China yaongoza duniani katika utengenezaji na uuzaji wa mabasi ya abiria

China yaongoza duniani katika utengenezaji na uuzaji wa mabasi ya abiria

Wewe jamaa unaleta ushabiki kwenye facts kwani green city zipo wapi?

Mbona kuna makampuni mengi tu ya mabus ya michina yamekufa sababu ya mikopo[emoji1787][emoji1787]

Ushawahi kujuliza kwa nini makampuni mengi ya kibongo hayakui licha ya kuwepo na michina ya bei cheese plus mikopo?

Bila wizi hauwezi kutoa hapa bongo kwa biashara ya mabus niamini[emoji1787][emoji1787]
Bongo biashara nyingi zinaendeshwa kwa mapato nje ya biashara husika na hadi biashara isimame yenyewe huenda umetumia zaidi ya miaka mitano. Sasa je wangapi wanaweza kuzi finance hizo biashara bila vyanzo vingine vya pesa.?😂

Ndio maana ufisadi hauwezi kuisha nchini na wafanyabiashara wengi kukimbilia kuwa makada wa chama ili walambe teuzi na kujilimbikizia mitonyo.
 
Na ndio maana ikaitwa biashara kichaa

Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa Abood na Shabiby wameweza kudumu kwenye hii biashara kwa miaka mingi sasa
Wale jamaa wao wanatumia kitu kinaitwa "Goodwill" kibiashara ukishawekeza kwa muda mrefu na ukawa na jina we unakula faida tu. Walishachoma sana pesa sasa wanakula matunda tu. Sasa we kurupuka umuige shabiby 😂😂😂
 
Kwa miaka 9 mfululizo kampuni ya Yutong ya China imekuwa kinara kwa kuuza mabasi mengi zaidi duniani.

Utengenezaji na uuzaji wa mabasi ya abiria imekuwa biashara kubwa yenye ushindani hasa mabasi ya umeme. Mabasi yamekuwa yakitengenezwa kwa kazi na makusudi tofauti tofauti.

Kinachoangaliwa katika ushindani wa biashara hii ni idadi (units) za mabasi ambazo makampuni katika nchi husika yameuza.

Ifuatayo ni 10 bora ya majina ya makampuni yaliyouza mabasi mengi zaidi duniani mwaka 2022 na idadi ya mabasi yaliyouzwa;

(1)YUTONG (China) – 58,688
View attachment 2679250


(2)MERCEDES BENZ (Ujerumani) – 32,612

View attachment 2679307

(3)KING LONG (China) – 26,450
View attachment 2679303

(4)GOLDEN DRAGON (China) – 19,392

View attachment 2874386

(5)MARCOPOLO S.A (Brazil) – 15,831
View attachment 2679298

(6)ZHONGTONG (China) – 15,054
View attachment 2679295

(7)MAN (Ujerumani) – 13,972
View attachment 2679308

(8)HIGER (China) – 11,412
View attachment 2679302

(9)VOLVO (Sweden) – 9,731
View attachment 2679309

(10)SCANIA (Sweden) – 7,777
View attachment 2679310

Katika tatu (3) bora duniani, makampuni matano ya China yameongoza kwa pamoja yaliuza mabasi 130,996, ikifuatiwa na makampuni mawili ya Ujerumani yaliuza jumla ya mabasi 46,584 na Sweden mabasi 17,148

REKODI YA CHINA KATIKA BIASHARA YA MABASI
●Kwa miaka 9 mfululizo kampuni ya Yutong ya China imekuwa kinara kwa kuuza mabasi mengi zaidi duniani.

●China ndilo taifa linalouza karibu asilimia 50 ya mabasi katika soko la dunia.

●China inaongoza kwa kutengeneza mabasi yasiyotumia mafuta (new energy vehicle) Asilimia 90 ya mabasi ya umeme duniani ni yaliyotengenezwa na makampuni ya China.

●Youngman ndilo basi kubwa zaidi lililovunja rekodi duniani lenye urefu wa mita 25 lenye uwezo wa kupakia abiria 300. Lilipewa jina la utani triple bus. Lilitengenezwa na kampuni ya China Youngman Automobile Group Co., Ltd.

View attachment 2679287

●China ndilo taifa pekee duniani lenye viwanda 16 vikubwa vya kutengeneza mabasi; Yutong, Higer, Zhongtong, Kinglong, JMC, Foton, BYD, Golden Dragon, Asia Star, Ankai, Changan, Dongfeng, Nanjing Iveco, Briliance Renault, Sunwin na Sunlong.
The sleeping giant has woken up!
 
Kwenye ndege katengeneza body tu ingini na parts zake zinatoka ulaya
Hilo hakuna tatizo. Watengenezaji wengi wa ndege huagiza baadhi ya vifaa muhimu ili kutengeneza ndege zenye uimara zaidi. Rolls Royce ni kampuni moja kubwa yenye uzoefu wa kuunda injini za magari na ndege. Kampuni nyingi duniani zinatumia injini hizi katika kuunda ndege au magari yao. Si dhambi kwa China kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom