Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) chamsimamisha Mhadhiri kwa tuhuma za ngono

Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) chamsimamisha Mhadhiri kwa tuhuma za ngono

Mswahili analeta uswahili wa kipumbavu,anashindwa kutafuta michepuko kwa mshahara wake
Tukienda nje ya maadili, rushwa ya ngono ina raha yake kisaikolojia kwa anayepewa nyie!

Ina izidi rushwa ya pesa kwa mbali vibaya.

Namna inavyotolewa ndiyo vichekesho, yaweza kushawishiwa kwa kuombwa ama ikashawishiwa kwa kutolewa!

Sasa mimi nipo na hii ya ya ushawishi wa kutolewa na siyo kuomba!

Mshawishii wa kutoa hujiandaa kwa mzunguko mzima hadi zoezi lote litakapo kamilika, yaani kuanzia chumba, usafiri, vinywaji, pocket money na mwili .

Yaani mpokea rushwa ya ngono huwa ni mnufaika wa mambo mengi sana kwa mkupuo kumzidi marioo anayelelewa na jimama rasmi.

Halafu akishapokea hiyo hongo hujiona kadume ka mbegu kajanja kuliko wanaune wote kudadeki!
 
Mbona ma lecture wengi ni madomo zege ...huponea kwa vidada ambavyo havijielewi kwa kushikwa sup tu kamevua ngua...
Harafu hao malecture tabia zao utaona kwenye milango ya ofisi zao ...

Tangazo
Muda wa consultation ni kuanzia saa 13:00 PM mpaka saa 18:00 sasa fatilia hiyo consultation wanakuwa wanapiga migegedo tu mabinti......
Ila jinsia ya kike inatabu kwenye Vyuo, ajira, bar, majumbani
Hakuna 13:00pm Wala 18:00pm
 
Chuo kikuu cha Dodoma kimeanzisha mchakato wa hatua za kinidhamu na maadili kulingana na Sheria na kanuni za utmishi wa umma.

UDOM imesema mtumishi Petro Bazil alisimamishwa majukumu yake tangu Oktoba 25, 2021 hadi uchunguzi utakapokamilika. Udom imesikitishwa na usumbufu uliojitokeza.

Pia, soma=> UDOM: Wanafunzi wamkamata mkufunzi anayewapa 'Sup' ili afanye nao ngono

View attachment 1989670
Huyu si wa kusimamishwa tu bali kufukuzwa na kushitakiwa. Hana elimu yoyote wala utu. Ni limbukeni na mshamba wa kawaida aliyechelewa kukua na kukataa kuelimika
 
Tuende mbele na turudi nyuma, swala la utelezi limekuwa tatizo sana

Wanawake naomba mjadiliane vizuri ili utelezi uwe wa kutosha mtaani
 
Mimi nashangaaga sana mtumishi ambaye ni kijana na sio mzee kupata msala wa ngono na mwanafunzi wake wa chuo.

Msomi mzima mwenye kazi yenye mshahara net around milion 2. Unashindwa kumtongoza binti under 25 akupe mwenyewe. Yaani huwezi kumpata binti uliyemzidi akili, pesa, umri na kila kitu mpaka umtishie kwa sup.

Wasomi mnakwama wapi kwenye kutongoza.

Mbona mishen town wa mtaani wanawala sana hao mabinti,, ama hata wafanyakazi wenye kazi zenye mshahara mdogo kama wafanyakazi wa kwenye branch za ma benk wanawala sana hao watoto bure.

Msomi mzima ,,,,,Yaani college girl huwezi kucheza na saikolojia yake mpaka akupe mwenyewe na bonus akupe kama akufulie na nguo na kukupikia
Vijana hawa wa shule za kata(miaka ya 2000) hawajui hata kutongoza.
Mfano halisi ni "anayedaiwa" kuwa shahidi wa kesi ya Mbowe,bwana Kaaya.
 
Huyo binti sio mjinga kuandaa mpaka watu wa kufumania...
kaanda watu wa kumfumania kitandani au kumfumani akimtongoza kwa kigezo cha kupasishwa chuo ?

the former is not a crime

na barua yenyewe imeandikwa kana kwamba keshahukumiwa... na imeandikwa na kitengo cha huduma za masoko... Chuo Kikuu kina kitengo cha masoko utadhani wanatatoa huduma za Tigo...
 
Hili swala ilibidi TAKUKURU ihusike.

Afikishwe mahakamani.

Akikutwa na hatia chuo nacho kitatoa adhabu yake.
Unamwomb fisi alinde bucha?
Hebu fuatilia fisi nyendo zake, ndio umpe bucha; weleedi si kwenye kipimo cha ngono pekee, issue ya kura zza uchaguzi kuibwa wakae kimya ndio suala la ngono wataongea, kila mtu achukue hatua achana na hao unao wataja.
 
