China yatuma ndege 38 za kijeshi mpakani mwa Taiwan

SAWA
 
Tatizo wanafikiri kila siku ni jumanne, hawajui kesho itakuwa jtano
Hawajui kwamba hii dunia imetawaliwa na dola mbali mbali...
Hawajui kwamba yesu kazaliwa kwenye ukoloni, chini ya warumi waliokuwa wanatawala dunia...
Hawajui ya kwamba Turkey imetawala dunia...
Hawajui kwamba yalikuwepo mataifa yenye Tech za hatari na advanced kabisa kwa kipindi hiko na muda wao ulifika wakawaachia wengine...
Mwisho kabisa tuseme kuimba kupokezana, hatuna budi sasa bali kujifunza ki China..., Ubishi wa kipumbavu kwa kudharau uwezo wa China alionao hivi sasa, nguvu kazi ya taifa na wingi wao...
Tuko hapa hizi comment watasoma wajukuu zetu na kusema tuliona mbali...
 
Yaani US alete vifaru toka toka DC mpaka Alaska wakat huo RUSSIA anawaangalia tuu hehehe
Sijataka US aingie vitani ila alishaingia vitani na RUSSIA zamani sana kuhusiana na CRIMEA nandio maana mpaka leo RUSSIA anaekewa vikwanza na US kisa CRIMEA
Unataka utuaminishe nn labda[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Ungejua uchumi wa marekani nao uko kwenye bubble bust. Wanaprint hela tu wale Sasa hv
Uchawi upo hapa, kwa mda mrefu wanafanya dirty floating na wakubwa wengi washawashtukia. 2015 BRICS walitaka kuunda Brexton Woods yao sijui walikwamia wapi...
Zimbabwe wakiprint pesa inashushwa thamani ilhali wao tunasikia tu sijui stimulus package na takataka zingine ila kwakuwa yeye mbabe hatuna budi kukaa kimya!
Kifo chake chaja, by 2050 China watakua na GDP 2x ya USA .... Labda apigane na ashinde vinginevyo itakuwa ndo bye bye
 
nimesema ikitokea vita pale Alaska ni njia muhimu na rahisi mno kwa russia kuingia Us.
 
K
Ukraine amekuwa akiomba kujiunga na nato for almost 15 years(sijui kwasasa) sasa wewe habari yakuwa cremia ilimegwa wakat Ukraine ikiwa ndani ya nato umezitoa wapi?.

View attachment 1963732
Kama wanawapenda hao kwanini hawawafungulii mlango...... ..wamejua watakacho kumbana nacho.....hio pia kwa Taiwan watapigwa tu maneno ya faraja huku mchina anabeba nchi
 
Ukraine haipo NATO na siioni in the future, labda Russia ipotee!
Haya mambo bana ni kwamba kila mtu anadeffend interests zake... wakati mnajiunga kumpinga flani, mmoja au wawili kati yenu ana/wanamtegemea huyo 'flani' kuafanikisha mambo yao ya msingi.
Rejea: NORD STREAM 2 project
Rejea: USA troops evacuation in Aghanistan
 
Nchi za Afrika hatuna budi kupeleka shukrani kwa Chinese...
China imetufungulia dunia, Infinix, Tecno, Xiaomi hizi piki piki n.k, ujenzi wa miundo mbinu na majengo mengi huku Africa, zana za kijeshi kama ndege na silaha, Tanzania ndege zetu zote za kijeshi ni Chinese halafu kuna watu wanawabeza...
Wazungu walikuwa hawana muda wa kufanya biashara na sisi, iPhone tunanunua si kwa ajili ya Africa huo ndio ukweli... China wamewatajirisha wafanya biashara wangapi pale Kariakoo?
China kaleta tik tok ku compete na IG,Youtube, Facebook... US kawafanyia roho mbaya... Huawei kaleta 5G US kashinikiza wenzie waisusie na si salama...
Leo hii unasema eti China bado Sana, don't you see wanavyoogopeka?

Hivi nyie pasipo gharama nafuu za ujenzi, mngekua mnaendesha gari kwenye vumbi bado ukweli mchungu, boda mnazopanda kila siku ni China huyo, ukifika kwako unawasha TV unakutana na China, ukiwasha iphone yako utumie ni assembled in China, ukishika simu uingie jf ni China, kwenye nguo na viatu ndipo usiseme kabisa... Ukiona hizo dalili ujue kabisa huyo ndio superpower mwenyewe kwamba humkimbii 😂😂😂
Mzungu alikuwa hana muda wa kufanya biashara na sisi , sisi kwao ni kama kima tu, mzungu alikuwa ana deal na Arabs na wazungu wenzie, Afrika kwa huu umasikini ilikuwa ngumu Sana kuweza kuendana na kasi ya dunia...

