Arusha. Hoteli ya kitalii ya Ngurdoto mountain lodge yenye hadhi ya nyota tano iliyopo wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha, imegeuzwa hosteli ya chuo cha Uhasibu Arusha baada ya kufungwa kwa siku kadhaa kutokana na ukosefu wa wateja, baada watalii kutoka nje kupungua kutokana na janga la ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19 duniani.
Hoteli hiyo ilikuwa ikimiliki na mfanyabiashara, Melau Mrema aliyefariki mwaka Agosti 2017 na wanahisa wengine,ilifunguliwa rasmi mwaka 2003 ikiwa na vyumba 300 ikiwemo vya kulaza wageni wenye hadhi ya wakuu wa nchi saba na wasaidizi wao.
Hoteli ya Ngurdoto itaendelea kukumbukwa kutokana na kupokea wageni kutoka maeneo mbalimbali duniani katika mkutano wa Sullivan mwaka 2008.
Pia kipindi cha awamu ya nne, hoteli hiyo ilitumiwa na Serikali kwa kufanyika semina elekezi kwa viongozi wote walioteuliwa wakiwepo mawaziri, makatibu wakuu na watendaji wengine.
Ngurdoto pia itakumbukwa kama hoteli pekee iliyokuwa ikifanyika mikutano ya wakuu wa nchi za Afrika ya Mashariki hasa kutokana na kuwa na vyumba maalumu ambavyo vilikuwa na uwezo wa kulaza marais na kuwa na kumbi kubwa zenye uwezo wa kuchukua zaidi ya wajumbe 2,000 wakati mmoja.
Akizungumza na Mwananchi jana, Mkuu wa chuo cha Uhasibu Arusha, Profesa Eliamani Sedoyeka alithitisha chuo hicho kukodi hoteli hiyo na sasa zaidi ya wanafunzi 1,000 wamepata sehemu ya kulala.
Hoteli hiyo ilikuwa ikimiliki na mfanyabiashara, Melau Mrema aliyefariki mwaka Agosti 2017 na wanahisa wengine,ilifunguliwa rasmi mwaka 2003 ikiwa na vyumba 300 ikiwemo vya kulaza wageni wenye...
www.mwananchi.co.tz