ya memory chip wako kwa leveo waliyopo sasa ni beyond that

Hapo wa kupata pressha ni samsung na baadhi ya kampuni ambazo ndio muuzaj mkubwa wa hiyo kitu.
 
Gaming GPU ni kifupi cha Graphics Processing Unit
Inatengenezwa mahsusi kwa michezo ya video (gaming). Bila GPU yenye nguvu, game nzito haziwezi kwenda smoothly. Hii ndiyo chip inayochora:​
  • graphics,​
  • shadows,​
  • reflections,​
  • textures,​
  • animations,​
  • FPS kwenye game.​
  • Pia hutumika kwenye AI na data centres​

Kampuni zilizokuwa zinaongoza kwenye gaming GPU kwa miaka mingi ni za Marekani Nvidia na AMD

China wanaanza kuingia kwenye hii market kupitia kampuni kama Moore Threads, Biren Technology na Innosilicon.

China kuingia kwenye memory market na GPU kunaongeza ushindani, kushusha bei na kuvunja dominance ya kampuni za zamani.
​
Huenda machine za GPU zikapoa beiz hasa tunao train model za AI tuanze fanyia hata kwenye local, badala ya kulipia hela kwenye resource za watu ambao siku vichaa vikiwapenda umeisha ila pia hakuna privacy ukisha train kwenye miundombinu ya watu
 
Akina nvidia, amd na micron hawawez pata tumbo joto, hawategemei mauzo ya memory chip wako kwa leveo waliyopo sasa ni beyond that

Hapo wa kupata pressha ni samsung na baadhi ya kampuni ambazo ndio muuzaj mkubwa wa hiyo kitu.
Yani mtu upo vigwaza, huna hata kibanda cha matunda lakn unachambua biashara za wachina eti zitakosa soko
 
Tatizo kubwa la Wachina ni ubora wa vitu vyao.

Mfano, wanatengeneza simu, computer, na vifaa vingi vya electronics, lakini ubora wake ni tia maji. Tecno zao kwa mfano ni duni kwa Samsung, iPhone, nk
20260524_065949.jpg
 
Kwa apps nzito nzito bora mchina amekuja especially ukiwa unafanya 3d rendering ukiwa unatumia reality capture kama kamashine kako ni core i 5 unakaskia kanavovuma
Wachache watakuelewa na ndio maana comment yako wengi wameiruka bila kuchangia

Hii kitu aliyofanya Mchina italeta unafuu sana hasa kwa wale wanaocheza na kubadilisha mfano wa kitu cha 3D kuwa picha au video inayoweza kuonekana kama halisi

Kuna jamaa yangu architect anasema sasa upele umemfika mkunaji
 
Kama kucopy ni rahisi hivyo kwa nini Tanzania mnashindwa wapi ku-copu and paste?
Watawala waliojikita kwenye ufisadi, wizi wa rasilimali za nchi, utekaji, mauaji, migogoro na uhasama dhidi ya wananchi wao hawawezi kumudu mambo ya maana ya maendeleo
 
Ukianza kufuatilia comments za CEOs wengi wa kampuni kubwa za Marekani na Ulaya wanaiadmire sana China

Kwa sababu za kibiashara wanavutiwa na soko la China linawapa urahisi kwenye uwekezaji kwa sababu ya uwepo wa teknolojia, techincal knowhow, supply chain, R&D centres, kasi ya utekelezaji wa miradi, skilled personnel, unafuu wa nishati na upatikanaji wake, logistics, IoT n.k

Ni washamba wachache tu kwenye mitandao wana mtazamo hasi kuhusu China na kwa sababu hawaijui kiundani
 
Watawala waliojikita kwenye ufisadi, wizi wa rasilimali za nchi, utekaji, mauaji, migogoro na uhasama dhidi ya wananchi wao hawawezi kumudu mambo ya maana ya maendeleo
Umesema vyema nchi nyingi zinazoendelea duniani zinahitaji kujifunza kutoka China

