CHINESE CUISINE: Nini ule ukienda kwenye mgahawa wa kichina...

CHINESE CUISINE: Nini ule ukienda kwenye mgahawa wa kichina...

Watu8

Platinum Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
73,773
Reaction score
102,126
Katika ulimwengu wa vyakula na mapishi kuna aina mbalimbali ya vyakula ambavyo upande mmoja wa dunia vinaweza kuwepo na upande mwingine kukosekana.

Ukiachana na hilo pia kuna jambo moja inabidi tutambue kuwa sehemu kubwa ya dunia aina ya raw materials za vyakula ni ile ile lakini namna ya upikaji ndio hutofautiana.

Katika thread hii ningependa kuweka bayana baadhi ya vyakula vilivyopikwa kwa recipes za kichina ambavyo Mtanzania na Muafrika yoyote anaweza kula pasipo kupata tabu ya ladha.

Kwa wale waliopo nyumbani Tanzania wanaweza kuingia kwenye Migahawa ya Kichina iliyopo huko na kuagiza hizi menu vivyo hivyo na kwa wale waliopo nje ya Tanzania.

NB:
Vyakula vingi vya kichina hupikwa kwa mtindo wa mboga ambapo ulaji wake huambatana na wali 'steamed rice' (huu hauwekwi mafuta wala chumvi), mikate ya kichina (mantou), tambi za kichina (miantiao) n.k..
Hivyo hakikisha uagizapo dishes hizi unaagiza na kimojawapo cha hivyo, lakini mimi nashauri muagize wali kwani ndio wengi wetu tumeuzoea.

Thread hii haitaelekeza namna ya upikaji wa chakula chochote cha Kichina bali itakupa mwangaza tu wa nini uchague utapoingia katika mgahawa wa Kichina.

Pia naomba sana mkuu Invisible na X-PASTER kwa heshima na taadhima thread hii uiweke kama Sticky thread ili iwe msaada kwa wananchi wengi.
 
Last edited by a moderator:
Chakula hiki chenye asili ya Jimbo la Sichuan hujumuisha vipande vya kuku, karanga zilizokaangwa, pilipili, hoho, karoti na spices kidogo za kichina ambapo vitu hivi vyote hukaangwa kwa pamoja na kupata mchanganyiko kama unavyoonekana katika picha hii hapa chini.

Ukiagiza mlo huu hakikisha unaagiza na wali(ingawaje huwa served na wali hata kama hautaagiza), pia kitu cha kuzingatia ni kuomba usiwekee pilipili(lajiao) hususani kama wewe sio mtumiaji.
 
炒饭 (chǎofàn)

Huu ni wali uliokaangwa (kwa muonekano ni kama pilau kama ukiwekwa soya source) ambao mara nyingi huja katika aina mbalimbali mathalani wali uliokaangwa na nyama ya ng'ombe/kitimoto/kuku, wali uliokaangwa na mayai/mbogamboga/mahindi mabichi. Mchanyato huo wakati mwingine hujumuisha viungo vyenye harufu nzuri, pilipili hoho, karoti, pilipili wakati mwingine huweka Soya source ili kubadili rangi nyeupe ya wali na kuupa ladha murua.

1. Wali uliokaangwa na nyama ya ng'ombe huitwa - 牛肉炒饭 (niu rou chaofan)

2. Wali uliokaangwa na nyama ya kuku huitwa - 鸡肉炒饭 (ji rou chaofan)

3. Wali uliokaangwa na nyama ya kitimoto huitwa - 猪肉炒饭 (zhu rou chaofan)

4. Wali uliokaangwa na mayai huitwa - 鸡蛋炒饭 (ji dan chaofan



chaofan.jpg
 
铁板牛肉 Tie Ban Niu Rou

Hii ni nyama ya ng'ombe ambayo hukaangwa kwenye kikaangio cha udongo au brittle iron. Kwa kawaida mjumuiko wake huwa na vitunguu maji, pilipili hoho, nyama ya ng'ombe na pilipili za kawaida na inapoletwa mezani huwa inaendelea kukaangika kutokana na moto ulijihifadhi katika kikaangio.


jumbo1.jpg
 
Vile vyakula wamechanganya nyama ya nyoka vinaitwaje? Nataka kuvikimbia kama ukoma

Kama una mpango wa kula katika mgahawa wa kichina basi jaribu kuchagua hizi menu ninazoziweka hapa na nitaendelea kuweka hapa.

Nyama ya nyoka huitwa 蛇肉 (she rou) hauwezi kuletewa nyoka au mbwa pasipo kuagiza maana nyama hizo ni gharama kidogo.
 
回锅肉 (huíguōròu) - Twice Cooked Pork

Hii ni nyama ya kitimoto hivyo kwa wale ndugu zangu msiotumia hii bidhaa inabidi kutoagiza hii.

Ni chakula chenye asili ya Jimbo la Sichuan na kawaida huwa haina vikorombwezo vingi zaidi huwa na majani ya kabichi ambayo huwekwa sour vinegar ili kuleta ladha ya uchachu na wakati mwingine huambatana na pilipili hoho na pilipili za kawaida.


