Christina Shusho: Nilimuacha mume nitimize ndoto zangu

Christina Shusho: Nilimuacha mume nitimize ndoto zangu

asije kukudanganya mtu, Mungu alituumba na hisia kwa makusudi, na zipo miilini mwetu. kama ulivyo na hamu ya kula chakula, njaa inauma, hata tendo la ndoa kama umri wako unaruhusu kama kina shushu, utakuwa nazo sana tu. tunachoogopa, mchungaji mara nyingi kazungukwa na diamond na vivulana hivyo, msimtetee sana, video zisije kuja kumuumbua siku moja, sheteni ni mjinga ajabu huwa anakuvuta unafikiri upo salama kumbe anakutafutia kituko. mambo yote tunayofanya sirini kuna siku tu huwa yanawekwa peupe, na hii ni kwasababu Mungu ni wa kweli, sio fake, na njia zake huwa sio feki na haitaji wewe ufeki kitu alafu useme ni yeye.
Yuko wapi P.Diddy leo hii kila kona ya marekani wanaanika uchafu wake. Mashuhuda kibao ila ni mambo aliyafanya kwa siri kwa miaka mingi tu.
 
Hapana mzee sizungumzii malaya wadangaji. And lets not generalize.

Unaweza anza mahusiano na mwanamke ukakuta ana shughuli fulani na ana ndoto nayo ya kwenda nayo mbali. Sasa mwanaume ana muoa anakua abusive na anazuia plan zake kukua ambazo kimsingi ni za manufaa kwa familia yote. Dunia imeshuhudia mf historia ya Tina turner kwenye ndoa yake ya kwanza ilikua impoteze kwenye muziki. Wapo wanawake ambao waume zao wamewasupport wake zao na still ni respectful kwa ndoa zao, mf Yvonne Chaka chaka.
Je, ni wangapi hao? Mke ni partner wako hawezi kuwa na vitu vya siri ilihali nyie ni mwili mmoja.
 
Hii ni kauli ya dada mwimbaji wa siku nyingi aitwae Christina Shusho, "Kusema ule ukweli mimi niliondoka kwa mume wangu ili nianzishe kanisa langu, nilijiongeza ili ndoto zangu ziweze kutimia maana kama ningeendelea kuungana na mume wangu sehemu moja ningeendelea kudidimia.

"Siku hizi hakuna mambo ya mke na mume ni mwili mmoja!! hiyo haipo utapotea ndugu yangu, wewe na mume wako au na mke wako hamuwezi kuwa sawa, hiyo haipo kila mtu ana njia zake.

Na mimi siogopi watu nasema ukweli, haya ninayoyasema ndiyo yapo kichwani kwangu, huyu ndio mimi, kwanini niendelee kudanganya watu. Kwanza mimi licha ya kuwa Mchungaji lakini sipendi watu waniite Mchungaji Christina Shusho, sipendi na sitaki"
Tunaomba audio au video yake akisema hivyo na Sisi tumsikie vizuri
 
Uzuri ni mwanamke wa KIHA hao wakishajanjaruka na mji huwa wanapenda hela kinoma. Mostly huwa malaya tu sababu wanapenda kuhongwa.
Mwanamke wa kiha[majority] ni mvumilivu kinoma, ukiona amefika sehemu ya kudiss mme wake, basi yawezekana ni mzinguaji sana.
 
we dada unalinganisha vitu viwili visivyolingana. Shusho kama angekuwa na wito huo tangu mwanzo asingeingia kwenye ndoa, angeendelea na maono yake ya kumtumikia mungu, acheni kupotosha ukweli
Ndio unajiuliza alikuwa wapi muda kabla ya ndoa? Alikuwa na nyimbo kibao nzuri kwanini asingeanza huduma kipindi kile kile.😂

Deep down utagundua alikuwa na njaa na less connections.
 
Ni Kweli tumwombee arudi Kwa mstari,

Lakini akikataa, apumzishwe Ili asiharibu zaidi.
apumzishwe? Je kama ni mwanachama wa jamii ile inayotawala dunia kwa mlango wa nyuma atapumzishwaje, si utaishia kupambana na jamii hiyo kwa kumghasi mwanachama wao wanaomtumia kutekeleza ajenda zao?
 
