SNAP J
JF-Expert Member
- Dec 26, 2013
- 7,106
- 8,043
Kumekucha. Mambo yanazidi kunoga.
Msemaji wa Waziri wa mambo ya nje wa China Bwana Wang Wenbin ameionya Marekani kuwa endapo Nancy Pelosi (US house speaker) atafanya ziara ya kuitembelea Taiwan, August mwaka huu, basi taifa hilo linaloaminika kuwa ndio lenye nguvu ya kiuchumi kwa sasa duniani litaijibu US kwa namna ambayo siyo tu inayoweza kupelekea kuvunjika kwa uhusiano wao wa kidiplomasia, bali pia inaweza hata kuwa ya kijeshi.
Msemaji huyo alisema adhma ya Pelosi kutaka kufanya ziara yakeTaiwan ni cha kichokozi, kwani ni sawa na kuingilia uhuru na mambo ya ndani ya Uchina.
"We are seriously prepared," Msemaji huyo alinukuliwa akisema.
..."and United States should be held responsible for any serious consequences", Mr. Wang aliongezea.
Ifahamike Serikali ya kikomunisti ya China inatambua Taiwan kuwa kama ni sehemu ya ardhi yake, wakati Taiwan yenyewe inataka kujitenga kutoka katika taifa hilo.
Mwezi April mwaka huu Pelosi alihairisha ziara hiyo kutokana na kuugua maradhi ya uviko-19.