Chongolo: Mbowe ana wajomba zake Nyeri na Zitto baadhi ya baba zake wanakaa Bukavu

Chongolo: Mbowe ana wajomba zake Nyeri na Zitto baadhi ya baba zake wanakaa Bukavu

Namsikiliza hapa Katibu wangu redioni anasema suala la Mama Samia kuwa na wajomba sehemu nyingine ya dunia sio kubwa Kama linavyotaka kuaminishwa.

Ameenda mbali na kusema mababu zake Zitto wakati wanahamia Kigoma wakitokea Bukavu DRC baadhi ya ndugu zao walibaki huko na wanatembeleana mara kadhaa.

Kwa Upande wa Mbowe amedai pia ujombani kwake Wana asili ya Nyeri nchini Kenya na hata akiwa Kenya huwa hakai hotelini, huwa anakaa nyumba za familia lakini bado alipata nafasi ya kuombea urais.

Amedai wapinzani wafanye kazi waache kutweet vitu vidogo vidogo.
Katibu mkuu bogus kuwahi kutokea
 
Hata mimi asili yangu, ni myahudi nina urefu wa futi 6...
Kuna shida ndugu zanguni jaman?
 
Hoja ndogondogo zinazidi kuwatoa kwenye njia kuu wapinzani. Wengi tu tuna asili za nje ya TZ na undugu wetu na kuliko asili yetu upo palepale. Tunataka hoja zitakazotuletea maendeleo.
 
Mnaosakama Magufuli kuwa ana ndugu zake Burundi na kuwa ni mrundi mumesikia? Benard Membe umesikia? Huna nduguzo Msumbiji? Unajitia mtanzania mzalendo wakati na wewe kwenu asili yenu Msumbiji
Sio kweli, anachokifanya unajaribu kubalansi tu story.
 
Hii nchi ina vituko,wengine mnasema Nyerere nae sijui ni mzanaki wa Kigali.
 
Zitto Mbembe wa kongo ana chama kinaitwa cha wazalendo wa Tanzania

Nape Nnauye na Membe wamakua wa Msumbiji kelele kibao Sisi ndio wenye nchi na chama wengine washamba tu watu wa kuja

Mbowe mkenya wa Nyeri ana chama chake Chadema

Wageni wanagombania utawala wa Tanzania
Nani ni mtanzania halisi

Kama vo kigoma tuirudishe Burundi
Bukoba,kagera tuirudishe Uganda
Moshi,arusha tuipe kenya
Mbeya,songea tuirudishe Malawi
Mtwara tuirudishe msumbiji
Kipande kitakachobaki ndy iwe tanzania halisi unaonaje mkuu

Ova
 
Hii nchi wenye haki ya kuimiliki wasio na mchangamano na mataifa mengine ni wagogo tu Hawa ndiyo wenye nchi
Sasa hao wakibaki itakuwa nchi tena
Marekani yenyewe wenye nchi ni red Indians tu,ila wote wahamiaji tu

Ova
 
Yaani Tanzania wahamiaji kuanzia wamakua wa Msumbiji akina Membe na Nape Nnauye na Wabembe wa kongo akina Zitto Kabwe nk ndio wanajifanya wazalendo sana kuliko wazawa
Kwa wafrika kawaida tu kuingiliana
Mkoloni si aliwagawa

Ova
 
Halafu bado mnawalipa TISS WA kazi gani sijui? Nawaambia siku zote taasisi yenye shida kubwa nchi hii si Polisi ni TISS. Kuwa kiongozi wa nchi si Jambo dogo, Leo tunafikia kuwa na Kiongozi wa nchi mwenye ukoo mkubwa nje ya nchi kuliko nchini. Tusisingizie Obama na Marekani, hao vetting yao Inajulikana ilivyofanyika na kabla hata Obama hajaja Kenya dunia yote ilijua kuna Bibi na shangazi yake. Leo Sisi tunashitukizwa Kwa ziara ya Kwa Mjomba?
Ukiona mzanzibari hana ndugu Oman basi huyo asili yake ni unywamwezi au msukuma...chill...kawaida sana...[emoji16]
 
Zitto Mbembe wa kongo ana chama kinaitwa cha wazalendo wa Tanzania

Nape Nnauye na Membe wamakua wa Msumbiji kelele kibao Sisi ndio wenye nchi na chama wengine washamba tu watu wa kuja

Mbowe mkenya wa Nyeri ana chama chake Chadema

Wageni wanagombania utawala wa Tanzania
Usimsahau Jiwe kwao Burundi...[emoji16]
 
Back
Top Bottom