Ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kiserikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Ndg. Samia Suluhu Hassan nchini China.
Leo tarehe 03 Novemba 2022, China imesamehe baadhi ya madeni ya Tanzania.
Sambamba na hilo; Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa China Xi Jinping wameshuhudia utiaji saini mikataba 15 ya kimkakati hii leo jijini Beijing inayolenga kuimarisha ushirikiano, biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili.
View attachment 2406015
View attachment 2406016
View attachment 2406017
Pia akirudi mwambieni Rais wetu kuwa waziri wake wa Ujenzi na Uchukuzi Professor Mbalawa hatufai tena.
Mambo aliyoyatoa Bungeni ni haibu kwa waziri msomi kama yeye. Alitakiwa ajiuzuru mara moja.
Yaani Professor mzima ameshindwa kutoa maelezo juu ya mwendelezo wa mkataba ambao unasadikika ku-exist baina ya serikali na hiyo kampuni iliyo tajwa ambayo ilitakiwa isiwepo tena. Mtu anajiuliza, inakuwaje serikali iwe na umiliki wa 100% hisa, lakini kampuni nyingine ambayo haiko tena, ndiyo ikusanye mapato na kuilipa serikali kwa mkataba upi? Na kidheria inakuwaje kuwaje hapo? Wakati waziri yupo? Anafanya kazi gani mda huo wote?
Watanzania wenzangu nadhani mnajionea wenyewe jinsi gani Rais wetu anavyotumiwa kuwaweka watu kwenye position kubwa za madaraka, ambao kimsingi hawapo hapo kwa maslahi ya nchi bali kwa malengo ya baadhi ya watu ambao wanafaidika na utendaji wa huyo waziri na kuwa kwake hapo.
Mama alikwisha onywa mara kadhaa na watu wenye ku-sense harufu mbaya juu ya uteuzi wa huyo Professor. Nafikiri Mama atakuwa amejionea mwemyewe kuwa chaguo lake la kumrudisha huyo mtumishi ni kazi ya bure.
Mama anatakiwa atambue kuwa sio watu wote wanao kuwa rehabilitated kwa kurudishwa madarakani wanakuwa wamejifunza vitu.
Issue ya Waziri Mbalawa inanikumbusha nyuma kwenye issue ya Professor Mhongo na yale mambo ya Makinikia. Inawezekana vipi waziri husika mwenye uzoefu kama yeye kushindwa kuliona hilo bomu lilipo? Hiyo kwangu ni ishara ya uzembe na ukosekanaji wa uadilifu wa huyo waziri.
Mama Waziri wako Professor Mbalawa hayuko serious na malengo yako. Bado anatenda mambo kwa misingi ya "Business as usual", lakini kimantiki ni Boya tu huyo. Hana Power ya kufanya kazi kwa ufanisi. Hii wizra ni nyeti sana inatakiwa iwe na mwenye vision na maarifa mapana. Vijana wengi wanategemea ufanisi wa hii wizara.
Ni kitu cha kustaajabu sana kuwa leo ndiyo tunasikia pia kuwa hata ule mradi wa SGR kipande cha tano kuzoka Tabora mpaka Kigoma nacho mpaka leo, takribani miaka miwili sasa, haujaanza kutekelezwa wakati Waziri husika na wasaidizi wake akina Kadogosa wapo na wanaendelea kuudanganya umma na wewe Rais kuwa mambo yanakwenda murua. Hivi Mtendaji mkuu wa serikali yuko wapi? Na anafanya nini?
Mama kama wewe baafa ya haya yote badunamshilikilia tu huyo waziri basi endelea, sisi tumemalizana naye.
Asante sana Mama, wewe ni Rais mzuri sana unaye ipenda nchi yako. Hawa ndiyo watendaji watakao tuvusha.
Endelea tu kutuchagulia watu wazuri kama hao. Watanzania wanakushukuru sana.
Mungu ibariki Tanzania na watu wake!