Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
It doesn't make sense at all...Ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kiserikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Ndg. Samia Suluhu Hassan nchini China.
Leo tarehe 03 Novemba 2022, China imesamehe baadhi ya madeni ya Tanzania.
Sambamba na hilo; Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa China Xi Jinping wameshuhudia utiaji saini mikataba 15 ya kimkakati hii leo jijini Beijing inayolenga kuimarisha ushirikiano, biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili.
View attachment 2406015
View attachment 2406016
View attachment 2406017
Nashukuru umeuona ulaghai huo.Kusema “mikataba 15 ya kimkakati”, bila kutaja ni mikataba gani ni sawa na bure tu. Sasa hiyo taarifa inamsaidia mwananchi wa kawaida kivipi?
Hapo hakuna tofauti na mikataba ya siri. Wangesema na hiyo mikakati ndo tutoe maoni. Maana ukiona kuna madeni yamesamehewa, halafu mikataba haitajwi, basi kuna uwezekano tumepigwa.
Umemdharau sana huyo mama anayewateua hao mawaziri.Watanzania wenzangu nadhani mnajionea wenyewe jinsi gani Rais wetu anavyotumiwa kuwaweka watu kwenye position kubwa za madaraka, ambao kimsingi hawapo hapo kwa maslahi ya nchi bali kwa malengo ya baadhi ya watu ambao wanafaidika na utendaji wa huyo waziri na kuwa kwake hapo.
Mh.Samia ni mwanadiplomasia mzuri sana kuliko Hayati JPM lakini hawezi kuwa bora kuliko Kikwete na kumfananisha na Nyerere ni kutomtendea haki Nyerere. Yule alikuwa wa kiwango kingine kabisa bado hajapatikana wa kumfananisha naye.Hakika Rais Samia Ni zawadi kwetu watanzania Tunayopaswa Kujivunia Na kuiheshimu, Amejenga Imani kwa kila mtu juu ya Tanzania yetu, kila mtu na kila Taifa kwa Sasa linatamani kushirikiana na Tanzania, Kila mtu anajiona Fahari kuwa na ukaribu wa kibiashara na Tanzania, Tanzania ya Nyerere kidiplomasia imerejeshwa na Rais Samia, Ni Kama Nyerere amezaliwa ndani ya Mama Samia, Tuendelee kutegemea makubwa kutoka kwa Rais Samia katika kuvutia wawekezaji watakao Leta fursa za ajira kwetu vijana
Bora wadai iwekwe wazi bungeni kuliko kudhania tumepigwa tu bila kuwa na ushahidi mahsusi. Upuuzi huuHahaaa unazani kwa nini hio.mikataba haiwekwi wazi waka kujua majina yake? Wewe hio.mikataba 15 unaijua? Unazani kwa nini haiwekwi wazi?
Nchi kubwa hii na rasilimali nyingi kila mmoja kapewa sehemu yake na bado vyanzo vingine vimebakiNilifikiri nchi kapewa waarabu .wa Oman na UAE..?
Unafikiri hatuna hiyo pesa bln 31? Symbion pekee tumemlipa billion 350 hata hatujamdai atulipe kodi yoyote.Unazo hizo? Unafikiri zinaweza kujenga vituo vya Afya vingapi? Shule ngapi? Madarasa mangapi?
Ulitaka upewe wewe? Kuna mijitu haioni zuri lolote lifanywalo na serikali, sijui ni ukosefu wa elimu?! Wee wadhania makubaliano yanakuja bure bure tu? Kuna nchi ngapi duniani zataka maslahi kutoka China? The fact kwamba rais amefanikiwa kufikia makubaliano hayo inaonesha ubingwa wa kukinaisha na kutoa hoja. Si lazima kwa China kuwekeza Tanzania, wala Tanzania si chochote katika maslahi mapana ya China. Nyie watu mlishibishwa uzalendo mchwara na aliyeondoka mwaona Tanzania ni kama kitovu cha dunia!Wachina sio MAFALA mpaka wasamehe bure pesa Yao kila mtu anajua kilichompeleka Samia China ni mkataba wa bandari ya bagamoyo na gesi ya mtwara kwakifupi nchi amepewa mchina tayari pia kuna mikataba mingine mingi Tanzania imeingia na China.
tumeshapigwa tayari acha watuzuge kusamehe madeni.
Huo ni uzushi wa Chadomo hao wanaitwa DiasporahMasharti haya si bora tu tulipe deni au wadau mnasemaje?
Hata wewe ukiwa mtu wa kutoa offer kila mtu atakupenda. Hali kadhalika nchi ikiwa inagawa rasilimali hovyo kila mtu ataipendaHakika Rais Samia Ni zawadi kwetu watanzania Tunayopaswa Kujivunia Na kuiheshimu, Amejenga Imani kwa kila mtu juu ya Tanzania yetu, kila mtu na kila Taifa kwa Sasa linatamani kushirikiana na Tanzania, Kila mtu anajiona Fahari kuwa na ukaribu wa kibiashara na Tanzania, Tanzania ya Nyerere kidiplomasia imerejeshwa na Rais Samia, Ni Kama Nyerere amezaliwa ndani ya Mama Samia, Tuendelee kutegemea makubwa kutoka kwa Rais Samia katika kuvutia wawekezaji watakao Leta fursa za ajira kwetu vijana
Maendeleo ya uchumi tunayaona kweli, litre ya mafuta ya kula ef 6 huku kilo ya maharage elfu 4 ndani ya mwaka tuHuyu ndio Rais aliyefanikiwa ndani ya muda mfupi Sana kujenga uchumi wa nchi unaogusa maisha ya mtanzania, kila mtu anaguswa na maendeleo makubwa ya uchumi wetu,