Chuo cha Uhasibu Arusha chadaiwa kudahili Wanafunzi wengi kuliko uwezo wake, wengine wasomea na kuishi Hoteli ya Ngurdoto

Chuo cha Uhasibu Arusha chadaiwa kudahili Wanafunzi wengi kuliko uwezo wake, wengine wasomea na kuishi Hoteli ya Ngurdoto

Wameachiwa hadi fenicha!? Hiyo floor ya mbao itakunywa maji na kuoza. Jamaa atakuwa alikuwa desperate sana hadi kufikia uamuzi huo. Unawezakuta ilikuwa iwe hostel apate ya kulipa madeni au iuzwe.
Yani inabidi aweke housekeepers na mwanafunxi atakaeharibu chochote ni lazma alipe. KILA siku pawe panakaguliwa.
 
Hii ndio taarifa ya sasa na ya kushangaza inayozunguka Tanzania mpya yenye uchumi wa kati , kwamba Hotel ya nyota 5 iliyo kwenye kitovu cha utalii Arusha , imefikia makubaliano na uongozi wa chuo cha Uhasibu ili kufanywa malazi ya wanafunzi ! kiukweli hili jambo linafikirisha haswa .

Nakulilia Tanzania .
hotel ya Ngurudoto ilitumika kama chuo toka enzi za Kikwete pia

chuo kikuu cha Garisa Kenya kiliposhambuliwa na magaidi wanafunzi walihamishiwa Hoteli ya Ngurudoto kuendelea na masomo
 
Mkuu utalii na watalii wanahusika na nchi nyingi sana mkapa afike na kuondoka Tanzania... Na nchi nyingi (source markets) bado Covid-19 inazidi kushika kasi...
So biashara ya utalii si direct kama kupanda daladala za makumbusho mawasiliano...
Arusha kama Arusha ni mji ulioathirika kiuchumi kupita miji yote (isipokuwa Unguja na Pemba) kutokana na kudorora kwa utalii...
Sasa hao watoto wengine hawajui kutumia vyoo vya maji si wanakwenda kuvunja vunja miundo mbinu ya vyoo?
 
Kweli kabisa. Kama hii familia ingeshauriwa vizuri hizo property wangetafuta management Kama doorways, serena , sheraton, wakazirun wao wakawa wanapokea gawio. Kugawa a mali za hivyo ni ushamba wao wangekia tu gawio linapotoka wao wanalipwa mshahara. Hivyo wangeendelea bila stress
Hiyo familia Wana njaa
Kila mtu anataka hela aFanye mambo yake
HaWana umoja kabisa

Ova
 
Uchumi wa kati ni pamoja na wanafunzi kulala sehemu nzuri,

Sehemu nzuri zilikuwa zinalaliwa na majizi na mafisadi

Sasa ni muda wa majizi na mafisadi kuisoma number na kuishi kama mashetwani

Kwani kuna dhambi gani watoto wako kulala sehemu nzuri?.

Eti msomaji unaesoma hapa, wewe hupendi mwanao alale sehemu nzuri?

Sio kila jambo ni kupinga pinga tu,, mjifunze kuwa alie juu saa yoyote ataporomoshwa
Ni hayo tu
Kuna faida zake kulalia mahali pazuri...au nasema uongo ndugu zangu?
 
Uchumi wa kati ni pamoja na wanafunzi kulala sehemu nzuri,

Sehemu nzuri zilikuwa zinalaliwa na majizi na mafisadi

Sasa ni muda wa majizi na mafisadi kuisoma number na kuishi kama mashetwani

Kwani kuna dhambi gani watoto wako kulala sehemu nzuri?.

Eti msomaji unaesoma hapa, wewe hupendi mwanao alale sehemu nzuri?