Kwanza lazima wawe na uongozi thabiti kama Mao na wenye maono kama wa Deng Xiaoping. Kufungua uchumi kama Jiang Zemin kusawazisha maendeleo kama Hu Jinto. Na kuimarisha nguvu ya kiteknolojia na kimataifa kama Xi Jinping

Mipango ya muda mrefu (long term planning)
China huweka malengo ya miaka 10 hadi30. Hii inasaidia miradi isiishie katikati kama mara nyingi hutokea kwenye nchi nyingi zinazoendelea

Uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu
China imewekeza sana kwenye reli za kisasa (high-speed rail), barabara na bandari, umeme na nishati. Miundombinu imara huongeza kasi ya uchumi

Industrial policy (kujenga viwanda kwa makusudi)
Serikali ya China inasaidia na kulinda viwanda vya ndani hadi viwe imara. Hii imesaidia China kuwa manufacturing hub ya dunia

Maeneo maalum ya kiuchumi (Special Economic Zones)
China ilianzisha maeneo maalumu ya uwekezaji yenye sheria rafiki kwa uwekezaji, kodi nafuu, majaribio ya soko huria. Haya yalivutia uwekezaji mkubwa wa kigeni

Elimu na ujuzi wa teknolojia
China imewekeza sana kwenye STEM (science, technology, engineering, math) vyuo vikuu vya utafiti, mafunzo ya wahandisi wengi. Matokeo yake ni nguvu kubwa ya innovation
 
Wachache watakuelewa na ndio maana comment yako wengi wameiruka bila kuchangia

Hii kitu aliyofanya Mchina italeta unafuu sana hasa kwa wale wanaocheza na kubadilisha mfano wa kitu cha 3D kuwa picha au video inayoweza kuonekana kama halisi

Kuna jamaa yangu architect anasema sasa upele umemfika mkunaji
Ni kweli. Kwa mim nilitumia reality capture kutengeneza 3d image. Sasa ile prog una upload jpeg si chini ya 20000ukitaka ile hologram iwe real 3d bila kupoteza ile reality yake sasa mchina alete mashine mapafu ya mbwa zpge mzigo chips hizo
 
Akina nvidia, amd na micron hawawez pata tumbo joto, hawategemei mauzo ya memory chip wako kwa leveo waliyopo sasa ni beyond that

Hapo wa kupata pressha ni samsung na baadhi ya kampuni ambazo ndio muuzaj mkubwa wa hiyo kitu.
Sikuzote China inapoanza production ya bidhaa huwa inachukuliwa poa lakini kadiri siku zinavyosonga mass production ya hiyo bidhaa inazidi kuteka soko, mifano ni mingi EVs, EV batteries, rare earth, solar, ship building n.k
 
Huenda machine za GPU zikapoa beiz hasa tunao train model za AI tuanze fanyia hata kwenye local, badala ya kulipia hela kwenye resource za watu ambao siku vichaa vikiwapenda umeisha ila pia hakuna privacy ukisha train kwenye miundombinu ya watu
Kweli kabisa, kadri GPU zinavyozidi kushuka bei na kuwa powerful, local AI training/inference itakuwa option bora zaidi

Privacy ipo mikononi mwako, hakuna vendor lock-in, na cost za muda mrefu zinapungua sana
 
Inatoa hata motisha hata kwa watafiti wa medium class kuwekeza, kwenye AI bei zikiwa zimepoa. Sasa hivi kuwa server za AI hata la chini kabisa ni kisanga kizito, kwa mtu wa kawaida hawezi afford tunajikuta tunajazana huko pa kulipia dollar bukuu kadhaa kwa mwezi na inategemea unafanya nini na bado unakuta project haikulipi 😁

Mchina ashukuliwe anakuja fanya balance duniani labda watu washindwe wenyewe
 
Back
Top Bottom