Hakuna undugu Kati ya mume na mke usijizime data.
Mke wako ndugu zake ni watoto mliozaa siyo wewe, Kwa akili hizi mtaendelea Sana kuteswa na wanawake maana hamuwajui.
Hosea 4:6a
" Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa"
Mithali 19:2 a
"Tena si vizuri nafsi ya mtu ikose maarifa"
Mkuu kuna Siri kubwa katika NDOA na Ndio taasisi ya kwanza MUNGU kuiumba kabda hata ya kanisa
mwazo 1:27
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke
aliwaumba.
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
MUNGU akawabarikia π aliwabarikia mwanamume na Mwanamke (NDOA) ina Maana aliibarikia NDOA na kuitiisha na na kuweka vyote alivyoviumba NDANI ya NDOA (mme na mke)
Baraka π ni Nguvu au UWEZO wa kufanikiwa na MUNGU aliweka Baraka katika NDOA yaani mme na mke b'se biblia inasema akawabarikia na sio akambarikia
Kusudi la MUNGU NDOA iwe MBINGU(pepo) ya duniani kama ilivyo kua pale edeni kabda ya anguko la dhambi MUNGU alikua akisema nao Adam na mke wake, alikua aliwatembelea na ndivyo inavyotakiwa kuwa kwenye NDOA za sasa B'se miguu ya MUNGU hapa duniani ni NDOA
Sasa imekua tofauti NDOA imekua vita, NDOA imekua jehunum, watu wanachinjana humo NDANI ya NDOA tatizo ni Nini?
Tatizo ni watu wanaingia katika NDOA harafu alieiumba NDOA wanamuacha nje na hizi ni NDOA ambazo ni mpango wa aduii shetani kuhalibu kesho ya mwanadamu
Mimi nakuhakikishia mkuu NDOA ambayo ni mpango wa MUNGU kamweeeeeeeeeeee haiwezi kuvunjika na amani, furaha, upendo, fadhili, utu wema, upole, KIASI vitatawala NDANI ya hiyo NDOA