Chumbani kwangu imepotea Tsh. 60,000 na ndani tupo wawili tu

Chumbani kwangu imepotea Tsh. 60,000 na ndani tupo wawili tu

nipo online

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2022
Posts
1,509
Reaction score
3,429
Wakuu polen kwa majukumu, naomba kuwajulisha changamoto niliyokutana nayo leo asubui, jana nimetoka nimeenda job, nimeacha elf 80 katika box dogo la mbao, leo asubui nakuta 20000, namuuliza wife na yeye anasema hajui.

Jana nilimwagiza achukue 2000 anunue kitu fulan, mimi nilikua mbali, ikumbukwe kua hiyo pesa ni hesabu ya saloon ya kuanzia jumapili to alhamis ya juzi.

Pia jana asubui hiyo hiyo nilimpa laki na 30 aweke sehem hiyo ipo yote lakini iliyopo katika box ndio imepotea hiyo elf 60.

Naomba nijifunze je, ni wezi? na kwanini abakishe? je chuma ulete kila siku naweka humo haijawai potea huu mwez wa 6 sasa, tafadhali naomba nijifunze, ni Mlipa zaka mzuri kabisa sijawai kengeuka katika hilo Asante.
 
Tuliza kichwa kama amewahi kuchukua basi ni yeye kama hajawahi kuchukua basi sie
Usifanye hitimisho haraka tena shirikiana nae kutafuta usipoipata piga kimya endelea na maisha
aliwahi chukua elf 20 ya kanisani nilipomwagiza apeleke kumbe nilisha piga simu kanisani kuwambia adi kais nikakuta pungufu hiyo ila nilimbana akarudisha
 
Hakuna uhusiano wa kutoa au kutokutoa zaka na kupotea pesa! Na kama unaamini kuna uhusiano, basi kupotea kwa pesa zako na huku ukiwa mtoa zaka mzuri basi kumethibitisha hakuna uhusiano.
namaanisha chuma ulete mkuu
 
aliwahi chukua elf 20 ya kanisani nilipomwagiza apeleke kumbe nilisha piga simu kanisani kuwambia adi kais nikakuta pungufu hiyo ila nilimbana akarudisha
Haya mbane tena huenda kachukua ila vitu kama hivyo ndio huanzisha migogoro ya ndoa
 
Vipi uchoyo aliacha kwanza?😅😅😅

Anyway, wanasema mchawi mpe mwanao akulelee.
 
Back
Top Bottom