Uh-Oh!
Mkuu 'Maneno'
Umeniuliza maswali ambayo yanaonyesha wazi kabisa hukunielewa nilichoandika hapo nawe ukarukia kujibu bila ya tafakari juu yake.
Hayo maswali uliyoniuliza nina majibu yake, na kama ungekuwa msomaji makini wa mada mbalimbali humu JF ungejuwa bila ya shaka yoyote ninaposimamia kuhusu hayo maswali.
Lakini, niseme, nina kumbukumbu za maandiko yako humu ambayo mara kadhaa tulishakutana na kuwa pande tofauti kati yetu.
Kinachonishangaza hapa leo ni kuhusu hayo maswali yako ambayo majibu yake huwa ni kinyume na misimamo yako.
[emoji3][emoji3][emoji3] Asante sana Mkuu Kalamu kwa mchango wako. Mungu akubariki sana! [emoji120]
Mkuu Kalamu ndungu yangu wewe ndiye mtu uliye nishutumu mimi kwa kauli yako ya kusema kuwa, na kunukuu;
"Umemdharau sana huyo mama anayewateua hao mawaziri."
Umeendelea kusema, ninakunukuu;
"Huwa siwaelewi sana watu kama wewe, sijui lengo lenu huwa ni nini hasa mnapojitoa akili kiasi hiki."
Ndugu yangu Kalamu naomba uelewe kitu kimoja, mimi nikitoa statements zangu humu mara nyingi huwa sifuati misingi ya kiitikadi za kisiasa na wala hutanisikia mimi nashabikia aidha CCM au CHADEMA. Mimi niko kwa ajili ya kutetea maslahi ya watanzania na vizazi vyetu vya baadae na ya nchi yangu ya asili Tanzania.
Mtu anaye perform kazi yake vizuri na ku deliver matokeo chanya kwa wananchi huyo mtu kwangu ni mtukufu, haijalishi anatoka chama gani.
Ndiyo maana inawezekana sisi wawili huko nyuma, pengine, tukawa na misimamo tofauti au mimi kuonekana nashabikia mtu wa upande fulani wa kiitikadi.
Kwa hali hiyo nakubali, ndiyo nilimpenda sana Rais Magufuli kwa matendo na dhamira zake. Na kama wewe hukumpenda Magufuli na hukuyathamini matendo yake, mimi basi sina budi kukubaliana na wewe kwa maamuzi yako hayo. Lakini, hata hivyo, mimi leo itabidi nikuambie ukweli kuhusu Magufuli ndugu yangu.
Kwa sisi tulio zoea kuishi Tanzania na nje ya Tanzania tunayapata mengi sana yanayo tokea ulimwenguni kuliko watu wasio na bahati hiyo au nafasi hiyo.
Wakati wa utawala wa Magufuli Tanzania ilisikika sana nje na watu walikuwa wana jiuliza, Tanzania ni nchi gani na ina nini cha maana? Hivi sasa toka Magufuli atuache, Tanzania nayo imeshatoweka kwenye uso wa dunia. Hakuna mtu anaizungumzia tena nchi yetu kama zama hizo za Magufuli.
Wakati wa utawala wa Magufuli waafrika wengi wanaoishi nchi zilizoendelea, wakisikia Tanzania walikuwa wanataka kumsikiliza Simba wa nchi Magufuli ananguruma nini. Niamini ninacho kueleza.
Mara nyingi nikiwa kwenye ndege kwenda Europe au nikiwa narudi Tanzania, nilikuwa nina enjoy sana ndugu yangu, kusikia sifa za Rais wetu John Pombe Magufuli pindi unapojitambulisha wewe mwenyewe kwa wasafiri wenzako kuwa wewe ni mtanzania.
JPM alisifika sana na alikuwa kivutio kikubwa sana cha nchi yetu, japo kuwa wapinzani wakishirikiana na majasusi ya kigeni ya Amerika na Europe na ma NGOs wao kutumia nguvu kubwa za kumpaka matope, asiyo stahili kwa ulafi wao wa madaraka ambayo hivi sasa yanawatokea puani.
Hivi sasa wametulia kimyaa, kwasabau wafadhili wao waliokuwa wakiwashawishi na kuwapa nguvu, hawana interest nao tena kwa mabadiliko yaliyotokea ya vita ya Ukrain na World crisis. Wamekwishni!
Magufuli pia ndugu yangu aliwapa faraja kubwa sana waafrika wa kutoka nchi nyingine za Afrika kwa kuwa Role Model wa ma presidents wa Afrika wanavyotakiwa kuwa. Nakuambia hivi ndugu yangu kwa sababu mimi mwemyewe nimeyashuhudia hayo. Sijaambiwa na mtu.
