luambo makiadi
JF-Expert Member
- Nov 28, 2017
- 10,602
- 8,798
@johnthebaptist umesikia?Nchi yetu bado ni masikini.
Uchagani masikini wapo lakini huwezi kulinganisha na mikoa mingine
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
@johnthebaptist umesikia?Nchi yetu bado ni masikini.
Uchagani masikini wapo lakini huwezi kulinganisha na mikoa mingine
Ulevi Ni starehe ya mtu,Kati ya ulevi na umalaya Ni kipi Bora? Hata Mimi huwa natandika bia Sana[emoji3][emoji3][emoji3] eti walevi ndo wana pesa hiki si kituko!!!! Mchagga akitoka kwenye mkoa wake huyo ndo amejinasua na ulevi otherwise uchaggani atakufa na ulevi. Ngoja tuwaambie waache uongo
Masikio ni matamu balaaa[emoji23][emoji23][emoji23] ukiyatafuna umachangamsha meno kweliKaribu shekhe Makame, tumekuwekea pua na ulimi meku, karibu sana kaskazini
Pombe wanakunywa bure?[emoji1][emoji1]Umaskini upo tena mwingi tu, mtu mlevi muda wote anapata wapi pesa??
MhhhhNa kwa takwimu Kilimanjaro ndo inaongoza kwa kufunga umeme wa REA vijijini, 85% ya vijiji vina umeme, imebaki 15% tu kumaliza vijiji vyote!
Nadhani itapendeza tukianzisha vuguvugu la kujitenga na Tanganyika, maana kilimanjaro na kaskazini kwa ujumla ni ardhi ya wastaarabu hatuwezi kuongozwa na Barbarian Meko wa Chato
CC kimsboy jibuMwaka huu niliamua kufanya tour trip huko Kilimanjaro ili kujifunza na kujionea shamrashamra za wachaga wakisheherekea sikukuu ya Christmas.
Mpaka sasa bado nipo Uchagani.
Nimefanikiwa kufika maeneo ya Rombo, Mwika, Marangu, Old Moshi, Kibosho na Machame. Sijafanikiwa kufika maeneo ya Kirua Vunjo na Uru. Kuna mambo mazuri sana na mabaya machache niliweza kuyaona, kwa mada hii leo hapa sitayazungumzia mabaya wala mazuri (nitakuja na mada yake baadaye nikikamilisha ziara yangu), bali nitazungumzia baadhi ya mambo yaliyokuzwa kuliko uhalisia wake.
1. Sio kweli kuwa karibu kila mchaga hurejea kwao kipindi hiki cha Kristmas. Ukweli ni kwamba idadi ya wachaga wanaorejea makwao kipindi hiki huenda haifiki hata robo katika Miji (namaanisha Boma la Ukoo lenye muunganiko wa familia kadhaa zenye kushare wazazi) niliyoweza kuipitia, zaidi ya 80% ya wauhusika hawakurudi kwao. Kuna maboma kadhaa yalikuwa yamefungwa kabisa, hakuna aliyerejea kabisa!
2. Sio kweli kuwa kila jamii ya kichaga kipindi hiki huweza kusheherekea Christmass kwa shamrashamra. Nimeweza kukutana na familia za wachaga waislamu (hasa maeneo ya Machame na Kibosho), jamii zingine maskini sana na familia nyingi zisizoeleweka nk, hao hawana muda wowote na sherehe za Krismasi. Wako busy na maisha yao mengine.
3. Misafara mingi ya magari binafsi yaliyokuwa yakielekea uchagani yalikuwa ni magari ya familia chache zenye uwezo mkubwa kifedha au maisha ya mbwembwe. Kifupi sana, magari yale huenda yanaakisi 10% tu ya familia za kichaga. Wengi wa wachaga wamekuja kula sikukuu kwa kutumia usafiri wa umma bila kujali kama wanamiliki magari mijini au hawana kabisa magari.
4. Sehemu kubwa ya miji (maboma) zimejengwa kwa nyumba za kawaida kabisa na nyingine ziko kizamani japokuwa zinaonekana kutunzwa vyema. Zaidi ya 90% sio nyumba za gharama kubwa au kisasa. Pia niliweza kukutana na nyumba duni au mapagala yanayoonekana kutelekezwa lakini nikakuta kuna watu wanakaa!
