Huo mmea hatari sio wa kukurupuka
kwenye sehemu nilizowahi kuwaona watu ambao wapo timamu wakiutumia mara nyingi niliwaona hawavuti ile moja kwa moja kutoka kwa pusha, huwa wana changanya na vitu kama tumbaku ndio vile unaona mtu anaifinya finya na vidole kwnye kiganja, ile ni kupunguza ukali wa kilevi apate ile vibe ya dakika chache tu na stim ziwe za kawaida tu na kuendelea na mambo mengine.
hawapigi moja kwa moja wanasema kwanza sio salama kwasababu mmea wa huku kwetu unaoteshwa maporini sio kama nchi nyingine unavyooteshwa kwa matunzo ya hali ya juu, halafu kitu kingine stimu yake huwa "inaning’inia” muda mrefu, inaweza kukaa kwa masaa mengi na kukupotezea umakini wa maisha unakuwa mtu wa kucheka cheka au kukaa kimya unatafakari kwanini serikali isitatue tatizo la kifungua kinywa kwa kujaza majani ya chai ziwa victoria. wengine hufikia stage ya dish kuyumba hawajijali tena.