Sio kila jambo ni kupinga pinga tu,, mjifunze kuwa alie juu saa yoyote ataporomoshwa
Ni hayo tu

nimecheka sana[emoji23]
una akili za jiwe yani umepita mule mule
 
Mitano tenaaa, na akimaliza hii mitano inabidi alazimishwe aendereee manake akiondoka hatutapata mwingine kama hyu. [emoji4]
 
Maisha ni pedeli ya baiskeli. Ikiwa juu baadae inaenda chini. Jambo muhimu maishani ni kuwa mvumilivu

mkuu, kwa muktadha huu pedeli imenyofoka kabisa sio kushuka
yani imagine mwanafunzi mmoja analipa laki mbili na hamsini kwa semister ,nadhani hapo watalii walitoa hata elfu 50 kwa siku kwa mtu mmoja
 
Kutokana na changamoto ya kibiashara katika sekta ya utalii uongozi wa hoteli yenye hadhi ya juu ya kitalii wameamua kuigeuza hoteli hiyo kuwa hosteli kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali vilivyopo Arusha.

Hoteli hiyo ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 2000 hivyo kuingiza mapato ya zaidi ya 70 milioni kwa mwezi.

Hoteli hiyo ilifungwa zaidi ya mwaka kutokana na changamoto za biashara.

Chanzo: Clouds Radio
Hesabu zako hazipo sawa.

Hawa wanalipa 400k kwa mwezi.
Kama wanafunzi wapo 2000 maana yake kw mwezi wanatengeneza mil 2
 
Huwaga unaubishi wa kijinga Ngurudoto ni swala la management ndo inshu nawewe Kama mdau ws JF humu Kuna mada nyingi sana zinavyoelezea jinsi warithi wanavyofuja Mali na kusahau kuwekeza kwenye uzalishaji
aliyeshindwa kuendesha anawezaje kuingia mikataba na chuo cha uhasibu ?
 
Arusha. Hoteli ya kitalii ya Ngurdoto mountain lodge yenye hadhi ya nyota tano iliyopo wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha, imegeuzwa hosteli ya chuo cha Uhasibu Arusha baada ya kufungwa kwa siku kadhaa kutokana na ukosefu wa wateja, baada watalii kutoka nje kupungua kutokana na janga la ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19 duniani.

Hoteli hiyo ilikuwa ikimiliki na mfanyabiashara, Melau Mrema aliyefariki mwaka Agosti 2017 na wanahisa wengine,ilifunguliwa rasmi mwaka 2003 ikiwa na vyumba 300 ikiwemo vya kulaza wageni wenye hadhi ya wakuu wa nchi saba na wasaidizi wao.

Hoteli ya Ngurdoto itaendelea kukumbukwa kutokana na kupokea wageni kutoka maeneo mbalimbali duniani katika mkutano wa Sullivan mwaka 2008.

Pia kipindi cha awamu ya nne, hoteli hiyo ilitumiwa na Serikali kwa kufanyika semina elekezi kwa viongozi wote walioteuliwa wakiwepo mawaziri, makatibu wakuu na watendaji wengine.

Ngurdoto pia itakumbukwa kama hoteli pekee iliyokuwa ikifanyika mikutano ya wakuu wa nchi za Afrika ya Mashariki hasa kutokana na kuwa na vyumba maalumu ambavyo vilikuwa na uwezo wa kulaza marais na kuwa na kumbi kubwa zenye uwezo wa kuchukua zaidi ya wajumbe 2,000 wakati mmoja.

Akizungumza na Mwananchi jana, Mkuu wa chuo cha Uhasibu Arusha, Profesa Eliamani Sedoyeka alithitisha chuo hicho kukodi hoteli hiyo na sasa zaidi ya wanafunzi 1,000 wamepata sehemu ya kulala.


ngurdoto-pic.jpg
 
Wakuu hii kitu imekaaje?

Hotel kubwa kabisa nchini ya hadhi ya nyota 5 imeyumba au kuyumbishwa toka 2016 na sasa imebaki historia.

Je, serikali haina mpango au mkakati wa kusimamia miradi mikubwa kama hii inayolipa kodi na kutuingizia fedha za kigeni kuendelea kuishi?

Je, sekta binafsi zipo katika hali gani maana ni kama sera zetu hazieleweki zinalindaje mitaji ya wawekezaji. Tuchukue hatua tuimarishe sekta binafsi kulinda Ajira za watu wetu. Hii n Aibu Kubwa kwa Nchi.
 
Back
Top Bottom