Kwa pamoja tuseme asanteni wa China...

Mchina kaifungulia dunia Afrika...,
 
K

Kama wanawapenda hao kwanini hawawafungulii mlango...... ..wamejua watakacho kumbana nacho.....hio pia kwa Taiwan watapigwa tu maneno ya faraja huku mchina anabeba nchi
kwa hiyo tuchukue lipi na tuache lipi katika hoja yako? Ukraine kuwa memba wa nato kabla cremia hajamegwa ama swali lako la kwanini jumuhia ya nato imechelewa kupokea mwanachama mpya(ukrane) kwasababu ya hofu yao tu dhidi ya urusi?.

ulikusudia nini hasa kutulisha matango pori kuwa Ukraine alikuwa ni memba wa nato wakati cremia inapokonywa?.
ulipitiwa tu ama ulikusudia?
 
Na mchina anakuja kutuondolee mkoloni wakizungu Africa
 
ila we jamaa wewe basi tu.
🤣🤣🤣🤣🤣 ushauri wangu kwako tafuta chanzo kingine cha habari sio jf tu.
ngoja nikashuse kago nipate hela ya kula
 
ila we jamaa wewe basi tu.
🤣🤣🤣🤣🤣 ushauri wangu kwako tafuta chanzo kingine cha habari sio jf tu.
ngoja nikashuse kago nipate hela ya kula
China haepukiki and it's too late...
Hata uwe tajiri China haepukiki mzee... Ukweli mchungu...
Ukitaka kuona matajiri hapo Kariakoo wanaanza shindia boflo na soda, China iingie vitani na exportation zisimame...
Hio ndio maana ya superpower...
 
Kosugi na and 100 others nawaomba tafadhalini achaneni na huyo jamaa, asiwatoe kwenye reli.

Mna madini, sisi wasomaji tunanufaika kupitia mjadala huu! Anayetusi mwacheni.

Isije ikawa kama suala rais Mwinyi alilolizungumzia upo mtoni unaoga chizi akaiba nguo zako, ukimkimbiza hali ya kuwa upo uchi na chizi ana mavazi hata kama ni ya hovyo nafikiri mnajua ni nini kitatokea.
 
Ukraine sio mwanachama wa Nato........angalia vizuri historia ya Crimea ilikuwaje ikawa sehemu ya Ukraine na raia wa hapo wengi wana asili ya wapi utaona kwanini ilikuwa rahisi kwa Urusi kuichukua kibabe.
 
Hakuna kilichomkuta na ndio maana zinapatikana hizo Korea mbili. Wewe usitake kutufanya wengine kama hatujui kusoma.
Kasome hiyo vita vizuri halafu urejee hapa useme kuwa hakuna kilichomkuta.
Kama hakuna kilichomkuta basi maeneo yaliyokaliwa na N.K kwa mabavu yangerudi.
 
Ila suala la kusema Taiwan iishinde China kivita umekosea sana.
CHINA IME ADVANCE KIJESHI SANA TENA SANA.
 
Ila suala la kusema Taiwan iishinde China kivita umekosea sana.
CHINA IME ADVANCE KIJESHI SANA TENA SANA.
Nikweli haiwezi kuishinda ila inaweza kujilinda bila China bara kuigusa ardhi ya Taiwani.
 
Nikweli haiwezi kuishinda ila inaweza kujilinda bila China bara kuigusa ardhi ya Taiwani.
Kaka watu washaingiza mpk ndege ktk anga lako bado utasema unaweza kujilinda dhidi yake!!??
 
Kaka watu washaingiza mpk ndege ktk anga lako bado utasema unaweza kujilinda dhidi yake!!??
Hata Russiana uwa anaingiza figher jet kwenye anga la UsA pia Us.A kwa Russia uwa wana zi nchi husika inatuna ndege kuzionya.
 
Hata Russiana uwa anaingiza figher jet kwenye anga la UsA pia Us.A kwa Russia uwa wana zi nchi husika inatuna ndege kuzionya.
Anaweza akaingiza 1 wakiishtukia wanatuma ndege inawaelekeza kugeuza ila sio hii ya kuingiza madege yote hayo.....ukifanya hivyo kwa taifa lenye msuli hapo ushamaanisha unataka vita....na hiko ndo kitu china anakitaka anasubiri upande wa pili wa jibu ....na wao wapeleke za kwao kwake au watume tu hata ka roketi kuelekea china ili na wao wajibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…