#COVID19 Chongolo: Viongozi wa CCM wanaopinga Chanjo mchakato wa kuwashughulikia umeanza, hakuna aliye mkubwa kuliko chama

#COVID19 Chongolo: Viongozi wa CCM wanaopinga Chanjo mchakato wa kuwashughulikia umeanza, hakuna aliye mkubwa kuliko chama

Katibu mkuu wa CCM ndugu Chongolo amesema mchakato wa kuwashughulikia kinidhamu viongozi wa CCM wanaopinga chanjo kinyume na maele!ezkezo ya chama umeshaanza na karibu utakamilika...
Chadema wajitayarishe kuwapokea Pole Pole na Gwajima
 
Muulize mama D na Jumbe Brown siempre siempre
🤣🤣🤣
Chanjo ni HIYARI.

Mh.Katibu Mkuu Chongolo hajakwenda kinyume na msimamo wa serikali sikivu.

Msimamo wake kinzani ni kwa WALE WAPOTOSHAJI kuhusu chanjo.....wale wanaowaombea LAANA madaktari na manesi wetu wanaotuchanja.

Wale wasio na tafiti za kisayansi bali "blah blah" za "CONSPIRACY THEORIES" dhidi ya chanjo na kutaka watu wasichanjwe.

Salaam ndugu yangu Komredi YODA🙏
 
Yani mnaamua kuiua CCM kwa Sababu ya chanjo? This is very bad kwa kweli. Hivi mnajifunzaga kwa Nani? Duniani kote kuna Makundi yameikataa hii chanjo.mmesikia wakifukuzana?

Kwa taarifa yenu akipatikana mwanasheria nguli akaishtaki serikali hamtapata pakutokea. I tell you. Acheni kuisambaratisha CCM. Labda Kama kuna laana inawatafuna.
 
Ukada au uanachama wa chama chochote haujawahi kuwa muhimu kuliko afya ya mhusika.
Na hapa ndo tutawaona wanafiki wasioyaishi maneno ya vinywa vyao.
Na kwa msimamo huu wenye akili tumeanza kuelewa kwamba kumbe chanjo si hiari bali ni lazima.
Kumbe Polepole anayaishi maneno toka kinywani mwake?.
Hapa kuna watu wawili tofauti yule wa Tume ya Warioba na Katibu mwenezi wa chama.
 
Katibu mkuu wa CCM ndugu Chongolo amesema mchakato wa kuwashughulikia kinidhamu viongozi wa CCM wanaopinga chanjo kinyume na maele!ezkezo ya chama umeshaanza na karibu utakamilika...
Chanjo si ni jambo la hiyari!? Sasa kama wapo wale wenye kuhamasisha watu wenye hiyari wajitokeze kuchanjwa. Je! Kuna ubaya gani kuwepo pia watu wenye mtizamo tofauti kupaza sauti zao kuzipinga chanjo hizi?

Serikali ikubali tu imekuwa na msimamo uliokuwa kigeugeu katika suala hili la chanjo. Ukiangalia kauli za serikali mwanzoni mwa mwaka huu, kupitia kwa wataalamu hawa hawa wa afya walizitilia mashaka chanjo hizi na kutoa kauli ya kutaka kujiridhisha.

Leo serikali inabadili msimamo wake ghafla na kuonyesha kuzikubali, na hata kuonekana kulazimisha watu kuchanjwa kupitia kauli za viongozi wake. Ingawa imetoa tamko la uhiyari katika mtu kuchanjwa, lakini kupitia tamko hili la KM ni kwamba mtu mwenye kuonyesha kutokukubaliana nazo anaonekana ni mwenye kustahili kuadhibiwa.

Kuna nini nyuma ya chanjo hizi? Mbona inaonekana kama hakuna tena uhiyari katika kuchanjwa!? Kupitia msimamo wa Gwajima na Polepole nafikiri tutaweza kupata somo zaidi.
 
Mtifuano wa hatari,[emoji28]na Gwajima alishasema anasubiri mtoe majibu kuhusu chanjo ili awapige pigo moja msambararike jumla
 
Wametoa maoni yao kuhusiana na chanjo ya uviko -19,hakuna sehemu yoyote wamevunja katiba ya chama cha mapinduzi au ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Na hii inatokana na msimamo wa tume ilioundwa na serikali kupitia Rais Samia. Katika mapendekezo ya tume,tume ilipendekeza pia chanjo iwe ni hiyari kwa watanzania.

Je?kuweka msimamo wa mtu kuhusiana na kutochanja ni dhambi?,je maoni yao wangesema watachanja wangetishwa?,,

Nashauri CCM iheshimu maoni ya wanachama wake na si kuwatisha.

Chama hakijui kuna wafuasi wangapi dhidi ya wasiopenda kuchanja ambao wanaungana na kina Polepoke na Gwajima,

Mwisho, chama kisiingie kichwa kichwa huu mtego,au kama pengine ni njia tu ya kupitia kutimiza ajenda viporo nyuma ya pazia.
 
Chama kikubwa kuliko MTU.

Je kama sio MTU ndiye anayeabudiwa mbona Chadema kilitumia kauli hiyo ya chama kikubwa kuliko MTU kuhusu wabunge 19 wasio na sifa bungeni lakini CCM waliwakingia.

Je vilikuwa vikao vya chama au yalikuwa maagizo ya MTU.

Upi uhalisia wa CHAMA KIKUBWA KULIKO MTU
 
Hawana hoja yoyote hao akina Gwajima na Polepole ni wapumbafu tu, Sayansi huwa haina kubishana nayo, Sayansi siyo ulimwengu wa kiroho
 
Kwa hiyo chanjo ni maamuzi ya chama sio taifa?
Hili neno .Chama kinapoteza mwelekeo .Raisi kusema chanjo hiari maana yake Nini ruksa kukubali au kupinga

Chanjo ya corona haimo kwenye Sera au ilani ya CCM katibu mkuu go slowly please.

Chanjo italeta makundi ndani ya CCM na chama kugawanyika ndani kwa ndani

Safari hii haitokei Kama kipindi Cha Lowasa .mkitimua vinara wafuasi wao hawataondoka CCM watabaki ndani .Mziki 2025 .Mtatimua vinara lakini timu zao zitabaki ndani 2025 kitaeleweka Moto utawaka ndani ya chama
 
Wagome lkn wajue watawekewa sheria ya marufuku kufungia bungeni bila chanjo
 
Hawana hoja yoyote hao akina Gwajima na Polepole ni wapumbafu tu, Sayansi huwa haina kubishana nayo, Sayansi siyo ulimwengu wa kiroho
Sayansi huwa inabishiwa kila siku, ila ni kwa njia za kisayansi...na ndio maana tunazidi kusonga mbele...tatizo ni pale wanapobisha kwa kutumia wanacho amini !
 
Halahala CCM isije ikawa Zenji na huku Bara kiduchu. Katibu chanjo si ni hiari? Vipi tena imewadodea nini?

Bora angeendelea kupiga kimya angalau angetuficha kitu.
 
Back
Top Bottom