Ndo maana nikasema licha ya nauli kuwa kubwa kwa factor ya distance lakini wahaya wanapanda ndege wanenda home lakini nyie nauli ni visenti tu lakini mnatusumbua, hamuoni kuwa mmezidi ushambaSasa hayo si mambo ya Geographocal location mkuu? Mbona unabiangusha. Hata ingekua kagera iko kenta ndo imeshakua. Nauli ikiwa kubwa ndo nini sasa? Si kutokana na distance? Na mangarangara yenu[emoji23]
Weweeee Mimi wilaya zote isipokuwa ngara na kyerwa nimefikaKagera ni mapori??? Kumbe wewe umeishia biharamulo, hivi hujui kwamba Kagera ni ya tatu kwa population density nchini?? Je hao watu wanaishi wapi?? Kumbe ukiona mashamba ya migomba unadhani ni mapori, wilaya tu ya muleba ina watu zaidi ya laki saba, ukitoka muleba mpaka bk mjini zaidi ya km 80 ni makazi ya watu
Mkuu, achana na hawa washupaza shingo... uhalisia wa huko kwao twaujua na wa kwetu twaujua. Walishaufyataga zaman ni sasa hv tu wameamua kuamka tu. Hata mleta mada hajafika huko basi tu kaamua kuleta uzi tu ili mvurugano ila hakuna lolote. Katandike bia. Tandika bia. Ongeza pato la taifa. Maskini hawez kuntwa bia. Mbege yenyewe mpaka kuinywa ni gharama. Bohora moja buku mpk buku jero. Maskini atakunywaje. Hao walevi wanaokunywa 24/7 wanaokota hela kwani ili wanunue hizo pombe? Halaf kule watu hawalali njaa. Mikungu kibao ya ndizi. Chalari tamuuu..Pombe wanakunywa bure?[emoji1][emoji1]
Akiiba ndo anaenda kunywa pombePombe wanakunywa bure?[emoji1][emoji1]
Watalii huwa wanapanda private jet kwa % kubwa ,60% ni civil aviations upo?KIA hujui inahudumia mikoa mingapi na watu wanaokwenda huko si wanajulikana
Wewe Ni lay man huwez bishana na professional surveyorsYaani wewe unchokisema huna tofauti na uchumi wa kati wa Tz achana na makablasha watu tumefika tukajionea hakuna hicho unchokisema
Hahaha amepanic anaongea vitu amvavyo ni unknownSasa hayo si mambo ya Geographocal location mkuu? Mbona unabiangusha. Hata ingekua kagera iko kenta ndo imeshakua. Nauli ikiwa kubwa ndo nini sasa? Si kutokana na distance? Na mangarangara yenu[emoji23]
wahaya hawaishi kwenye center, hizo center ni kwa ajili ya kufanyia biashara ndogo ndogo jioni wanarudi vijijini ndo maana nikasema hupajui uhayani,Weweeee Mimi wilaya zote isipokuwa ngara na kyerwa nimefika
Ukitoa muleba _bukoba Centers ni kagoma,izigo,kaboya,kagondo tena vi Center vidogo vidog ukiangalia huku na huku ni miti na vichaka tu
Kwan wachaga hawapand ndege? Ndege zote zimejaa,mabasi,treniNdo maana nikasema licha ya nauli kuwa kubwa kwa factor ya distance lakini wahaya wanapanda ndege wanenda home lakini nyie nauli ni visenti tu lakini mnatusumbua, hamuoni kuwa mmezidi ushamba
Kwamba mnasumbuliwa? Mnasumbuliwa sababu ya nauli? Come on, you are better than this bwana. Ndege ndo hatupandi ama? Aiseee... halafu kwa kupenda kuchomekea watu wa Arusha ndo wanaopanda ndege[emoji23] mnaujua uchumi wa Arusha nani wameutengeneza? Hao wameru wenyewe ni wamachame waliopooza walihamia huko. Ndege zinapandwa. Binafsi napenda kusafiri kwa basi napata new friends kbs. Na naenjoy. Si kwamba hakuna private cars ama hatuafford hapana. Kwa ndege sioni kama ni adventure. Na watu kwenda kwao ni furaha. Excitements hizo. Hata wewe ukiwa unaenda kijijin kwenu lazima furaha iwepo kama mazingira ni mazuri. Yakiwa mabovu utafurahia nn? Na hapo kumbuka unaenda kukutana na ambao hukuonana nao mwaka mzima mnapishana ktk kupambania maisha.Ndo maana nikasema licha ya nauli kuwa kubwa kwa factor ya distance lakini wahaya wanapanda ndege wanenda home lakini nyie nauli ni visenti tu lakini mnatusumbua, hamuoni kuwa mmezidi ushamba
Nmeshamjibu huyo hata huku wahaya wa Mwanza wanasafiri sana kuliko waliopo Dar, the same kwa Wachaga waliopo Dar ukilinganisha na waliopo Mbeya, so factor ya nauli ni muhimu, nipo na mchagga hapa bk amekosa nauli hajaja hukoHahaha amepanic anaongea vitu amvavyo ni unknown
Kwa hela gani za kuibiwa? Watu bwana.Akiiba ndo anaenda kunywa pombe
Ukiangalia ratio ya makaz unakuta Ni scattered,sehemu chache ndio Kuna mwingiliano Mimi nimekaa miaka 3 kule hasahasa mulebawahaya hawaishi kwenye center, hizo center ni kwa ajili ya kufanyia biashara ndogo ndogo jioni wanarudi vijijini ndo maana nikasema hupajui uhayani,