Kila sehemu Europe tukikutana na waafrika wenzutu, mazungumzo yalikuwa ni kuhusu President wa Tanzania JPM.
Of course mambo kama haya hutayasikia kwenye Mainstream Media za wazungu kama BBC, CNN, CNBC na mengineyo. Hizi media haziwezi toa vitu kama hivyo, kwasababu, hivi vyombo viko kwa lengo moja tu, la kutufanya sisi tuwe chini ya mabeberu kwa kupiga propaganda za wafadhili wao.
Tambua kuwa, nchi nyingi za Europe zinategemea cheep resources kutoka Afrika.
Serikali zote za wazungu na mabepari wao zimeapa kutotusaidia sisi kuinuka kiuchumi, ili tujitegemee wenyewe. Hili wanatakiwa viongozi wetu walitambue.
Sasa nikimwona Rais ambaye anajitahidi kwa kadri anavyoweza, kuhangaika kwote huko kutafuta misaada ya kuwaneemesha watanzania, anawapa watu incompetent madaraka ya kumsaidia kutekeleza malengo yake hayo, inanisikitisha sana.
Utakubaliana na mimi kuwa watu wengi aliowaweka kwenye maeneo nyeti ya utendaji, wengi wao hawako serious na majukumu yao ya utendaji na pia hawana uwezo huo. Maisha na maendeleo ya watanzania kwao ni nothing.
Ni watu ambao mimi nawaona hawajitambui na hawajui ulimwengu wa leo uko vipi. Na unakwenda wapi. Ni watu ambao kifikra na kimaono bado wako kwenye karne ya kumi na tisa.
Wangejua ulimwengu wa leo jinsi ulivyo, sidhani kama wangekuwa na luxouary ya kufurahia, kupotea kwa hela za umma kijinga namna hiyo. Wangekuwa watu wengine kabisa, wenye malengo thabiti ya kupigania maendeleo ya nchi yao kwa hali na mali.
Hapo ndipo unapoona lawama zangu kwa Mama Samia. Amewaacha hao watu wale kwa urefu wa kamba zao, ni kauli yake mwenyewe kwenye baraza lake la Mawaziri.
Rais wetu amekwenda Amerika kuunadi Utalii wetu na kushuhudia utiaji saini wa mikataba kadhaa ya uwekezaji nchini, tujiulize kitu gani watanzania wamefaidika na mikataba hiyo so far?
Na sasa tunaambiwa pia kuwa ameshuhudia utiaji saini wa mikataba 15 nchini China. Tutayaona hayo matokeo yake kwa watanzania.
Bro, kwa jinsi ninavyowajua wazungu, hawana interest hata moja ya kutuona sisi tukipaa kama wachina, kama hatutajitahidi sisi wenyewe kwa nguvu zetu.
Kitu ambacho Rais wetu, nadhani, hajui ni kwamba watanzania kwa ujumla hawana imani tena na mikataba na makampuni ya nchi za nje. Wanaona ni mikataba ya kuiuza nchi na kutuvua sisi nguo. Wanaona Rais anapoteza tu mda wake. Watanzania hawataki kusikia hayo maswala ya mikataba. Wanachotaka ni yeye awe mkali katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini kwa watendaji wake .
Naamini ya kwamba umefuatilia Report ya CAG na maelezo yaliyotolewa na kamati za Bunge na maazimio yaliyotolewa.
Sasa kama Mama amezisikia scandals hizo za ubadilifu wa hela za umma na mawaziri aliowateua kushika dhamana hizo, kushindwa kuwadhibiti waarifu kwa kuwachukulia hatua stahiki za kisheria, wewe unafikiri atakuwa anawatendea watanzania haki kweli?
Mama ajaribu sasa strategy nyingine. Hao washauri wake wanao msaidia kuteua viongozi sio watu wema kwake. Wananamshauri watu ambao hawana uwezo mkubwa wa ku perform mambo vizuri. Ni watu ambao hatima yake kumchonganisha yeye na wananchi wake.
Katika karne hii ya 21Tanzania inahitaji viongozi wenye maono na ufanisi mkubwa katika utendaji na sio kuwa na viongozi wasio weza kujituma na kubuni mbinu mpya za kutafuta nyezo za kuleta maendeleo kwa watu, viongozi wa aina hiyo hawahitajiki kabisa. Ni mzigo tu kwa Taifa letu na wanaturudisha nyuma.
Sikiliza mwenyewe yaliyojiri jana Bungen:
Nina mpa pole Mama na watanzania wezangu.
Mungu aibariki Tanzania na watu wake! Amina[emoji120]