mtu wa Kigoma muulize kabila akikwambia ni mmanyema huyo ukoo wake nusu uko Congo DR au Burundi!! Zitto hawezi kuwa exceptional! ukitaka kuamini chukueni simu yake muone wajomba zake wako wapi!!Mbona pale Kigoma sio stori watu wanaenda kwao DR Congo na Burundi na wa huko wanakuja Kigoma na maboti tu tena bila passport na wanakaa muda wanaotaka na kurudi kwao!
Ila turudi nyuma wa Kilimanjaro kwao Kenya, Mbeya sijui Mbamba Bay kwao nje, wa Ruvuma kwao nje, Tanga kwao nje, Rukwa kwao nje, Kibondo kwao nje, Bukoba kwao nje, Wajaluo?Wanyasa? Wamakonde? Wadigo?Wangoni?Barbaig? Wamasai kwao wapi? nusu ya ukoo zao ziko nchi jirani! Tanga watu wengi nusu ya ndugu zao wako Mombasa na ni raia wa Kenya!na sio stori Tanga mabasi kila siku yanajaza kwenda na kurudi Mombasa!!
Hivi nani ni mtanzania halisi? tuanzie hapo! labda mi naona Ndugai peke yake kutoka kwa wagogo walio katikati ya nchi ndio raia OG na ndo maana Ndugai ana uchungu wa kweli kweli na akakataa "nchi yake" isiuzwe kwa mikopo isiyo na mwelekeo!