China yasamehe baadhi ya madeni ya Tanzania

Ukishaona mikataba haitajwi wazi badala yake wanajifichia kwenye vijineno mkakati jua tumepigwa kama kawaida!.

Hata kwenye Roho Tour walituzuga watawataja wafadhili wa safari hadi leo kimyaaaa wanadhani wananchi wote hamnazo tumesahau!.
 
It doesn't make sense at all...

Unasemehewa mkopo wa TZS 34.7bn halafu wakati huohuo huyo huyo anakupa mkopo mwingine wa $56.72m sawa na karibu na TZS 1.31trn...!

Hii imekaaje..?
 
Nashukuru umeuona ulaghai huo.
Nilitikisa kichwa niliposoma hilo gazeti la Zuhura hapo juu. Hawa watu wanawadharau sana waTanzania siku hizi.

Hata hayo madeni tunayodaiwa na wachina hawasemi ni kiasi gani tunachodaiwa, sehemu ya ulaghai wenyewe.

Siyo kwamba wamesahau, au kuona si muhimu kuyataja hayo, bali ni uamzi wa maksudi kabisa kufunika kombe!

Halafu angalia ujuha wanaodhani waTanzania wanao: "Miradi iliyosajiriwa ya bilioni 9.6" inakuwa ni sehemu muhimu ya kutueleza sisi wapumbavu ili tushangilie! Hiyo dola bilioni tisa, nusu yake tu ingeanzishwa hali ingekuwa ni tofauti na ilivyo sasa!

Huyu mama katoka na zaidi ya dola bilioni 7, kule Arabuni; sasa kuna bilioni 9 za China!
 
Umemdharau sana huyo mama anayewateua hao mawaziri.

Huwa siwaelewi sana watu kama wewe, sijui lengo lenu huwa ni nini hasa mnapojitoa akili kiasi hiki.
 
Mh.Samia ni mwanadiplomasia mzuri sana kuliko Hayati JPM lakini hawezi kuwa bora kuliko Kikwete na kumfananisha na Nyerere ni kutomtendea haki Nyerere. Yule alikuwa wa kiwango kingine kabisa bado hajapatikana wa kumfananisha naye.
 
Hahaaa unazani kwa nini hio.mikataba haiwekwi wazi waka kujua majina yake? Wewe hio.mikataba 15 unaijua? Unazani kwa nini haiwekwi wazi?
Bora wadai iwekwe wazi bungeni kuliko kudhania tumepigwa tu bila kuwa na ushahidi mahsusi. Upuuzi huu
 
Asante mchina, lakini bado tunataka utuondolee nusu ya madeni tuliyo kuwa nayo kwa kwao jamani, maana nao pia wanafaidika sana na nchi yetu!
 
Ulitaka upewe wewe? Kuna mijitu haioni zuri lolote lifanywalo na serikali, sijui ni ukosefu wa elimu?! Wee wadhania makubaliano yanakuja bure bure tu? Kuna nchi ngapi duniani zataka maslahi kutoka China? The fact kwamba rais amefanikiwa kufikia makubaliano hayo inaonesha ubingwa wa kukinaisha na kutoa hoja. Si lazima kwa China kuwekeza Tanzania, wala Tanzania si chochote katika maslahi mapana ya China. Nyie watu mlishibishwa uzalendo mchwara na aliyeondoka mwaona Tanzania ni kama kitovu cha dunia!
 
Masharti haya si bora tu tulipe deni au wadau mnasemaje?
 

Attachments

  • Screenshot_20221104-144522_WhatsApp.jpg
    267.7 KB · Views: 4
Hata wewe ukiwa mtu wa kutoa offer kila mtu atakupenda. Hali kadhalika nchi ikiwa inagawa rasilimali hovyo kila mtu ataipenda
 
Hao waliosamehewa ni makosa gani hayo , hlo hlo deni lililosamehewa Tanzania haiwez shindwa kulipa ...!!
 
Huyu ndio Rais aliyefanikiwa ndani ya muda mfupi Sana kujenga uchumi wa nchi unaogusa maisha ya mtanzania, kila mtu anaguswa na maendeleo makubwa ya uchumi wetu,
Maendeleo ya uchumi tunayaona kweli, litre ya mafuta ya kula ef 6 huku kilo ya maharage elfu 4 ndani ya mwaka tu
 
Nasikia Kuna uozo mwingi sanaaa,
Bandari ya bwagamoyo ndo Basi tenaaa macho kuvimba wanaichukua,
 
Hivi ni bilioni 31 ya madafu, au mimi ndo sioni.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…