Avumaye baharini ni papa, wengine wapo, huu ufuska upo mpaka vyuo vya kati, sekondari na msingi mambo haya yamedhibitiwa kwa nguvu kubwa sana za kiutumishi na kisheria kule chini visa hivi vimetulia vimeibukia huku juu kwa kasi kubwa kana kwamba hawa mabinti walisubiriwa wapande juu na nguvu ya kisheria ipungue kuwalinda ili washughulikiwe kwa hamu kubwa kama watu wazima. Mwanafunzi mtu mzima ana mahitaji mengi ikiwemo hitaji la penzi.

Tatizo ni approach yake kufanyika katika mazingira yasiyo muafaka hata kama kuna makubaliano mujarabu itaonekana ni rushwa ya ngono tu.

Huyu mkufunzi hakusoma saikolojia ya mahusiano ya kimapenzi kulingana na status yake na exposure aliyonayo.

Hilo jambo lingefanyika vizuri tu nje ya mukhtadha wa kazi yake hata kama angetaka kuwabumunyua wanachuo wote wawe wapenzi wake.

Kuna udhaifu mkubwa kwa pande zote wanafunzi na wakufunzi kama ni hukumu ipite kwa wote.

Wanafunzi wa chuo kikuu ni watu wazima wana utashi na uamuzi wa kufanya jambo kwa usahihi. Huyo mkufunzi apewe onyo tu
 
MHADHIRI WA CHUO CHA U-DOM ASIMAMISHWA KWA RUSHWA YA NGONO

Chuo Kikuu cha Dodoma kinapenda kutaarifu Umma kuwa mnamo tarehe 25 Oktoba, 2021 kilipokea kwa masikitiko makubwa taarifa za tuhuma dhidi ya Mtumishi wake ndugu Petrol Bazil, Mhadhiri Msaidizi juu ya kujihusisha na rushwa ya ngono kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma. Baada ya kupokea taarifa hizo, Chuo kimeanzisha mchakato wa hatua za kinidhamu na maadili kulingana na Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma.

Aidha, mtumishi huyu alisimamishwa kufanya majukumu yake yote yakiwemo kufundisha kuanzia tarehe 25 Oktoba, 2021 hadi uchunguzi utakapokamilika.

Chuo Kikuu cha Dodoma kimekuwa kikichukua hatua stahiki za kinidhamu kwa mujibu wa Sheria na Taratibu za Utumishi wa Umma bila kumuonea mtumishi yoyote.

Aidha, Chuo kinapenda kuutaarifu umma kuwa kitendo hiki hakivumiliki wala kukubalika na kwamba wakati wote Chuo kitaendelea kusimamia nidhamu na maadili kwa watumishi wake wote. Pia, Chuo kitaendelea kuchukua hatua kali kwa mtumishi yeyote atakayebainika kujihusisha na makosa ya kinidhamu.
Chuo kimesikitishwa sana kwa usumbufu uliojitokeza.

MHADHIRRI.PNG
 
Hayo yatafahamika baada ya uchunguzi kukamilika. Kwa mfano huenda wakina dada waliodhurika ni wengi. Uchunguzi utabaini hilo.

Pia huenda wengine walikataa ombi wakafelishwa. Hao nao itabidi wafikiriwe wapozwe vipi. Ili mradi basi yote hayo ni baada ya uchunguzi kukamilika.
wangeenda mbali zaidi wampime huyo mwanataaluma kama ni mzima au ana maambukizi ya ukimwi ili adhabu kali ichukuliwe zidi yake.
 
Kama ni ile video... Probably pale Ni geto kwa demu... Na inavyoonekana jamaa walimuona hivyo wakavizia aingie ili nao waingie ili mfumanie... + Kisasi cha usaliti wa mapenzi (mahusiano)
Kwenye hiyo clip nilisikia kama demu analalamika 'si haki, si haki' nafikiri ni kama fumanizi lililotokana na kusalitiana kwenye mahusiano. Hivi vitoto vya chuo vitakuwa pia vinatoka na wahadhiri kwa sababu wana mshahara na life zuri hivyo kuweza kupelekea kuzungukana na hivyo kupelekea hivi visa vya fumanizi uchwara vinavyobandikwa kilemba cha rushwa ya ngono kama njia ya kukomoa. Inabidi UDOM waliangalie kwa jicho la tatu swala la huyu muhadhiri. Badala ya kufikiria rushwa ya ngono tu wangejitahidi pia kufuatilia tabia na mienendo ya hawa mabinti wawapo chuo kwani wanachukuliwa kama watu wazima......​
 
Amesimamishwa wakati uchunguzi unaendelea. Mara baada ya uchunguzi kukamilika, hapo ndipo hatua stahiki zitachukuliwa kufuatana na maelekezo ya kanuni za utumishi.
Tatizo, ni kwamba anaweza akafukuzwa kazi halafu akapata kazi kwenye private institutions na kuendelea kuchafua hali ya hewa. Sijui kama taasisi ya Elimu ya juu inachukua hatua kama za Wizara ya Afya kwa wale wanaokosa maadili ya kitaaluma.
 
Back
Top Bottom