Chonde chonde viongozi wa CHADEMA; Tazameni hili kwa upana wake

Chonde chonde viongozi wa CHADEMA; Tazameni hili kwa upana wake

Father Kitima kashambuliwa na hakuna hatua yoyote imechukuliwa. Je na yeye kamtukana nani ili tuone huu utetezi wako una maana?
Yule ana skendo ya kuwa na mahusiano yasiyofaa na mke wa muumini, ndio maana hata wenzake wamemchunia
 
Mbowe kajivunjia heshima mwenyewe na kwa sasa siyo mwanachama wa Chadema tena amerudi CCM na wamempeleka Chaumma
1000046826.jpg
 
Kuna kitu mnakosea sana kukaa kimya na kuacha vijana wadogo kama akina Hilda Newton kumshambulia Mbowe na kumvunjia heshima kwa kiwango kikubwa, hii siyo sawa na haikubaliki hata kidogo na mbegu inayopandwa ni hatari sana.
Ukiangalia mambo yanavyoenda inaonekana kazi ya kulinda Legacy ya Mbowe ni kama anaifanya au kaachiwa Heche peke yake, huyu ndiyo pekee kidoogo anaonyesha Uongozi kwenye hili.

Tuchukulie sawa nyie mlioko Madarakani ni Miungu hamna madhaifu Mbowe yeye ana madhaifu, lakini kwa kuwalindia Chama hadi mnakikuta hapo kilipofika kiko Mioyoni kwa kila Mtanzania kweli anastahili kutukanwa kiasi hicho na mtu kama Hilda Newton ambae ameikuta CHADEMA imeshasimama na Mbowe ni kama baba yake?

Mbowe ameshakaa Jela mara ngapi kwa ajili ya hiki Chama halafu muulize Hilda ambae siyo Msaliti ufanye Comparison, kwanza huyu Hilda ha huyo Twaha Mwaipaya mimi binafsi nina mashaka nao mda mrefu sana kwa wanayoyafanya mbona hawajawahi kupata misukosuko yoyote ya maana kama wenzao?Siyo kina Zitto wengine hawa?

Kosa la Mbowe ni kuruhusu kutukanwa na yeye kukaa kimya na kulinda image ya Taasisi?Au kukubali kushindwa?

Ni aina Gani ya Siasa zinazofanyika leo hajafanya Mbowe?Kususia Uchaguzi?Kuandamana?Kuongea na Serikali?Kufungwa?Naona yote yanayofanyika ni marudio tu ila yalishafanyika huko nyuma kipindi cha Mbowe.

Naombeni sana Viongozi hata kama mna maumivu ya Uchaguzi jitahidini sana kulinda Legacy ya Mbowe katika Upinzani wa nchi hii, ntawaona wanafiki sana sasa hivi mkae kimya halafu siku ya kumuaga akiwa amelala mjitokeze na masuti yenu meusi kumpamba, natamani siku hiyo msiwe wanafiki mfanye hayahaya mnayoyafanya.

Mkumbuke Mbowe ni mstaafu mambo ya kumlazimisha afanye siasa au harakati baada ya kustaafu msiyalete humu, Povu Ruksa!
Hilda anyonyeshe mtoto kwanza.Aachane na siasa chafu za chadema
 
Katupotezea muda sana huyo jamaa na tunamsubiri apande jukwaani atajuta.
Mfikishie ujumbe.
NO Reforms sasa ni ya wanzania wote wenye akili timamu.

Utakuwa ni taahira kupanga foleni kuchagua mtu ambaye tayari washampitishwa na mifumo ya uchaguzi
 
Back
Top Bottom