Chonde chonde viongozi wa CHADEMA; Tazameni hili kwa upana wake


Kuna msemo unasema "Mambo mawili yanaweza kuwa sahihi au kweli kwa pamoja kwa wakati mmoja" kwa mfano;
  1. Mbowe ni kiongozi mwenye mchango mkubwa ndani ya CDM kwa kadri alivyokitumikia, kukipambania na kukikuza chama kwa miaka zaidi ya 20.
  2. Mbowe ni kiongozi aliyemaliza uongozi wake kwa sintofahamu na kutia doa chafu alama yake ya uongozi ndani na nje ya chama.
au
  1. CDM Ina vijana wenye kiu ya mabadiliko na ambao wako tayari kujitoa kusukuma chama kwa gharama yotote.
  2. CDM ina vijana ambao bado hawana ukomavu kwenye siasa, wanajifunza na wanahitaji kuelekezwa pale wanapofanya ndivyo sivyo.
Taasisi au mtu yoyote ambaye hayuko tayari kukosolewa na kujisahihisha huyo ni mfu.
CDM fanyieni kazi maoni, msichague yale tu mnayopenda kuyasikia hata haya magumu, yapokeeni.
 
Kila siku baadhi ya wanachama wanamtukana JPM na Samia yupo kimya, huoni kuwa haya mambo huwezi kuwa na control nayo? Heche aanze kuangalia nani anamtukana Mbowe? Hiyo ni nidhamu na maadili ya mtu mmoja mmoja peke yake, kama Makonda alipompiga kibao cha shavuni mzee Warioba. JK akampa ukuu wa wilaya Makonda na kumsifia
 
Mbowe aliwakemea wakina Yericko na Ntobi walipokuwa wanamsemea ovyo Lissu. Huo ndio uongozi. Ukiyanyamazia hadharani ina maana unakubaliana nayo.

Amandla...
 
Wembo amejivunjia heshima yeye mwenyewe kwa tamaa acha kulaumu watu mlaumuni yeye mwenyewe amechelewesha sana harakati
 
Father Kitima kashambuliwa na hakuna hatua yoyote imechukuliwa. Je na yeye kamtukana nani ili tuone huu utetezi wako una maana?
 
Waache wamtukane Mbowe ili zamu yao itakapofika tuwe tunawakumbusha!
 
Kwangu mimi kwa tabia ya Lissu alitakiwa akae sehemu sahihi zaidi ya mahabusu!
 
Kwendraaa zrakroooo unafurahia lisu kuka jela HUYO shahidi WA Siri unamjua. Pyeeeeeeeee
 
watu walimuonya Lisu kuwa hiki unachokifanya hakina afya kwa chama na wewe pia......... alijawa na ufahari/ukubwa akasahau kuwa bila Mbowe kulazimisha kupelekwa Nairobi angelikuwa historia leo. Yote hayo aliyasahau!
Lisu mwanasiasa mzuri, lkn hilo lilimshinda!
 
Jakaya kawa raisi wa Tanzania kwa miaka 10 Hana legacy? Anaheshimiwa? Kwann sasa?
 
Ni ngumu sana kwa sasa kumtetea uyo mzee, wenda ule msemo usemao mtu akizeeka anarudi utotoni ndo huu, mara kumi uyu mzee angeondoka zake akaa huko nje ya nchi ,tukajua moja kwamba hayupo nchini ,ameniboa sana uyu mzee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…