201203151331794297.jpg
 
大盘鸡 (Da Pan Ji)

Hiki ni chakula chenye asili ya Jimbo la XinJiang lipatikanalo Kaskazini Magharibi mwa China na wengi wa wapishi wa pishi hili ni Wz XinJiang ambao wana migahawa karibia kila kona ya China na baadhi ya nchi nje ya China.

Chakula hiki huwa ni mchanganyiko wa supu ya vipande vya kuku, viazi mviringo na viungo (seasoning spices) vingine vingi kwa ajili ya kutia ladha na harufu murua.


20110118134826789.jpg
 
西红柿炒鸡蛋 (Xi Hong Shi Chao Ji Dan)

Chakula hiki ni mchanganyiko wa mayai yaliyokaangwa na kuchanganywa na supu ya mayai.

Kwa kawaida huwekwa sour vinegar na viungo vinginevyo kuleta ladha nzuri mdomoni...


17441084.jpg
 
重庆辣子鸡 (Chóngqìng làzǐj&#299😉

Kama wewe ni mpenzi wa chakula chenye pilipili kali basi jaribu kula hii menu kwani pengine nusu huwa ni pilipili na nusu nyingine huwa ni vipande vya kuku na viungo vingine.


35-%E9%87%8D%E6%85%B6%E8%BE%A3%E5%AD%90%E9%B8%A1-Chongqing-Style-Spicy-Chicken-1024x768.jpg
 
mmmh!! sijui kwann mimi nikiwa migahawa ambayo vyakula vyake ni vile ambavyo huwa vinavuta hisia za kushinda kukila huwaga na opt kula french fries na nyama ya ng'ombe ama samaki aliyekaangwa.

kiti moto ya mchuzi?? siwez ama kuku wa kisasa wa mchuzi huyu nitamtapika ama mayai yaliyopondwa pondwa kama uji mzito haya nayo nitarudisha chenchi
 
糖醋里脊 (táng cù lǐ ji) - Sweet and Sour Pork

Chakula hiki hutengenezwa na nyama ya kitimoto na huzungushiwa na seasonings ambazo huwa na ladha kama ya sukari hivi.


113256085_80683e86e7.jpg
 
kiti moto ya mchuzi?? siwez ama kuku wa kisasa wa mchuzi huyu nitamtapika ama mayai yaliyopondwa pondwa kama uji mzito haya nayo nitarudisha chenchi

Twice Cooked Pork huwa haina mchuzi, hicho unachokiona ni mafuta tu yaliyotumika yanayochuruzika kutoka kwa hiyo nyama...

Xi Hong Shi Chao Jidan (Mboga ya Mayai) huwa na mchuzi wa nyanya na wala sio mchuzi wenye ile harufu ya mayai kwani hayo mayai hukaangwa pembeni kabla. Usifananishe na ile mboga ya kibachela ambayo wabongo wengi huvuruga mayai ndani ya mchemsho wa nyanya.

Vyakula karibia vyote utakavyoviona hapa mimi tayari nimeshawahi kuvila na najua kwa taste yake Watanzania wengi wanaweza kula. Binafsi nipo selective sana kwenye kuchagua vyakula na ladha yake.
 
干煎黄鱼 (Gan Jian Huang Yu) - Pan Fried Yellow Fish

Ni samaki aliyekaangwa na wakati mwingine huwekwa viungo vyenye kumfanya awe na ladha nzuri mdomoni.


3254577175_05b7ca0163_o.jpg
 
重庆辣子鸡 (Chóngqìng làzǐj&#299😉

Kama wewe ni mpenzi wa chakula chenye pilipili kali basi jaribu kula hii menu kwani pengine nusu huwa ni pilipili na nusu nyingine huwa ni vipande vya kuku na viungo vingine.


35-%E9%87%8D%E6%85%B6%E8%BE%A3%E5%AD%90%E9%B8%A1-Chongqing-Style-Spicy-Chicken-1024x768.jpg

hiki utawashwa mpaka kunako loh!!! utakula huku unalia...
 
鱼香茄子 (Yu Xiang Qie Zi) - Eggplant with Sweet and Sour Flavor

Hili ni chakula kitengenezwacho na biringanya ambazo hukaangwa na kuwekwa viungo pamoja na sour vinegar huku kikichagizwa la ladha ya usukari kwa mbali. Kuna baadhi ya wapichi huwa wanaweka nyama ndogo ndogo za kuku au bata.


20090924054140949.JPG
 
watu8 naona leo unatupeleka china! Usije kutulisha froglegs tu!
 
Last edited by a moderator:
红烧茄子 (Hong Shao Qiezi) - Braised Eggplant/Red Cooked Eggplant

Hiki ni chakula pia kinachotokana na biringanya lakini huwekwa sauce nyekundu na pia kuna baadhi ya waandaaji huweka pia sukari kwa mbali.


9124a485e6add84a0669dc26a06fc55c.jpg
 
watu8 naona leo unatupeleka china! Usije kutulisha froglegs tu!

Ha ha ha!!!

Usijali maana kila chakula niwekacho hapa ninazingatia ulaji wake nyumbani Afrika na Tanzania.

Sio kila Chinese Cuisine utaiona hapa maana najua kuna wengine hamtoweza hata kuvitazama
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mimi nataka nijaribu kula konokono ,vyura na nyoka. .unaweza kupata menu yake nione kabla sijafanya maamuzi magumu?
 
Back
Top Bottom