Wamejivalisha ngozi ya Kondooooooo
Kumbe Ndani ni mbwa mwituuuuu

Anakuja kuharibu Sacrament ya Ndoa.
50 kwa 50 kumalamamake zao ashakuma siomatusi na hio 50/50 ndio agenda yao kuu all over the world muanzilishi Shetani Baba wa Uongo (soma historia ya Lilth) hata HUKO kwenye Ndoa hakuna mwili 1 wewe ulifikiri imekaa kisiasa tu mpaka makanisani HUKO mentality ni hio chukua 50 zako nichukue 50 zangu ndio zimekaa vichwani mwao waliowengi asikwambie nini sijui kimekua nini
 
Wakati ukute ndio mtu alomleta mjini 😆😆
Ukute amemtoa Kasuru huko porini.
Au kama wali kutana kimjinimjini hapo thawa.

Zamani wanaume walikuwa wanaoa makwao huko vijijini,
Mwanamke analeta hata ku-flush choo hajui anafundishwa, kutumia jiko la umeme hajui, usafi wa Nyumba kupiga deki hajui, kusafisha choo hajui, n.k

Yanni full mshamba.

Kuna wanawake wanaume zao wamewatoa mbali sana yawapasa kuwaheshimu na kuwashukuru siku zote.
Lakini sasa wakishajua ya mjini huwaambii kitu 👌👌😅
Mwanamke wa KiHA akishakujua mjini tamaa tamaa na ujuaji mwingi sana
 
Kwa hukumu zenu kumbe ndio maana wanawake wengine hung’ang’ania kwenye ndoa hadi kuuliwa, kuumizwa, kudhalilishwa kwa sababu wanaogopa kują kudhalilishwa na kutikanwa na wana jamii.
Badolini namna zenu za mitazamo.
What if kuondoka kwake ndio pina yake na salama yake kwa mfano?
Angesema anapigwa bila sababu tungeelewa. Sio eti unaachana na mume kwa ajili ya mwito wa Mungu halafu hapo hapo unapingana na taratibu za ki Mungu.
 
Yaaan mm always napenda mtu anayekuwa mkweli anayependa kuishi uhalisia wake haijalishi Nan atasema nn au jamii itamuonaje
Shusho na yy ni mtu tu ameamua kuwek Hisa zake juu ya ndoa yake na her next goals
Anaona kuwa ndoa inamkwamisha kwenye kufkia her goals so fu*k it away and focus on her goals that's itView attachment 2958717
Nitafutie IMAMU Mwanamke, Waislamu always wanaume Mbele wanawake nyuma popote utapokuta Waislamu wanawake nyuma wanaume Mbele na wanawake wa kiislamu sio visabengo wa kujiamulia Mambo kwamba na wao wanataka wawe Mbele sio nyuma, welcome to Taliban msiba wa Waislamu makaburini hukuti Mwanamke anatia udongo kaburini wanazika wanaume tupu Ila msiba wa kule kwa kinafulani yoyote anafanya anavyojisikia usishangae hata Ibada ya mazishi ikaongozwa na Mwanamke
 
Angesema anapigwa bila sababu tungeelewa. Sio eti unaachana na mume kwa ajili ya mwito wa Mungu halafu hapo hapo unapingana na taratibu za ki Mungu.
Hakuna Mungu anayevunja ndoa ili umtumikie. Huyo Kanogewa na umaarufu na kaona yule mmewe ni kama mshamba na mzee anataka aanze kuliwa na akina Diamond tu. Anatafuta justification sasa aonekane hajaolewa ili apigwe pumbu bila watu kuhofia kuwa yu mke wa mtu.
 
Je, ni wangapi hao? Mke ni partner wako hawezi kuwa na vitu vya siri ilihali nyie ni mwili mmoja.
Nilichosema, tatizo ambalo unalikwepa kulikubali, pia wanaume wapo wanaozuia plan za wake zao[ambazo ni za manufaa kwa familia] kukua.

Mimi nina mtu, yeye ni civil servant, tatizo lake ni mtu asiyejihangaisha kabisa, anaishi on his salary tu. Mkewe ni visionary sana, anahofia hatma ya familia maana hawajajenga, na wana watoto wa4, watatu wanasoma hizi english mediums. Fedha haitoshelezi maisha ya familia. Mkewe akaanzisha biashara ya sabuni za maji na unga. Mmewe akawa anachukua hela za biashara, kurudisha ni mbinde. Wameua mtaji mara tatu. Sasa hivi mwanamke ameanzisha biashara kwa siri. Unawezaje mlaumu huyo mwanamke?
 
Back
Top Bottom