Ni bahati mbaya sana hapa duniani kila mtu amekuja na karama yake (talanta) ambayo Mungu amekuumba nayo kwa kuifaidisha dunia hii. kama hautaitumia, au kama utaitumia vibaya, ipo siku kila mtu atatoa hesabu na kuhukumiwa sawasawa na namna alivyoishi hapa duniani kwa kile Mungu aliweka ndani yake. hii ndio sababu sio sisi wote waimbaji, hata tukijitahidi kuhubiri sio wote tunaweza kuhubiri sawa, Mungu ameweka kipawa kwa kila mtu kwa faida. ni sawa na gari, usukani una kazi yake na hautakiwi kuidharau breki, tairi zina kazi yake na zinahitajiana na injini n.k, kama una gari tairi zikawa zimepasuka hata kama ulizinunua, ni kuzing'oa na kuzitupa, ila haimaanishi kwamba hizo sio tairi, ni tairi ila zilizopasuka tofauti na vile ulivyotegemea ulivyozinunua, utanunua mpya na kufanya replacement. hiyo ndio hukumu yake.
Mungu amsaidie shusho, hakuna ubishi kwamba kwa wale wanaoijua historia yake ametoka very humble background, ni Mungu amemtoa toka kuuza nyanya na ndizi za kupanga barabarani na kutembeza karanga, (kwa mujibu wa maneno yake), kwa kipawa kile cha uimbaji, Mungu alimwinua hadi akawa hivyo alivyo. nilimsikia akisema kwamba anaijutia ndoa yake kwasababu aliolewa akiwa mdogo, hakuolewa akiwa na akili zake vizuri, ni kama Joyce kiria aliposema aliolewa miaka 8 na yule dj kwasababu alikuwa na shida na pesa ila hakumpenda dj. hili ni pepo moja limeingia wanawake wengi sana. imagine, alipokuwa anauza nyanya aliomba Mungu ampe mume, akampa tena mfanyakazi akamtoa kigoma huko akamleta dsm, akamsaidia akawa mwanamuziki, sasaivi amepata ameoga, anasema anajuta kuolewa akiwa hana umri wa kutosha. sawa na joyce kiria, alikuwa housegirl, akapanga alipiishia hela ya kodi na matumizi akaolewa na DJ, akakaa naye miaka 8 bila kumzalia kwa makusudi ati kwasababu alikuwa hampendi, aliolewa naye ili apunguze ugumu wa maisha, akaja kuachana naye kwa tarumbeta na msafara wa magari, kwa kumuaibisha kabisa, akapata talaka akaendelea kumwaibisha kwenye matv na mitandaoni. hawa ndio wanawake wa kisasa. mwanaume hajawahijibu, sawa na mchungaji shusho hajawahi jibu.
Enzi hizo mchungaji shusho alikuwa mfanyakazi mwenye pesa za mshahara, inasemekana wametofautiana miaka kumi na kitu kiumri, na kwa sasa bila shaka amezeeka na anaweza asimudu mahitaji? NO, hiyo isingekuwa sababu, kwasababu hata wanandoa wenye miaka 30s mmoja huwa anaweza kuugua au kupata ajali, ila wanavumiliana, kwenye ndo ausitegemee kwamba mtakuwa fit miaka yote. sisemi mchungaji sio fiti, NO, najaribu kuwaza kitu gani yule mchungaji amekosea hadi huyu anarukaruka na kina diamond namna hii, na yule kijana alishoot naye kenya alikokaa miezi kibao alimtolea shutuma nyingi kwamba alikuwa anamtaka, na alitoa shutuma kwamba anamloga. ziwe za kweli au sio za kweli ila kwa anayoyafanya nani asiamini allegations hizo?
shusho alikuwa na Mungu kabisa awali, na nyimbo zake zilikuwa za Mungu kabisa, ila amekengeuka, shetani amemwingia, kiburi cha pesa kimemjaa, alipokuwa Burundi akirekodiwa alisema alitoka kwao masikini ila alirudi kwao kwa ndege na akiwa na pesa ya kutosha bank. wanawake wengi wakipata huwa akiri zinawaruka, hapo amesahau yote mchungaji shusho alimfanyia, jinsi alivyovumilia kuoa mwanamke wa hali yake, akampa msaada hadi akawa mwanamziki akajulikana, sijawahi msikia ameappreciate hata siku moja.
NI hasara sana na huzuni katika kanisa. hata hivyo Mungu anampenda, anatamani arudi, na nafasi bado ipo, na afanye hivyo mapema kabla nyundo ya kuvunja tufe la kiburi haijashushwa, hakuna aliyeinua mabega kwa kiburi akasahau fadhili za Mungu aliyedumu, wote huwa wanaishia pabaya na kwenye majuto na kila mtu ataona ili iwe funzo kwa wengine. simuombei hayo ila historia kwenye Biblia inaonyesha hivyo, the more unaleta disgrace kwenye kanisa kwa kiburi baada ya Mungu kukufanikisha, the more unatengeneza mazingira ambayo utashushwa hadi chini hadi wote wajue ni Mungu amekushusha kwasababu ulimsahau. Mungu amsaidie.
kwa matendo yake anayofanya tangu kitambo, ni watu wangapi waliorudi nyuma kwa kumwangalia yeye kama kioo? kipawa chake cha uimbaji ambacho Mungu alimpa kilifanya wengi wamjue Mungu, kati ya hao ni wangapi wamerudi nyuma kwasababu yake? Hivyo kipawa chake cha uimbaji kimemwinua Mungu au kimefanya watu walitukane Jina la Bwana? hicho kipawa amepewa ajue ni dhamana, sio kwa aajili yake binafsi, ni kwa ajili ya kazi ya Mungu hivyo asilete hisia zake binafsi ambazo wakati anauza nyanya huko kijijini kwao sijui kigoma sijui wapi huko, hakuwa nazo na hakuota kama angekuja kuwa na kiburi cha aina ile. pia, ni wanawake wangapi wanafuata matendo yake na ndoa kuharibika na watoto kuwa bila familia kwasababu yake? ajue yeye alipewa kipawa hicho awe kioo na barua watu wengine wamsome na kumfuata Mungu, Joyce kiria tu amerudisha ndoa nyingi sana nyuma kwa ujinga wake walikuwa anausambaza channel ten, huyu pia ataharibu ndoa nyingi, wanawake wengi watamwiga na ni hasara kubwa sana.